Kama kuna tabia inayokutesa soma hapa .........!!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Inawezekana kuna tabia ambazo unazo lakini unatamani kuziacha lakini zinakushinda

Inawezekana kuna mambo ambayo unayafanya na unasikia watu wanasema kuwa hayafai lakini unayaona kuwa yanafaa kwasababu unadhani yanakupa furaha

Hayo yote yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku na tunashindwa kuondokana kwenye hali hizo na kujitengenezea sababu au uhalali wa sisi kuendelea kuwepo kwenye mambo au tabia tunazofanya

Kuna wengine wanajua kabisa kuwa jambo fulani ni baya na wengine hawajui ubaya kwa kuangalia upande mmoja tu wa jambo ambalo wanakuwa wanalifanya,mara nyingi hawa wa pili wanakuwa hawajui uhalisia wa tabia au jambo ambalo wanalifanya

Kama una tabia fulani ambayo sio nzuri basi unaweza kuwemo kati ya hayo makundi hapo juu

Hapa nitakwenda kuelezea kwa uzoefu wangu namna ya kwenda kuacha tabia au mambo ambayo yanaonekana yamekushinda kuacha au hutaki kuyaacha kwasababu wewe binafsi hujaona ubaya wake

Kwa kawaida haya ambayo yanasemwa kuwa mabaya au tunayaona kuwa mabaya huwa yana upande ambao tunadhani unatufurahisha,yaani uzuri wake

Mfano,uzinzi
Mtu anaweza kuwa ana tabia hiyo ya uzinzi na anatamani kuiacha lakini kila akimuoda mdada wenye umbo fulani anajikuta tu ameshamfuata na kwenda kumtongoza huku nyumbani ana mke

Kuna mwingine yeye hataki kuacha japokuwa anasikia watu wakisema uzinzi ni mbaya na haufai kwa binadamu kwasababu ni aibu kwa binadamu kufanya tabia kama za wanyama lakini yeye anakuwa anaangalia namna anavyoburudika anapokuwa na wadada tofauti tofauti na raha ya tendo lenyewe

Mazingira yote haya ya mambo haya yanamfanya mtu asiache kufanya kile ambacho anataka kukiacha au ambacho anasikia kuwa ni kibaya

Kutokujua ubaya na kuujua lakini mtu anashindwa ndio janga kubwa

Nitatoa mfano mwingine
Kila uchao tunaambiwa kuwa kula chakula halafu wakati huo huo unakunywa maji sio vyema kwa afya,wengi tumeshindwa kuachana na jambo hilo kwasababu hizo hapo juu ambazo ni mbili,yaani kuna mtu ambae anashindwa kuacha kunywa maji wakati wa kula kwasababu wakati anakula anashikwa na kiu kitendo ambacho kinamfanya ayanywe maji

Huyu mwingine ambae anasikia tu watu wakisema kuwa kunywa maji sio salama kwa afya yeye anaendelea kuyanywa kwasababu kwanza anaburudika wakati anafanya hivyo na zaidi sana hajawahi kuona mtu akipata tatizo linalodaiwa kuwepo kwa wale ambao wanafanya hivyo

Kwa hayo yote hapo juu nadhani utakuwa umenielewa kile ambacho nataka kukisema hapa

Ki msingi tabia ziko nyingi sana lakini kuna jambo ambalo linaweza kukusaidia kuacha tabia yoyote ile ambayo unayo na inakusumbua kuacha au umeshindwa kuacha kwasababu inakufurahisha

Kwenye makundi yote hayo mawili ya watu ambao wana tabia hizo wote kitu kimoja tu ndicho kinakuwa kinamfaya kila mmoja wao kuendelea kufanya kile ambacho anakifanya,kitu hicho ni raha ambayo anakuwa anaipata kutokana na kile ambacho anakuwa anakifanya,kusingekuwa na raha fulani kwenye haya mambo wengi sana wangekuwa wameacha hata kwa kujilazimisha

Tunashindwa kujilazimisha kwasababu tu ya ile burudani kutoka kwenye suala husika,hili wavutaji wa sigara na wanywaji wa pombe watalielewa sana

