Kama mimi ndiyo ningekuwa Mungu...

GRAMAA

JF-Expert Member
Nov 1, 2014
1,155
3,399
Kama ingetokea mimi ndiyo ningekuwa Mungu basi haya nisingeyafanya kabisa.

1. Ningemuua shetani haraka iwezekanavyo ili kuwalinda wanangu na majaribu ya shetani.

2. Nisinge mtoa mwanangu kafara (Jesus) kama njia ya kuwakomboa watu wengine. Ningetafuta njia nyingine ya kuwakomboa watu WANGU

3. Nisingewasha limoto likubwa ili niwachome watu wangu siku ya mwisho eti kisa walikuwa hawanisikilizi.

4. Nisingeruhusu vitabu vyangu (Biblia na Quran) viwe na utata na viwe na mafumbo mazito. Ili iweze sasa.

5. Nisingeona sababu ya kujificha kwa viumbe nilivyoviumba mimi mwenyewe. Ningejitokeza wazi kabisa.

6. Nisingeruhusu machafuko, magonjwa na shida zozote kwa watu wangu. Nisingeweza kumuumba mtu alafu aje ateseke duniani.

7. Ningetoa utata juu ya ipi ni dini ya ukweli. Nisingeacha watu wangu wahangaike na madini mengi na madhehebu mengi.

8. Nisingesubiri mpaka watu wangu waniombe kitu wakati najua kabisa kitu hicho wanauhitaji nacho.

9. Ningeifanya dunia kuwa sehem ya amani kwa watu na viumbe vyote.

10. Bifu langu na ibiris ningelisolve haraka ili niwaokoe watu WANGU.

Toka warumi walipomuua Mungu msalabani dunia imekosa Mungu kabisa.
 
hapo mwisho umemaanisha kuwa mungu pia alikufa au mm ndo cjakuelewa na kama anaweza kufa basi n kama tulivyo binadamu wengine tu hana utofauti nasi
 
Back
Top Bottom