Kama Lowassa atapata nafasi ya kugombea urais kura yangu anayo pamoja na u-CHADEMA wangu

KV LONDON

JF-Expert Member
Jul 18, 2012
903
241
Aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza kwa utawala wa JK ndg Edward Lowasa 'EL' maarufu kama mzee wa 'RICHMOND' au mzee wa 'White hair' nadiriki kusema kuwa kama akipata nafasi ya kugombea taasisi ya Uraisi atakuwa na kura yangu moja kwa moja pamoja na uanachama wangu makini wa CHADEMA.
Hii ni kutokana na sababu zifuatazo;
1. Ni mchapakazi
2. Hana woga wa aina yoyote
3. Anajiamini kwa mambo anayoyasimamia
4. Anawapenda wananchi.
5. Siyo fisadi kama tunavyomtangaza.
6. Ni mpenda maendeleo kuliko kitu kingine.
7. Anasimamia maslahi ya taifa zaidi kuliko chama.

Hayo nimeyaona kwa EL' kuliko ninavyomwona Pinda.
Lowasa aliisimamia serekali kikamilifu sana ukimlinganisha na Pinda aliyejipambanua kama mtoto wa 'MKULIMA' kumbe ni mtoto wa mjini(mjanja tu), anajua anachokisema ila hawezi na wala hathubutu kukisimamia ila EL aliweza na nina imani ataweza.

Tutofautiane kwa hoja na siyo viroja na matusi yasiyojenga.
Nimeyasema haya nikiwa na imani kuwa Tanzania tunahitaji viongozi makini na siyo maswala ya vyama'.
Mungu ibariki Tz.
 
Kama unataka kujinasua kwenye hili lindi la umaskini piga chini CCM 2015

Lowassa anao mtandao wake. Na mitandao inahitaji pesa ili kujiendesha kufikia malengo yake. Matokeo yake wataendelea kuhujumu uchumi kwa kuleta kampuni feki.

Wanakwamisha maendeleo hawa
 
Jamaa wanayo chapaa.....
 
Kaka ninaiman hadi sasa umeshakuwa mtu mzima kwa mwendo huu nazani wadogo zako hawana wajifunzalo kutoka kwako! Watanzania kwa sasa tuchague viongozi bora sio chama
 
Siku zote nimesema ndani ya Chadema kumejaa mapandikizi ya CCM (Lowassa). halafu watu wanapiga kelele humu JF kuwa wataing'oa CCM madarakani, wafuasi wa Chadema wameanza kukiri wote watarudi CCM na kumuacha Dr Slaa peke yake.
 
Nakubaliana na ww kwenye baadhi ya mambo hasa utendaji wake,nina shaka kwenye hoja ya kutokuwa fisadi. Nitangaze conflict of interest kuwa ni mpenzi na mshabiki wa CDM, but tukiacha mambo ya vyama umetangaza kumchagua uki ignore uwezo wa wagombea wengine kati ya machaguo tuliyo nayo kati ya wagombea, kutakuwa na tatizo kama atagombea kwa CCM kwa sababu mfumo ulisha haribika na unatakiwa kusukwa upya ili aweze kuwa na ujasiri na kuendelea kutokuwa muoga, alisimamia vizuri suala la shule za kata kama sijakosea, ni mtu anayeweza kuchukua maamuzi hasa magumu (ndio tatizo tulilonalo kwa sasa), kuna limitation ya baadhi ya maamuzi kulingana na mfumo hivyo kutoa picha ya Uoga, mfano si jambo jepesi kumchukulia hatua mtu aliyeua wakati amekusaidia kuua ili uwe kwenye nafasi uliyonayo.Nifupishe kwa kusema yafuatayo
1. Alikuwa mmoja wa wanamtandao waliochota fedha za wananchi ili kufanikisha ushindi wa CCM na uenda akatumia tena mbinu hizohizo na kuzidi kubobea kwenye ufisadi.
2. Atakuwa mgombea mzuri kama nchi haitakuwa na watu makini wa kugombea na hivyo taifa kukosa mbadala
3. Mtandao alioutengeneza uliojaa mafisadi ndani yake utamkwamisha na dhana ya kutokuwa muoga itatoweka kwa kuwa atalazimika kuwalinda.
4. Nguvu kubwa ya fedha inayotumika kumsafihsa na kujitengenezea mazingira/ network ya kushinda inaweza kulipeleka taifa pabaya.
 