Njia nzuri ya kuacha tabia au jambo lolote lile ni kuanza ku deal na kile ambacho kinakufanya ulifurahie jambo lenyewe ambacho ni raha au "furaha"

Tunatakiwa tujue kuwa mambo yote huanzia ndani mwetu kwenye imani zetu [sio za kidini] yaani ukiamini jambo au kitu fulani ni kizuri basi utajikuta tu kinakuvutia

Sasa kama tatizo linaanzia huku ni bora hata hatua za kuacha zikaanzia huko pia,wazungu wana msemo wa o kuwa "kama unataka kumuuwa mbwa mpe jina baya na utapata sababu ya kumuua",msemo huu una maana kubwa sana kwani kadiri unayoendelea kumuita mbwa huyo kwa jina lile baya linakwenda kubadili mtazamo wako kwa mbwa ulioko ndani mwako,kama ulikuwa mtazamo wako ni mzuri basi utaanza kubadilika na kuwa mbaya

Hilo linaweza kuonekana ni jambo kama la kitoto hivi lakini ndivyo ilivyo

Kama unapenda sana kuvuta sigara kwasababu ya "burudani" ambayo unaipata kila ukivuta sigara,unatakiwa uipe sigara jina baya na kila unapoikumbuka iite kwa jina hilo na taratibu utaanza kuichukia na hatimae utakuja kukosa sababu ya kuendelea kuitumia nahata ile furaha au burudani ambayo ulikuwa unaipata utaanza kuiona kama haifai tena

Jambo hili la kuacha tabia fulani limetufanya tulione kuwa gumu kwasababu ambazo sisi wenyewe tulizojijengea na wala hakuna uhalisia wowote ule,mambo haya huingia ndani mwetu taratibu na hatimae kuota mizizi na kuondoka kwake nako ni hivyo hivyo pia

Mvutaji wa sigara hakuifurahia sigara siku ya kwanza ya kuivuta kwasababu sigara kiuhalisia sio nzuri,lakini kutokana na maneno ya wavutaji wazoefu walipokuwa wanamuambia huyu mvutaji mpya uzuri wa sigara nae alianza kuutafuta huo uzuri hata kwa kulazimisha kwani hakuuona kwa mara ya kwanza na hatimae aliijenga imani ndani mwake kuwa sigara ni nzuri na jambo hilo likaja kuwa hivyo kweli kwenye uhalisia

Kwa kifupi tabia zetu kwenye mambo mengi huanza hivyo taratibu taratibu hadi zinaota mizizi ndani mwetu bila sisi kujua kuwa mchango wa tabia hizi kuota mizizi ni sisi wenyewe na hata kuziondoa tunaweza,matokeo yake tunaendelea kuzipa majina makubwa ya kuzifanya kuonekana kuwa ni vigumu kuziacha na hapo ndipo tunapoendelea kuzifanya kuwa na ukomavu ndani mwetu bila sisi kujua

Unapoanza kufanya mazoezi ya kuacha tabia yoyoe ile lazima utakutana na changamoto kwani zile imani zetu tulizozijenga kwenye suala husika hazitakubali kuondoka hivihivi tu bali zitataka kubisha,usiogope kwani hilo ni suala la muda tu na hatimae zitaondoka

Hilo ni sawa tu na wakati unaanza kufanya jambo husika,mwanzo ni kulikuwa na vipingamizi ambavyo vilikuwa vinakuambia "mbona jambo hili sio zuri" lakini uliamua kuzipuuza kauli hizi kwa kupeleka imani yako kwenye uzuri wa jambo lenyewe uliokuwa unaambiwa na kwakuwa imani yako umeiondoa kwenye kulikataa jambo husika na umeipelekakwenye kulikubali hata kama hukua unaiona raha ya jambo lenyewe umejikuta ukilipenda jambo lenyewe kwasababu ya imani yako kwenye jambo husika

Jambo hili ni swa na mtu ambae anataka kupenda jambo wakati analichukia,unabadilisha mtazamo wako tu kuhusiana na jambo husika na taratubu chuki iliyoko ndani mwako itabadilika na kuwa furaha

Kanuni ni hiyo tu wala hakuna nyingine na hii kanuni ina nguvu kubwa jaribu uatona

