Kama mbwai na iwe mbwai

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Great thinkers, nimechoshwa na hizi tabia za polisi kujichukulia sheria mikononi kama hatuna mahakama. Imekuwa ni kitu cha kawaida kusikia jambazi sugu limeuawa na polisi au polisi wameua wamajambazi. Sisi raia tumebaki kushangilia. Ikumbukwe kuwa hata kuua mtu kuna taratibu zake...na hizo taratibu zinasimamiwa na mahakama. Na raia anaposhangilia kuuawa kwa raia mwingine naye pia anashiriki yale mauaji.

Sababu kuu ya polisi kuua raia (wanaoitwa majambazi) ni kuthibitisha kuwa katika nchi hii ya Tanzania hakuana utwala wa sheria. Moja ya wajibu wa serikali ni kulinda raia wake. Wananchi, tunatakiwa tuungane kupinga dhuluma zoooote za jeshi la polisi hasa hili la kuua raia kila kukicha. Polisi anayeua, anatakiwa afunguliwe mashitaka.

Kuna matukio mengi yanayojitokeza kila mara na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari ambayo yanathibitisha tabia hii mbaya.

Naomba kuwakilisha
 
Hujaeleweka. .na unachoongea bila data....!!

Kwajiyo mkuu unataka nibandike magazeti yote yenye taarifa hizo na vipande vya video na matangazo ya redio ile uelewe? Subiri "great thinkers" wanakuja kuchangia ha ha ha
 
1.Unajua ni hatua ipi inafikia hadi polisi wanaua majambazi.?ni ktk majibizano ya risasi.
2.Ulitaka hao majambazi wapewe pipi ndio ufurahie kazi ya polisi.?
3.Je raia wanaoua wezi wa kuku unawachukuliaje?
..laumu ktk ishu nyngne kama vile mauaji ya raia ktk mikutano na mauaji mengne km vile ya watoto.
 
Great thinkers, nimechoshwa na hizi tabia za polisi kujichukulia sheria mikononi kama hatuna mahakama. Imekuwa ni kitu cha kawaida kusikia jambazi sugu limeuawa na polisi au polisi wameua wamajambazi. Sisi raia tumebaki kushangilia. Ikumbukwe kuwa hata kuua mtu kuna taratibu zake...na hizo taratibu zinasimamiwa na mahakama. Na raia anaposhangilia kuuawa kwa raia mwingine naye pia anashiriki yale mauaji.

Sababu kuu ya polisi kuua raia (wanaoitwa majambazi) ni kuthibitisha kuwa katika nchi hii ya Tanzania hakuana utwala wa sheria. Moja ya wajibu wa serikali ni kulinda raia wake. Wananchi, tunatakiwa tuungane kupinga dhuluma zoooote za jeshi la polisi hasa hili la kuua raia kila kukicha. Polisi anayeua, anatakiwa afunguliwe mashitaka.

Kuna matukio mengi yanayojitokeza kila mara na kuripotiwa kwenye vyombo vya habari ambayo yanathibitisha tabia hii mbaya.

Naomba kuwakilisha

nina mashaka na wewe mbona una watetea majambazi? Mbona hao majambazi ndo wanao ongoza kwa kuua? Wanapo ua na kupora wanafuata utawala wa sheria ? Nina kila sababu kukutilia mashaka
 
1.Unajua ni hatua ipi inafikia hadi polisi wanaua majambazi.?ni ktk majibizano ya risasi.
2.Ulitaka hao majambazi wapewe pipi ndio ufurahie kazi ya polisi.?
3.Je raia wanaoua wezi wa kuku unawachukuliaje?
..laumu ktk ishu nyngne kama vile mauaji ya raia ktk mikutano na mauaji mengne km vile ya watoto.

Hata zombie aliua in cold blood wafanyabiashara wa madini toka Mahenge na kusema walikuwa ni majambazi, hiyo ya juzi waliotaka kumbambikia raia fuvu la kichwa ili awape pesa, binafsi hili jeshi la polisi hili tena chini ya Mwema nimepoteza imani nalo na nalichukia, hata nikimkuta nyoka anapambana na polisi namsaidia nyoka..... nimepita.
 
1.Unajua ni hatua ipi inafikia hadi polisi wanaua majambazi.?ni ktk majibizano ya risasi.
2.Ulitaka hao majambazi wapewe pipi ndio ufurahie kazi ya polisi.?
3.Je raia wanaoua wezi wa kuku unawachukuliaje?
..laumu ktk ishu nyngne kama vile mauaji ya raia ktk mikutano na mauaji mengne km vile ya watoto.

huyo nadhani hayajamkuta, ngoja majambazi yamvamie yamcharange mapanga kwanza and then aje hapa awatetee vizuri.
 
1.Unajua ni hatua ipi inafikia hadi polisi wanaua majambazi.?ni ktk majibizano ya risasi.
2.Ulitaka hao majambazi wapewe pipi ndio ufurahie kazi ya polisi.?
3.Je raia wanaoua wezi wa kuku unawachukuliaje?
..laumu ktk ishu nyngne kama vile mauaji ya raia ktk mikutano na mauaji mengne km vile ya watoto.
Hujamuelewa mtoa mada.... Nitakupa mfano, hivi Kombe baada ya kuawa kwa kupigwa rsasi na polisi, ilitolewa sababu gani? Si walisema wamemfananisha na jambazi? Na sisi wananchi tulichuwa hatua gani? HIVI NANA ANATAKIWA KUTHIBITISHA HUYU NI JAMBAZI NA HUKUMU YAKE IWE KIFO? Kinachofanywa na polisi ni kujichukulic sheria mikononi IN THE NAME OF UJAMBAZI... Kwani mtu akitajwa kuwa jambazi ndo anastahili kuuawa? Kama ni hivyo kwa nini wasiwauwe majambazi waliothibitika walioko magerezani?
 
Wanamgoma baridi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwa hiyo kama akiny.a barabarani nawe ut.akunya...??

Kuna uhusiano gani hapo?!

Wewe vifo ni vya hao tu,hakuna askari aliyewahi kuuliwa na Majmbazi?

Askari sio Malaika kama ulivyo wewe sio Malaika pia

NB;
Risasi ni kwa matumizi ya Binadamu huu ndo ukweli usiopendeza masikioni...
 
Uhusiano upo mkubwa tu...Hukuwa specific kwa vile naye hakuwa specifi, na ndiyo maana nikakupa mfano kwa njia ya swali...
Ni kweli, kwa sehemu fulajni risasi ni kwa ajili ya binadamu, lakini kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa na si kutumia tu .... vinginevyo watumiavyo majambazi hakutakuwa na tofauti na watumiavyo polisi...
 
Back
Top Bottom