Tumchoka na CCM kwa ujumla. Hakuna jipya Mkapa alukuwa mchapa kazi lakini ufisadi uliendelea. Hatutaki kuendeleza ufisadi TZ. waTZ msijute kama mtaendelea na CCM madarakani. Tuweke utaratibu wakubadilisha watawala ili wajue kuwa kama hawatekelezi matakwa ya wananchi wanatolewa na sula la "impunity" litakwisha na inch itakuwa na maendeleo. Zambia na Kenya mameweza kwanini TZ hatuamki ni usingizi huu tulio naio?
 
Kama unataka kujinasua kwenye hili lindi la umaskini piga chini CCM 2015

Lowassa anao mtandao wake. Na mitandao inahitaji pesa ili kujiendesha kufikia malengo yake. Matokeo yake wataendelea kuhujumu uchumi kwa kuleta kampuni feki.

Wanakwamisha maendeleo hawa

hata richmond nina unaimani kuwa walimpakazia ila japokuwa naipenda sana chadema tena hasa Dr Slaa nampenda sana katibu wangu mkuu ila tufanye kazi ya ziada kulikomboa taifa letu
 
Aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza kwa utawala wa JK ndg Edward Lowasa 'EL' maarufu kama mzee wa 'RICHMOND' au mzee wa 'White hair' nadiriki kusema kuwa kama akipata nafasi ya kugombea taasisi ya Uraisi atakuwa na kura yangu moja kwa moja pamoja na uanachama wangu makini wa CHADEMA.
Hii ni kutokana na sababu zifuatazo;
1. Ni mchapakazi
2. Hana woga wa aina yoyote
3. Anajiamini kwa mambo anayoyasimamia
4. Anawapenda wananchi.
5. Siyo fisadi kama tunavyomtangaza.
6. Ni mpenda maendeleo kuliko kitu kingine.
7. Anasimamia maslahi ya taifa zaidi kuliko chama.

Hayo nimeyaona kwa EL' kuliko ninavyomwona Pinda.
Lowasa aliisimamia serekali kikamilifu sana ukimlinganisha na Pinda aliyejipambanua kama mtoto wa 'MKULIMA' kumbe ni mtoto wa mjini(mjanja tu), anajua anachokisema ila hawezi na wala hathubutu kukisimamia ila EL aliweza na nina imani ataweza.

Tutofautiane kwa hoja na siyo viroja na matusi yasiyojenga.
Nimeyasema haya nikiwa na imani kuwa Tanzania tunahitaji viongozi makini na siyo maswala ya vyama'.
Mungu ibariki Tz.

Umejuaje kwamba atakayegombea urais kupitia CHADEMA hana sifa hizo au zaidi?

Jibu hilo kwanza
 
View attachment 71417

naona unaelekea kazini

Kuchukua+chakula.JPG
 
Siku zote nimesema ndani ya Chadema kumejaa mapandikizi ya CCM (Lowassa). halafu watu wanapiga kelele humu JF kuwa wataing'oa CCM madarakani, wafuasi wa Chadema wameanza kukiri wote watarudi CCM na kumuacha Dr Slaa peke yake.

Dua ya mwewe...
 
Kaka ninaiman hadi sasa umeshakuwa mtu mzima kwa mwendo huu nazani wadogo zako hawana wajifunzalo kutoka kwako! Watanzania kwa sasa tuchague viongozi bora sio chama

nakuunga mkono ndugu, mimi ni mwana CDM sana ila napenda kumchagua mtu na siyo chana' na pia sijaona mtu mwingine wa kumchagua ndani ya CCM zaidi ya Lowasa'
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom