Nyarupala
JF-Expert Member
- Jun 2, 2024
- 641
- 1,055
Uhali gani mwanaJamii Forum?
Nimekaa hapa geto kwangu nikawa na-review matukio ya kwenye historia niliyoanza kuisoma tangu mtwivila primary school, Tegeta secondary school, na Lufilyo high school ambapo baada ya hapo niliamua kuachana na hili somo nilipofika chuo kikuu na kilichosababisha ni baada ya kuona kwenye Ile course ya BAED Kuna watu nyomi sana, na mimi nilikuwa na tabia ya kutokupenda kujazana darasani.
Baada kusoma history kwa muda huo mfupi nimegundua kwamba; kama kweli Mungu yupo, basi yeye ndiye aliyeruhusu Afrika kutawaliwa na Wazungu pamoja na Waarabu.
Kwanini nasema Mungu aliruhusu sisi kutawaliwa?
Afrika hapakuwa na sayansi na teknolojia inayoendana na mahitaji ya Waafrika wenyewe, ni kweli kwamba kabla ya ukoloni Afrika ilikuwa na sayansi yake pia na teknolojia yake katika namna ya kukidhi mahitajio ya watu wa jamii ya kipindi kile. Lakini teknolojia ya sisi Waafrika kabla ya kuja kwa wazungu isingeweza kuendana na mahitaji ya watu wa Karne ya leo, yaani kwa namna nyingine naweza kusema mahitaji ya huduma zetu yangekuwa makubwa kuliko kile tunachohitaji kutokana na udunu wa teknolojia na hivyo Mungu akaona Kuna haja ya sisi Waafrika kutawaliwa kwa lengo la kushare Yale mazuri ya wenzetu wazungu.
Teknolojia ya mkoloni ilileta muunganiko kwa watu kati ya Afrika na dunia nzima kwa ujumla. Kwa mfano kwa kutawaliwa kwetu sasa viwanjwa vya ndege vilijengwa, relief zilijengwa, bandari zilijengwa na barabara pia zilijengwa ambapo zimefanikisha hadi leo hii tuna mahusianoazuri na haohao wakoloni kupitia biashara, Elimu na siasa. Lakini kwa udhaifu wa teknolojia yetu Waafrika ungeweza kukuta tu hata kufanya utafiti wa sehemu ya kujenga bandari ingekuwa tatizo.
Bila mkoloni Afrika tungefutika kwa magonjwa . Magonjwa kama haya yanayosababishwa na wanyama kama ebora, mpox na mengine mengi yaliyowahi kutokea yangetumaliza kutokana na udhaifu wa kiteknolojia wa sisi Waafrika wa kugundua aidha chanjo au dawa za magonjwa husika na ndyo maana Mungu aliamua na sisi tuipate au tunufaike na teknolojia ya wazungu kupitia ukoloni.
Nb:
Masuala ya kusema eti kabla ya Karne ya 15 Afrika na ulaya zilikuwa sawa kimaendeleo jamani binafsi naona hizi ni stori za kubuni tu kama stori zingine.