Kama kikokotoo kipya ni matokeo ya actuarial valuation ya mifuko, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi atumbuliwe? Tusishangilie tuu...mwishowe...

Wewe huwa unasoma kweli au unasubiri watu waandike halafu ubishe

Unafahamu SSRA imeanzishwa lini?

Hii mifuko inadai serikali kwa deni la kurithi, Hivi Unadhani wale wazee wa zamani walichangia makato yao kwenye mifuko?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu,wewe ndiye unayesoma mwenyewe,ndio maana ulisema kwenye uzi wako mmoja kuwa watanzania tuna uelewa mdogo kuhusu kikokotoo kipya,yani wewe na SSRA ndio mna akili kuliko watanzania wote waliowafanyakazi,what a joke?
 
Watanzania hususan Pascal Mayalla acha tabia ya unafiki,uzandiki na ulofa.Bi.Irene kikokothajatumbuliwa na Mh.Rais kwa sababu ya kikokotoo kipya.
Kosa kubwa la Bi. Irene Isaka ni udhaifu wa muda mrefu wa usimamizi wa uwekezaji wa mifuko hii hususan PSPF na NSSF katika miradi mingi ambayo haikuwa na TIJA kwa wanachama wa mifuko husika.
Bi.Irene alishindwa hata kushauri mamlaka za juu yake kama WAZIRI ,nk kuhusiana na uwekezaji wa hasara uliokuwa unafanywa na mifuko ambayo kimsingi yeye alikuwa MSIMAMIZI wake......Mayalla kwa uelewa wako mdogo na mapenzi yako ya dhati kwa Bi.Irene Isaka unamtetea bibiye kwa hoja dhaifu kabisa tena za kijinga..Bi Irene ndiye ameifikisha hii mifuko ICU kwa kutokuwa makini katika kutekeleza majukumu yake ya msingi.
Pascal Mayalla Bi Irene Isaka alikuwa MKURUGENZI WA SSRA ambaye ni msimamizi wa MIFUKO YA JAMII mifuko imefilisika kwa uzembe wake ulitaka Rais Magufuli amzawadie?
Kama Pascal ulikuwa "mapenzi" ya kweli kwa Bi Irene ungemshauri asingeishia kuuza sura kwenye vyombo vya habari.

Nani kakudanganya Kuwa Mifuko ya Jamii imefilisika?,

Unajua determinant ya Taasisi kutambulika Kama Muflisi?

Tuanzie Hapa kwanza tukupe somo ili uache Kuwa Unazungumzia usichokijua

Kwanza Google ujue tofauti ya liquidity problem Na bankruptcy then urudi Hapa nikupe Darsa duara uachane Na propaganda Za Wanasiasa wanaojifanya Wachambuzi wa Uchumi
 
Na worse enough aligeuka kuwa competitor wa Mifuko badala ya kuwa regulator.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna rocket sayansi hapa paskali,serikali ilipe trilioni 8 inazodaiwa na mifuko,hayo mambo mengine lissu anasema ni matango pori,hakuna mfuko utaofirisika kwa maana wanachama kila mwezi wanachangia mabilioni ya shilingi...

-Waachane na uwekezaji hewa kutapakanya fedha tu kama Dege village
-Kulipana mabonus hadi mili 400 hao wakurugenzi
-waache kukopesha wanasiasa
-wajikite kwenye miradi yenye tija tu tena itakayoidhinishwa na bunge.
Unachosema ni kweli lkn kumbuka kinachochangiwa ni namba tuu kama za Mpesa au tigo pesa sio hela halisi, serikali ikiambiwa lete hiyo hela nataka kwenda manalumango kununua mihogo hiyo pesa hawana.
 
View attachment 980931
Wanabodi
Jana nilibahatika kufustilia mkutano wa Rais Magufuli uliofuta kikokotoo kipya na kurejesha cha zamani.

