Kama milo 3 bado na kura bado

Kama milo 3 bado na kura bado

Marekani ni mfano wa donor country,je wanaokula mlo mmoja hawapo???alaumiwe trump au Obama???
Takwimu zinakuambia nini kuhusu % ya wasiopata milo 3 huko Marekani? au unajisemea tu. Idadi na Sababu zao za kula milo chini ya 3 ni tofauti na za kwetu. 80% ya watu wetu wanaishi kwa kilimo cha kutegemea mvua na kulima kwa jembe la mkono na masoko yasiyo na uhakika, sanaa zinaibiwa, wachezaji hawalipwi, mishahara midogo. Kama angelikuwa mimi ningehangaika na hawa 80% kabla ya wale 0.36% ya wanaosafiri kwa ndege. Hapa sasa hivi ningeshachimba mabwawa 5000 makubwa ya kumwagilia ili kumaliza njaa yao kwanza. Matunda ya kuokoteza ukijenga kiwanda malighafi ya kuendesha kiwanda kwa mwaka mzima itatoka wapi? pamba je ipo? alizeti je ipo wapi ya kuwalipa mwaka mzima wafanyakazi watakaoajiriwa kwenye viwanda vya mafuta? ngozi bora zisizo na makovu je zipo za kutosha? Wakulima na wafugaji je nani amewafundisha namna bora ya kulima na kufuga, wanayo mitaji?
 
Back
Top Bottom