Mada hii ina mambo mengi sana lakini ni nimeona niweke kwa ufupi ili kama kuna ambae atataka basi afanye na ataona mabadiliko

Narudia tena,changamoto zipo hivyo usiogope kwani ukiendelea kwa juhudi utafanikiwa,lakini kwanza unatakiwa ujenge mazingira ya kukipenda hiki ambacho unakifanya kwa kufuata kanuni hiyo ya kuacha au kulifurahia jambo ambayo ni kulipa jambo jina au mtazamo mbaya au mzuri kutegemea na hitaji lako kwenye jambo lenyewe

Jumapili njema ......!!
 
Tabia ya mademu kuomba fedha baada ya match siipendi lol
 
Hivi ukinywa maji wakati wa kula tatizo lake ni nini?
Maana ndo kawaida yangu!
 
Mkuu Eiyer ametoa somo zuri sana hasa ktk kupambana na tabia zisizofaa. Kwa kuendelezea ni kwamba, kama alivyosema mleta mada kuwa tabia zinatokana na mambo tunayoyaamini, lakini wakati unapojaribu kuacha kufanya jambo fulani ambalo si jema, jaribu kupima athari zinazoweza kukupata kutokana na kufanya jambo fulani.
Mf. hakuna mtu aliyezaliwa mlevi, ila mazingira yanakufanya uwe mlevi, kumbe tatizo ni mazingira sio? kwahyo unapodhamiria kuacha hakikisha unakuwa mbali na eneo la ushawishi mf, vijiweni nk.
 
Last edited by a moderator:

Well said mkuu!!
 
Somo zuri sana hili na kwayeyote anaetaka mabadiliko amekuelewa.

Unajua sio kila mtu anajitathimini, wapo watu wanaofanya biashara ya kujiuza huku akijua inamuweka kwenye hatari ya kupata VVU ama ulevi unaoweza kumletea kisukari au kansa.
Kama mtu haoni ubaya wa kitu anachofanya ujue hatathimini maisha yake walau hata kwa miaka 10 au 20 ijayo, mtu wa namna hii hata akisoma ushauri huu wa Eiyer hautamsaidia kwani hajali future yake.
 
Ni kweli kabisa mkuu na ndomaana nikasema anaetaka mabadiliko ataelewa na kufanyia kazi somo hili. Ila kwa ambae anaona bado muda wa mabadiliko hayo kwake ataishia kusoma tu,ila ni vizuri tukajitathmin mapema na kuamua kubadilika kuelekea katika njia sahihi mana kesho yako unaitengeneza leo.
 
Pamoja sana.
 
Kweli kabisaa!!
 
nataka kuacha kupenda cjui unanisaidiaje baba paroko
 
Inawezekana kuna tabia ambazo unazo lakini unatamani kuziacha lakini zinakushinda

Inawezekana kuna mambo ambayo unayafanya na unasikia watu wanasema kuwa hayafai lakini unayaona kuwa yanafaa kwasababu unadhani yanakupa furaha

Hayo yote yanatokea kwenye maisha yetu ya kila siku na tunashindwa kuondokana kwenye hali hizo na kujitengenezea sababu au uhalali wa sisi kuendelea kuwepo kwenye mambo au tabia tunazofanya

Kuna wengine wanajua kabisa kuwa jambo fulani ni baya na wengine hawajui ubaya kwa kuangalia upande mmoja tu wa jambo ambalo wanakuwa wanalifanya,mara nyingi hawa wa pili wanakuwa hawajui uhalisia wa tabia au jambo ambalo wanalifanya

Kama una tabia fulani ambayo sio nzuri basi unaweza kuwemo kati ya hayo makundi hapo juu

Hapa nitakwenda kuelezea kwa uzoefu wangu namna ya kwenda kuacha tabia au mambo ambayo yanaonekana yamekushinda kuacha au hutaki kuyaacha kwasababu wewe binafsi hujaona ubaya wake

Kwa kawaida haya ambayo yanasemwa kuwa mabaya au tunayaona kuwa mabaya huwa yana upande ambao tunadhani unatufurahisha,yaani uzuri wake

