Kuna taarifa zenye utata ya kuwa viongozi wa Iran wamesemea hawatoi msaada kwa Hamas eti kwa vile hawakuwaeleza mapema kuhusiana na shambulio lao la okotoba 7.
Hizbolah nayo ya Lebanon iliwahi kusema haikuhusika na taarifa kuhusiana na shambulio la oktoba 7.Mpaka sasa hakuna aliyesema kwamba aliwasaidia Hamas kwa namna yoyote ile katika kupanga na kutekeleza shambulio lao hilo.
Hiyo ni habari njema kwa wale wanaokuwa kwenye shida kubwa za maisha.Usiwe unalialia tu bila kuchukua hatua za kujinasua kwa nafsi yako.
Na kwa ujumla hiyo ndiyo kanuni muhimu ya maisha kila mtu huipenda aione kwa mwenye shida.Hata benki huwezi kulala nyumbani mpaka ukaota ukurutu halafu unakwenda kupeleka barua upewe mkopo.
Serikali nyingi hupenda kusaidia wananchi waliojikushanya kushughulikia changamoto za maeneo yao kabla ya kuomba msaada serikali kuu.
Ukiwa na fedha za kusaidia watu pia usiwe unatoa pesa kwa omba omba wa mitaani.Tafuta mwenye akili aliyeanza kuuza hata vitu vya mkononi.
Hamas wameonesha mfano kwa kujisaidia wenyewe kwenye shida zinazowakabili wao kwanzo japo zinawahusu na wengine duniani.Hawakuwa na sababu ya kuomba ruhusa kwa yeyote wala kutoa taarifa ya mipango yao.
Inajulikana kuwa Gaza imekuwa kama Gereza kwa muda mrefu.Kila kinachoingia lazima kipitie mikononi mwa Israel na kibaraka wao Misri.Katika hali hiyo wamekuwa wakitumia chuma chakavu na mabaki ya makombora ya Israel kujiundia makombora yao hatua kwa hatua mpaka yamefikia kuruka mpaka Tel Aviv mji mkuu wa Israel.
Sasa kama kuna anayewalaumu au kufanya nongwa kwamba hakujulishwa Hamas wanaweza kumwambia nenda zoko huko.
Kama waweza kutusaidia fanya kama wajibu kwako na kama hutaki tuwache na Mungu wetu.