Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 36,355
- 23,759
Ndugu zangu Watanzania,
Kama kuna mtu alikula pesa za Mabeberu na maadui zetu kwa ajili na kwa lengo la kutaka kumpindua Rais Samia pamoja na kuleta ama kuchochea machafuko hapa Nchini yatakayo liangamiza Taifa letu. Ni lazima afahamu ya kuwa Atazitapika Tuuu hizo pesa atake ama asitake.
Ni lazima kila mmoja afahamu ya kuwa watanzania hawapo tayari na haiji kutokea wakaangamia Taifa hili kwa mikono yetu wenyewe. Taifa letu ndio mboni yetu na kila mmoja anajua hatuna Nchi nyingine yenye kuweza kutuhifadhi na kutupatia Maisha bora ya amani na utulivu kama tupatayo hapa Nchini.
Leo hii Tanzania unaweza kwenda mkoa wowote ule ukapokelewa vizuri ,kufanya biashara kwa uhuru wako ama shughuli yoyote ile ya kiuchumi kama vile kilimo bila kikwazo cha aina yoyote ile bila kubaguliwa na wenyeji wa eneo hilo. Leo unaweza kwenda kokote kule ukaishi kwa amani na ukaoa huko huko na kujenga Familia yako.
Leo unaweza kutoka Mbozi mkoani songwe kwa wanyiha na kwenda kuishi mwanza ama Geita kwa wasukuma. Leo hii mchaga anaweza kutoka moshi Kilimanjaro na kuishi na kuoa na kujenga Familia yake Mbozi ama Momba kwa wanyamwanga ama Ileje kwa wandali pasipo kubaguliwa. Ndio maana hata upangaji wa watumishi wa umma wa ajira mpya hauangalii Dini ya mtu ama kabila ama ukoo ama ukanda.
Kinachoangaliwa ni mahitaji ya watumishi wa umma ama wapi kuna upungufu wa watumishi wa umma wa kada fulani. Ndio maana unaweza kutolewa Mara ukapelekwa Mpui ama kalambazite mkoani Rukwa na ukaenda kuishi vizuri na kupokelewa vizuri kabisa.
Sisi miaka nenda rudi tunaishi kama ndugu wa familia Moja. Sisi ni Taifa ambalo tumelijenga katika Muundo wa Familia .mfumo ama muundo wa kupendana ,kuishi kwa pamoja , kusaidiana na kupendana. Ndio maana hatuwezi kuinua mapanga ama visu kuanza kukatana ama kuchinjana. Kwa sababu sote ni ndugu na tuna muingiliano wa kindugu .
Hii ndio Tanzania aliotuachia Mwalimu Nyerere na hii ndio Tanzania Ya Rais Samia Mama wa 4R ambaye anayetambui misingi ya Taifa letu iliyoasisiwa na waasisi wetu. Hii ndio Tanzania ambayo kila mtanzania anajua muelekeo wetu kama Taifa na kipi tunaweza Kugusa na kipi ni mwiko kukigusa. Kwetu amani yetu ni mti usioguswa ama kuchezea. Ni mti unaolindwa kwa gharama yoyote ile.
Maadui Zetu walijaribu kuharibu ama kutingisha tunu hii ili kuleta machafuko hapa Nchini na pengine kujaribu kumpindua RAIS wetu . Lakini kwa bahati mbaya wameshindwa vibaya sana mpaka hawaamini macho yao. Kwa hakika Tanzania na Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.