Taarifa ya Waziri Mhagama ilieleza uamuzi wa kikokotoo kipya ni kufuatia actuarial valuation ya afya ya mifuko iliyobaini mifuko ina hali mbaya ambapo kikokotoo cha 1:580 ni kile kile kwa sheria zote mbili ila tofauti ni malipo ya mkupuo kuendelea kulipa 50% kungeiua mifuko ya PSPS na LAPF hivyo ikaamuliwa malipo ya mkupuo yawe 25% badala ya 50% halafu ile 75% iwe distributed evenly for the rest of your life ambapo monthly pension inakuwa kubwa zaidi

Watanzania ni watu wajinga na wa ajabu, kuwahi kutokea duniani, wanashangilia kikokotoo kile kile na hakuna tofauti ya formula ya kikokotoo bado ni ile ile hebu someni bandiko hili mshuhudie jinsi tulivyo wajinga

Kikokotoo cha mafao ya pensheni kilirekebishwa Julai 2014, na ndicho kinachotumika hadi sasa, japo jina la kanuni limebadilishwa.
pension_formula_2014-png.932966

Kikotoo cha pensheni cha mwaka 2014 (hapo juu) kilinganishe na kile cha mwaka 2018 (hapa chini)

pension_formula_2018-png.932967

Hivyo wajemeni, kikotoo bado ni kile kile cha 1:580

Swali langu ni bila kuingilia mamlaka ya rais ku hire and fire as he pleases, kama taarifa hiyo ya actuarial ni kweli, mifuko ina hali mbaya, kosa la Irene Isaka ni lipi hadi kupelekea kutumbuliwa?.

Hii ni kufuatia kila anayetumbuliwa kuonekana ni jipu mbele ya jamii, kuna uwezekano baadhi wanaotumbuliwa sio majipu bali ni kondoo tuu wa kafara?.

Wataam wa masuala ya pensheni tufafanulieni, kama taarifa ya Waziri Mhagama imesema hali ya mifuko ni mbaya, kikokotoo kingeendelea mifuko ingekufa, sasa rais amekirudisha, jee mifuko hiyo italipa pensheni hizo nene kwa uwezo upi, tusije kujikuta kwa sasa tunashangilia tuu halafu baadae tunakuja kukaza mikanda kwa government bail out kwa hazina yetu?.

Utumbuaji: Tuache Siasa Kwenye Professionalism, Sio Kila Mtumbuliwa ni Jipu!. - JamiiForums

Utumbuaji Majipu wa Rais Magufuli: Is It A Right Thing, At The Right Time, And Doing It Right, Or ?! - JamiiForums

Hii Tumbua Tumbua ya Rais Magufuli, Hivi Kikwete Anajisikiaje?!. Anajisikia Sifa Au Anajuta?!. - JamiiForums

.View attachment 980871View attachment 980927View attachment 980930

By the Way,
Ukimwangalia the way this lady look like, she looks yile mama wa TIC aliyetumbuliwa, usikute... it was just the most opportune moment to strike baada ya...
Kuna mambo mengine wajemeni yataka uwe na moyo haswa, sio mchezo...
hata ningekuwa mimi...
P.
Usitake kumsafisha huyu mama,ni jipu lililo kuwa limesha iva ndio maana likatumbuliwa,huyu kama regulator kuna miradi mingi sana ya hovyo ambayo hamna return hizi hifadhi za jamii ilifanya na yeye hakuzuia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kakudanganya Kuwa Mifuko ya Jamii imefilisika?,

Unajua determinant ya Taasisi kutambulika Kama Muflisi?

Tuanzie Hapa kwanza tukupe somo ili uache Kuwa Unazungumzia usichokijua

Kwanza Google ujue tofauti ya liquidity problem Na bankruptcy then urudi Hapa nikupe Darsa duara uachane Na propaganda Za Wanasiasa wanaojifanya Wachambuzi wa Uchumi
You are wrong, as always!
 