Mfano,uzinzi
Mtu anaweza kuwa ana tabia hiyo ya uzinzi na anatamani kuiacha lakini kila akimuoda mdada wenye umbo fulani anajikuta tu ameshamfuata na kwenda kumtongoza huku nyumbani ana mke

Kuna mwingine yeye hataki kuacha japokuwa anasikia watu wakisema uzinzi ni mbaya na haufai kwa binadamu kwasababu ni aibu kwa binadamu kufanya tabia kama za wanyama lakini yeye anakuwa anaangalia namna anavyoburudika anapokuwa na wadada tofauti tofauti na raha ya tendo lenyewe

Mazingira yote haya ya mambo haya yanamfanya mtu asiache kufanya kile ambacho anataka kukiacha au ambacho anasikia kuwa ni kibaya

Kutokujua ubaya na kuujua lakini mtu anashindwa ndio janga kubwa

Nitatoa mfano mwingine
Kila uchao tunaambiwa kuwa kula chakula halafu wakati huo huo unakunywa maji sio vyema kwa afya,wengi tumeshindwa kuachana na jambo hilo kwasababu hizo hapo juu ambazo ni mbili,yaani kuna mtu ambae anashindwa kuacha kunywa maji wakati wa kula kwasababu wakati anakula anashikwa na kiu kitendo ambacho kinamfanya ayanywe maji

Huyu mwingine ambae anasikia tu watu wakisema kuwa kunywa maji sio salama kwa afya yeye anaendelea kuyanywa kwasababu kwanza anaburudika wakati anafanya hivyo na zaidi sana hajawahi kuona mtu akipata tatizo linalodaiwa kuwepo kwa wale ambao wanafanya hivyo

Kwa hayo yote hapo juu nadhani utakuwa umenielewa kile ambacho nataka kukisema hapa

Ki msingi tabia ziko nyingi sana lakini kuna jambo ambalo linaweza kukusaidia kuacha tabia yoyote ile ambayo unayo na inakusumbua kuacha au umeshindwa kuacha kwasababu inakufurahisha

Kwenye makundi yote hayo mawili ya watu ambao wana tabia hizo wote kitu kimoja tu ndicho kinakuwa kinamfaya kila mmoja wao kuendelea kufanya kile ambacho anakifanya,kitu hicho ni raha ambayo anakuwa anaipata kutokana na kile ambacho anakuwa anakifanya,kusingekuwa na raha fulani kwenye haya mambo wengi sana wangekuwa wameacha hata kwa kujilazimisha

Tunashindwa kujilazimisha kwasababu tu ya ile burudani kutoka kwenye suala husika,hili wavutaji wa sigara na wanywaji wa pombe watalielewa sana

Njia nzuri ya kuacha tabia au jambo lolote lile ni kuanza ku deal na kile ambacho kinakufanya ulifurahie jambo lenyewe ambacho ni raha au "furaha"

Tunatakiwa tujue kuwa mambo yote huanzia ndani mwetu kwenye imani zetu [sio za kidini] yaani ukiamini jambo au kitu fulani ni kizuri basi utajikuta tu kinakuvutia

Sasa kama tatizo linaanzia huku ni bora hata hatua za kuacha zikaanzia huko pia,wazungu wana msemo wa o kuwa "kama unataka kumuuwa mbwa mpe jina baya na utapata sababu ya kumuua",msemo huu una maana kubwa sana kwani kadiri unayoendelea kumuita mbwa huyo kwa jina lile baya linakwenda kubadili mtazamo wako kwa mbwa ulioko ndani mwako,kama ulikuwa mtazamo wako ni mzuri basi utaanza kubadilika na kuwa mbaya

Hilo linaweza kuonekana ni jambo kama la kitoto hivi lakini ndivyo ilivyo

Kama unapenda sana kuvuta sigara kwasababu ya "burudani" ambayo unaipata kila ukivuta sigara,unatakiwa uipe sigara jina baya na kila unapoikumbuka iite kwa jina hilo na taratibu utaanza kuichukia na hatimae utakuja kukosa sababu ya kuendelea kuitumia nahata ile furaha au burudani ambayo ulikuwa unaipata utaanza kuiona kama haifai tena

