Kama Mkataba wa Bandari ya Dar es Salaam utapita, basi kuna haja pia ya kuwaachia wachina Bandari ya Bagamoyo

IFAC

JF-Expert Member
Dec 12, 2021
3,626
9,146
Naandika nikiwa na mawazo ambayo hayajasababishwa na mahusiano ya kimapenzi kama Vijana wengi wa kiswahili wanavyo hangaika.

Bali kuhusu mwendo wa Taifa langu na hatima ya bandari zetu. Ndio ni za kwetu maana kuwa Mtanzania ni haki ya kuzaliwa na hatujaichagua.

Bandari ya Bagamoyo na uwekezaji wa Wachina tuliupinga vibaya tukionyesha kasoro kadhaa ikiwemo kuto iendeleza bandari ya Dar es salaam na nyinginezo kuwa hauna afya kwa mustakabari wa Taifa letu.

Fursa ambayo Wakenya waliidaka juu kwa juu na Sasa ukiangalia kwenye Belt and Road Initiative Kenya ndio ipo included.

Sasa wanatuletea kitu kile kile ila kutokea kwa Waarabu ila afadhali ya Wachina kuhusu bandari moja, hawa Sasa watamiliki bandari zote nchi nzima.

Yaani kuanzia Mtwara -Tanga mpaka zile za Ziwa Nyasa. Kitu ambacho kitakuwa na athari za kiuchumi na usalama wa nchi.

Kifupi watakuwa na uwezo wa kukontroo kinachoingia na kutoka Tanzania kwa muda usio na kikomo.

Je, ndio njia sahihi kwenye kudhibiti rasilimali za nchi na kuendelea watu wake?

Tujitafakari!!?
 
Ndio maana yake. Afrika hii vipandevipande vya ardhi zenye manufaa zitaanza kuchukuliwa na mataifa ya nje kwa mikataba ya kizuzu. Mara maji, mara ardhi, mara anga, wengine watakuja na kutaka wapate mikataba ya kuendeleza misitu na wanyama pori. Muafrika anaanza kuwa mtumwa tena kwenye nchi yake. Uhuru unaanza kutoweka na ukoloni unaanza kurudi kwa mlango wa nyuma
 
Back
Top Bottom