Kama mikutano ya CHADEMA ndio hii, ninamuhurumia sana Bernard Membe

Nadhani ukitembelea tovuti ya Tume ya Uchaguzi unaweza kuyapata!
 
CCM INAFANYA TAMASHA LA MUZIKI DODOMA
 
Nilishawahi kusema JF imeshakosa uhalisia wa neno GREAT THINKERS,,, LISU amezindua mbagala mkutano, siyo dar. .mlitaka watu wa gongo la mboto waende mbagala wakati wameambiwa wasubiri watafikiwa. Na siyo lazima watu wasombwe na magari. Kura iko mioyoni mwa watu...siasa ni sayansi halisi siyo feki ya kuita MSAGA SUMU alazimishe wanafunzi kuja kusikiliza. .ndo mana CCM inaweka mpira kwapani
 
Nadhani ukitembelea tovuti ya Tume ya Uchaguzi unaweza kuyapata!
Wataalam wa computer science kwa mawazo hayo watakwambia kichwa kina virus thereforth needs antivirus to deal with it. Ulimwengu wa kistaarabu tulionao saizi unaogopa kushindana kwa hoja unapita kwa mapingamizi meanwhile chama chako wote wakipita how comes
 
Unaleta ushahidi wa picha ya TBC? Pumbavu kabisa, wameweka picha ya saa 5 ndiyo wanatuaminisha nfiyo mahudhurio ya wananchi hayo? Ndiyo maana Mbowe aliwatimua uwanjani!
Picha ya saa tano yenye vivuli virefu zaidi ya kimo cha mwenye kivuli!

Ungesema picha ya saa mbili za asubuhi ambapo mpaka viongozi wakuu walikuwa wamewasili jukwaani!
 
Na ni yaleyale tu. 2015 mpaka siku ya mwisho wa kampeni, tuliambiwa ilani tukasome kwenye Website, 2020 tunaambiwa ilani haisomwi mpaka siku watu wakiwa wengi uwanjani😂😂
Bila ilani CDM walishinda uchaguzi,hawakutangazwa
 
Huoni kama ungesindikiza hizi kelele zako na picha hata ya ku-edit ungeeleweka vizuri zaidi?

Ni kelele kwasababu licha ya kuaminisha vipofu Chadema haina mvuto, lakini kila siku mnawaengua wagombea wake bila sababu za msingi, atleast ungeleta thread kuhusu huo ujinga wa Tume ningekuelewa, tofauti na hapo ni kelele tu.
 
Ukweli usemwe.
Mzuka wa Chadema haupo. Si kama mwaka 2010 na 2015.Hii inasababishwa na sababu nyingi, lakini moja kubwa ni ile hamahama ya baadhi ya viongozi wake kuunga mkono juhudi imewakatisha tamaa watu wengi. Inawapa nafasi CCM kuendelea kupeta tu.
 
Kwanini Membe na sio Lipumba au mgombea wa NCCR?
Tunaona CCM mlivyojipanga kwa kujaza wasanii!
 

Maelezo yako yanahitimisha kuwa CHADEMA na vyama vya upinzani kwa ujumla haviakisi matarajio ya Watanzania wengi. Kwamba “upinzani” uliopo ni mzigo (liability) badala ya kuwa tegemeo (asset) kwa wananchi.

Bado unafikiri kuna haja ya “upinzani” nchini? Kwamba ni kiasi cha kuungana tu (wawe chama kimoja) ndipo wapate uungwaji mkono mkubwa? Kwa mantiki hiyo, dhana ya mfumo wa vyama vingi itakuwa na maana ipi na manufaa gani kwa Mtanzania ikiwa vyama vyote vitakuwa na mtazamo wa aina moja na lengo kuu ni kupata fursa za u-Rais, ubunge na udiwani tu! Tena kwa upinzani wasiguse u-Rais kabisa!

Ni kama vile inavyonipa taabu kuelewa kwa nini UDP na LDP wasitangaze kuvunja vyama vyao na wote kuhamia CCM. Baada ya maazimio ya mikutano yao mikuu, sioni kama wana “raison d'être” tena.

Ukiwa mnazi wa CCM, unaweza kufikiria (envision) CCM ikiwa chama pinzani na jinsi utakavyokitengenezea mikakati ya kurejea madarakani au kupata wabunge + madiwani wengi bila kuwa na nyenzo za dola wala mwenyekiti mwenye madaraka yote ya ki-Rais (absolute power) kama ilivyo sasa?
 
Kuna tofauti ya watu kupewa posho na usafiri hlf wakaenda mkutanoni na watu kwenda kwa hiyari. Kuna tofauti ukimweka juma nature jukwaani wa mbagala tutajaa tu. Wapinzani wanaenda kusikilizwa na watu wanaotaka kusikiliza sera na wengine hao wanajaza uwanja kwa kua watu wanaenda kumuona simba anaperform.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…