Kama ni bibi yako ungemsaidiaje?

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Jul 22, 2011
3,752
5,497
Ahsante
 

Attachments

  • chama.jpg
    chama.jpg
    35.2 KB · Views: 112
Ningemsaidia sana,lakini nina uhakika kuwa msaada wangu ungeniletea matatizo ikiwamo kushambuliwa na wananchi wenye hasira na hata kupelekwa jela.Kwa sababu ningeuchukua mkongojo wake na kumcharaza bakora kama tatu hivi za harakaharaka,nashukuru sikuwepo eneo hilo...
 
Ningemuogesha maji ya moto na kuyachoma moto haya magamba aliyovaa na kumpa nguo zinazoendana na umri wake ila si hizi, kisha ningempaka lotion na perfume aendane na umri wake. Usije kukuta huyu bibi ana miaka 50 (kijana sana), ila amezeeka kutokana na matatizo anayopatiwa na TANU/CCM toka enzi na enzi. Ningemuelimisha ya kuwa toka tupate uhuru wakati wewe bibi uko kijana mpaka hivi sasa kuna maendeleo gani uliyoyapata baada ya kuongozwa na hawa wahuni? Najuwa atanijibu hakuna, huku akilia na kamasi likimtoka. Nami nitamwambia pole bibi, sasa kuna faida gani mzee kama wewe na jua hili unakwenda kuhudhuria mkutano wa wahuni wa nchi, huoni kama ni upuuzi? Kuna jambo gani la maana watakalokuambia ambalo wewe hujalisikia toka enzi hizo? Atazidisha kulia, nitamwambia sasa wakati muafaka umefika, vua hizi nguo na tuzichome moto mbele ya vuvuzela na umpe yako ya moyoni kwanini umechukua hatua hii. Atafurahia na kuniambia kuwa wewe ndo mjukuu pekee nikupendaye, wenzako wote wameridhika na ujinga wa nchi hii wewe tu ndiyo umeweza kuona mbali. Mungu akulinde mjukuu wangu ila usije kugombania urais ama ubunge katika nchi hii watakuua wenzako kwa uchungu ulionao kwani hapa hawapendi watu kama wewe. Wanataka watu wahuni na wapuuzi ili nchi iendelee kuomba msaada nje huku viongozi wakijitajirisha wao na familia zao. Ahsante sana mjukuu wangu. Mungu akulinde!
 
Back
Top Bottom