Jambo hili la kuacha tabia fulani limetufanya tulione kuwa gumu kwasababu ambazo sisi wenyewe tulizojijengea na wala hakuna uhalisia wowote ule,mambo haya huingia ndani mwetu taratibu na hatimae kuota mizizi na kuondoka kwake nako ni hivyo hivyo pia

Mvutaji wa sigara hakuifurahia sigara siku ya kwanza ya kuivuta kwasababu sigara kiuhalisia sio nzuri,lakini kutokana na maneno ya wavutaji wazoefu walipokuwa wanamuambia huyu mvutaji mpya uzuri wa sigara nae alianza kuutafuta huo uzuri hata kwa kulazimisha kwani hakuuona kwa mara ya kwanza na hatimae aliijenga imani ndani mwake kuwa sigara ni nzuri na jambo hilo likaja kuwa hivyo kweli kwenye uhalisia

Kwa kifupi tabia zetu kwenye mambo mengi huanza hivyo taratibu taratibu hadi zinaota mizizi ndani mwetu bila sisi kujua kuwa mchango wa tabia hizi kuota mizizi ni sisi wenyewe na hata kuziondoa tunaweza,matokeo yake tunaendelea kuzipa majina makubwa ya kuzifanya kuonekana kuwa ni vigumu kuziacha na hapo ndipo tunapoendelea kuzifanya kuwa na ukomavu ndani mwetu bila sisi kujua

Unapoanza kufanya mazoezi ya kuacha tabia yoyoe ile lazima utakutana na changamoto kwani zile imani zetu tulizozijenga kwenye suala husika hazitakubali kuondoka hivihivi tu bali zitataka kubisha,usiogope kwani hilo ni suala la muda tu na hatimae zitaondoka

Hilo ni sawa tu na wakati unaanza kufanya jambo husika,mwanzo ni kulikuwa na vipingamizi ambavyo vilikuwa vinakuambia "mbona jambo hili sio zuri" lakini uliamua kuzipuuza kauli hizi kwa kupeleka imani yako kwenye uzuri wa jambo lenyewe uliokuwa unaambiwa na kwakuwa imani yako umeiondoa kwenye kulikataa jambo husika na umeipelekakwenye kulikubali hata kama hukua unaiona raha ya jambo lenyewe umejikuta ukilipenda jambo lenyewe kwasababu ya imani yako kwenye jambo husika

Jambo hili ni swa na mtu ambae anataka kupenda jambo wakati analichukia,unabadilisha mtazamo wako tu kuhusiana na jambo husika na taratubu chuki iliyoko ndani mwako itabadilika na kuwa furaha

Kanuni ni hiyo tu wala hakuna nyingine na hii kanuni ina nguvu kubwa jaribu uatona

Mada hii ina mambo mengi sana lakini ni nimeona niweke kwa ufupi ili kama kuna ambae atataka basi afanye na ataona mabadiliko

Narudia tena,changamoto zipo hivyo usiogope kwani ukiendelea kwa juhudi utafanikiwa,lakini kwanza unatakiwa ujenge mazingira ya kukipenda hiki ambacho unakifanya kwa kufuata kanuni hiyo ya kuacha au kulifurahia jambo ambayo ni kulipa jambo jina au mtazamo mbaya au mzuri kutegemea na hitaji lako kwenye jambo lenyewe

Jumapili njema ......!!
kuna katabia kangu sikasemi hapa,ngoja nikaijaribu hii kanuni nione kama kataaga dunia!
 
Mazoeya ni sumu kali sana jamani na maendeleo ya mtu pengne yana kwamwisho na mazoeya ma bovu jaman mi kunakitu apa nimejfunza inabidi kuanzia kesho nakifanyia kazi nakiacha,.
 
Usijaribu .....

Fanya kabisa huku ukiamini inawezekana!
 
Mazoeya ni sumu kali sana jamani na maendeleo ya mtu pengne yana kwamwisho na mazoeya ma bovu jaman mi kunakitu apa nimejfunza inabidi kuanzia kesho nakifanyia kazi nakiacha,.

Hongera mkuu!!
 
Back
Top Bottom