Nakubaliana na ww kwenye baadhi ya mambo hasa utendaji wake,nina shaka kwenye hoja ya kutokuwa fisadi. Nitangaze conflict of interest kuwa ni mpenzi na mshabiki wa CDM, but tukiacha mambo ya vyama umetangaza kumchagua uki ignore uwezo wa wagombea wengine kati ya machaguo tuliyo nayo kati ya wagombea, kutakuwa na tatizo kama atagombea kwa CCM kwa sababu mfumo ulisha haribika na unatakiwa kusukwa upya ili aweze kuwa na ujasiri na kuendelea kutokuwa muoga, alisimamia vizuri suala la shule za kata kama sijakosea, ni mtu anayeweza kuchukua maamuzi hasa magumu (ndio tatizo tulilonalo kwa sasa), kuna limitation ya baadhi ya maamuzi kulingana na mfumo hivyo kutoa picha ya Uoga, mfano si jambo jepesi kumchukulia hatua mtu aliyeua wakati amekusaidia kuua ili uwe kwenye nafasi uliyonayo.Nifupishe kwa kusema yafuatayo
1. Alikuwa mmoja wa wanamtandao waliochota fedha za wananchi ili kufanikisha ushindi wa CCM na uenda akatumia tena mbinu hizohizo na kuzidi kubobea kwenye ufisadi.
2. Atakuwa mgombea mzuri kama nchi haitakuwa na watu makini wa kugombea na hivyo taifa kukosa mbadala
3. Mtandao alioutengeneza uliojaa mafisadi ndani yake utamkwamisha na dhana ya kutokuwa muoga itatoweka kwa kuwa atalazimika kuwalinda.
4. Nguvu kubwa ya fedha inayotumika kumsafihsa na kujitengenezea mazingira/ network ya kushinda inaweza kulipeleka taifa pabaya.