Kwanza Google ujue tofauti ya liquidity problem Na bankruptcy then urudi Hapa nikupe Darsa duara uachane Na propaganda Za Wanasiasa wanaojifanya Wachambuzi wa Uchumi
Ili ijulikane kama shirika lina "Liquidity Problem or Bankruptcy" ni lazima kwanza ufanyike ukaguzi wa kina na huru kujua hali ya taasisi kifedha na kirasirimali ikoje. Jee ukaguzi umefanyika na ni lini umefanyika na matokeo yake yalikuwaje?
 
Watanzania hususan Pascal Mayalla acha tabia ya unafiki,uzandiki na ulofa.Bi.Irene hajatumbuliwa na Mh.Rais kwa sababu ya kikokotoo kipya.
Kosa kubwa la Bi. Irene Isaka ni udhaifu wa muda mrefu wa usimamizi wa uwekezaji wa mifuko hii hususan PSPF na NSSF katika miradi mingi ambayo haikuwa na TIJA kwa wanachama wa mifuko husika.
Bi.Irene alishindwa hata kushauri mamlaka za juu yake kama WAZIRI ,nk kuhusiana na uwekezaji wa hasara uliokuwa unafanywa na mifuko ambayo kimsingi yeye alikuwa MSIMAMIZI wake......Mayalla kwa uelewa wako mdogo na mapenzi yako ya dhati kwa Bi.Irene Isaka unamtetea bibiye kwa hoja dhaifu kabisa tena za kijinga..Bi Irene ndiye ameifikisha hii mifuko ICU kwa kutokuwa makini katika kutekeleza majukumu yake ya msingi.
Pascal Mayalla Bi Irene Isaka alikuwa MKURUGENZI WA SSRA ambaye ni msimamizi wa MIFUKO YA JAMII mifuko imefilisika kwa uzembe wake ulitaka Rais Magufuli amzawadie?
Kama Pascal ulikuwa "mapenzi" ya kweli kwa Bi Irene ungemshauri asingeishia kuuza sura kwenye vyombo vya habari.
Chukua tano mzee!
Tumshukuru JPM ambaye ana gut instincts, pale kitu kinaenda ovyo.
 
Mimi najijali mimi peke yangu,nikiona kama nikikufukuza kazi nitapata mtaji wa kisiasa basi sitajali lolote nitakufukuza kazi tu,sitajali kama una kosa au hauna!
 
Ametumbuliwa kwa kushindwa kusimamia mifuko nafikiri unajua menejimenti za mifuko zilivyokuwa zinatumia pesa ovyo kwenye miradi ambayo haifai kama mradi wa Dege wa Kigamboni. Hivyo alisitahili kuachia ngazi ili wengine waongoze kwani yeye tu ndiyo anatakiwa kuongoza SSRA tangu 2012!!?

Ule mradi wa sukari kule morogoro unafaaa?? Thio?? Nani aliyeubuni?? Hela si ya hao hao pensioners??
 
Nilisema humu jamvini kwamba Irene ametolewa kafara. Natoka kayika jamii ambapo mkubwa akij..ba unaambiwa mtoto uluyeko karibu kwamba wewe ndo umej..ba nawe unabana kimya. Kama ni kofi unabanangwa kidogo. Hayo ndo Irene.
 
Ili ijulikane kama shirika lina "Liquidity Problem or Bankruptcy" ni lazima kwanza ufanyike ukaguzi wa kina na huru kujua hali ya taasisi kifedha na kirasirimali ikoje. Jee ukaguzi umefanyika na ni lini umefanyika na matokeo yake yalikuwaje?
Kama haujafanyika ukaguzi huru Na wa kina hoja ya kusema Mifuko umefilisika imetokea wapi?
 
