Kama Mtume Paul aliweza kuwatangazia watu wa mataifa na kuwabatiza kuwa Wakristu bila tohara kanisa liruhusu ndoa za wake wawili kuepusha michepuko

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,593
215,347
Sikuhizi kuwa na mchepuko ni kitu cha kawaida sana. Hasa kwa wenye ndoa za mke mmoja. Mchepuko anapata mahitaji yote lakini hajulikani kwenye ukiona.

Si jambo la kushangaza unakuta mama anamuona mwanaume J3 mpaka Ijumaa akitoka kazini lakini saa tatu lazima awahi kwa mke wake.

Mchepuko asipomuona mzee, dereva atatumwa apeleke mahitaji lakini haruhusiwi kupiga simu aulize mzee yuko wapi. Ikitokea amepata ajali au kifo, watoto wanapata tabu. Si ajabu mama ni hana njia yeyote ya kuingiza kipato.

Kanisa lifikirie jinsi ya kuokoa roho za waumini hawa kwani wengi tu wanaishi kwa dhambi.
 
Mkuu kwa wanawake wasasa mchepuko haukwepeki.. Ila jambo la kuangalia ni mchepuko aina gani unao??
Kuna baadhi ya michepuko ni ya faida mchepuko anakupa ushauri mnafanya jambo la maana na sio kwa maslahi yake tu Bali kwa maslahi ya pande zote
 
Mwanaume kuepuka kuchepuka yakupasa ujifunge kibwebwe haswaa.

Inabidi waafrika kwenye mambo ya mahusiano tufuate mila zetu lakini haimaanishi ndio tuache mengine ya kibiblia.

Mbona wazungu wanaoana kimikataba na maisha yanasonga? Wakiona goma limenoga wanarenew mkataba. Wakiona wamechokana wana-retire mkataba.

Tatizo kubwa waafrika tunapenda kuishi kwa kupretend sana.

Unforgetable
 
Biblia inakataza

(Marko 10:6-12)
Lakini tangu kuumbwa ulimwengu, Mungu aliumba mwanamume na mwanamke. 7 Hivyo mwanamume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, 8 nao wawili watakuwa mwili mmoja. Kwa hiyo, wao si wawili tena bali mwili mmoja. 9 Basi, alichounganisha Mungu, binadamu asitenganishe.”
10 Walipoingia tena ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza juu ya jambo hilo. 11 Naye akawaambia, “Anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, anazini dhidi ya mkewe. 12 Na mwanamke anayemwacha mumewe na kuolewa na mwingine anazini.”(1 KOR. 6:18-20)
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
 
Ni jambo jema hili kwa Maaskofu wetu, badala ya KUSIFIA JUHUDI tu, wangeshughulika na hili mapema sana.
Kabla ya kulishughulikia hili nafikiri wangeanza kujishughulikia wao kwanza.. WAOE... maana wana watoto hovyo huku mtaani.
 
Wanaume hata ukiwapa wanawake kumi,akipita mwanamke wa 11 bado watamtaka...so kuoa wake wawili sio solution ya kuchepuka..
Ila atleast wakiwepo zaidi ya mmoja ambao ni permanent wanakupunguza spid kuliko kua na mmoja pekee.

Ukweli ni kua mwanamke mmoja hatoshi.
 
Maudhi madogo madogo katika ndoa.
Jamii yetu imekua na tabia ya kuchukulia hili swala simple sana la ndoa,,

Lakini endapo mwanamke utatoka katika familia wanayokupenda sana, na hakika haya yote hayawezi kukutokea.
Mume anapaswa kuchunguzwa hata mwaka kabla ya kupewa mchumba.
 
Siku hizi ndoa kwa maana halisi ya ndoa ni kama hazipo tu. Kuruhusu ndoa za wake wengi si suruhisho la michepuko bali ihararishwe ili kuondoa dhana ya dhambi kwa muhusika. Mwanaume kujifungamanisha kwa mwanamke mmoja ni kujinyanyasa kibaiyolojia na kujipumbaza kisaikolojia... Haikuwezekana toka enzi za mfalme daudi, suleiman... Nitawezaje mimi leo kuwa na mwanamke mmoja, tena hawa wa leo pasua kichwa.
 
Wee mwanamke nakukubali sana , ila kwa hapa umeonesha ulivyo finyu kwenye suala la michepuko, tofautisha kati ya udini na uhalisia.

1. Kumiliki wanawake wengi ni ishara ya tamaa ya ngono.
2. Dunia imekengeuka, suala la mtu kuchepuka ni suala binafsi sana na hivyo kuwa na wanawake wengi hakumzuii mtu kuchepuka na hata hivyo wenye wake wengi ndo malaya na tamaa kubwa kuliko wenye mmoja.
 
Back
Top Bottom