Wanapochangia wenye elimu, MPUMBAVU kama ww ni vyema ukae qt
Ametumbuliwa kwa kushindwa kusimamia mifuko nafikiri unajua menejimenti za mifuko zilivyokuwa zinatumia pesa ovyo kwenye miradi ambayo haifai kama mradi wa Dege wa Kigamboni. Hivyo alisitahili kuachia ngazi ili wengine waongoze kwani yeye tu ndiyo anatakiwa kuongoza SSRA tangu 2012!!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sioni kosa la Irene Isaka, lakini ndiyo hivyo tena...Dada huyu ni mchapa kazi wa ukweli na ameigeuza SSRA kuwa taasisi inayofanya kazi kwa weledi mkubwa utafikiri ni taasisi ya kimataifa...Kwangu mimi tatizo ni kuwa positions hizi huwindwa na watu wengi...majungu hayakosi...Lakini pia utendaji mbovu wa mifuko kama NSSF, PPF na hasa katika suala la uwekezaji nadhani ndiyo sababu ya watu wenye majungu..Binafsi sitashangaa kama akipata nafasi ya kimataifa..au pengine JPM anaweza kumpa kazi nyingine muhimu...Kwangu mimi kumuweka pembeni dada huyu ni kumpoteza mmoja wa wachapakazi wazuri ambao taifa hili limewahi kuwapata..
Kuchapa kazi vizuri kinatakiwa kuwe reflected kwenye kuboreka kwa mafao ya wenye mifuko (wafanyakazi) mengine yooote ni mbwembwe tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fikiria, mtu anahama private kwenda serikalini, anaamua kuchukua pension yake yote huku akiwaambia rafiki zake kuwa kikokotoo kipya ni kibaya. Kingine yeye kama regulator alipaswa kufahamu/kushawishi umuhimu wa sheria mpya kuanza kutumika baadaye ili pawe na kipindi cha mpito. Huyu mama kosa lake ni kushindwa kumshauri rais/waziri, maana angesababisha watu kukosa imani na serikali na kupunguza ari na uzalendo wa kazi. Mi kwa upande wangu huyu mkurugenzi hafai kwa sababu huwezi kuongea academic kwa watu wa kawaida, hata waziri mhagama naye alikishwa sumu, maana unaposema mifuko mingine ilikuwa na uhai mpaka 2075 alimaanisha nini???

Jiwe huwa halishauriki wewe!
 
Magufuli alishapanga kumtumbua Irene kabla ya kile kikao. ukisikiliza kwenye hotuba yake anasema kwamba uwekezaji mbaya wa mifuko ya jamii inatokana na usimamizi mbaya wa rejuleta. kwamba rejuleta alitakiwa azuie uwekezaji usio na faida. swali la kujiuliza ni iwapo hilo ni moja ya kazi ya rejuleta wenye usimamizi wa mifuko. ni kazi yake kukagua na kupisha miradi ambayo mifuko inayotekeleza? rejuleta ana nguvu na utaalamu gani wa kukagua na kujua thamani ya kila mradi ili kujua unafaa au vinginevyo? watu watashangaa sana watakaposikia sababu halisi ya kufukuzwa kwake.
Sasa huyu regulator ana regulate nini hasa kwenye hii mifuko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa watawekeza wapi? Nyie watu ni vituko sana,

Soko La hisa letu ni la kuunga unga

Rate za Bond na TB bills ni ndogo sana

Sasa Ulitaka wakae na pesa ziwe eroded na Mfumuko wa bei?

Punguzeni kuwashwa someni

Sent using Jamii Forums mobile app
Wafanye uwekezaji wenye tija, waache kuparamia uwekezaji wa kudidimiza michango ya wafanyakazi.... Halafu unaweza kunionyesha kwenye kikokotoo cha zamani au kipya faida from huo uwekezaji mfanyakazi anapata asilimia ngapi? I mean michango yako na ya mwajiri say ni 50 milioni je unawekewa another 10 million as your % from investments profits??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pasko,
Usijifanye kutokujua kosa la "Dr" Irene.
Naiweka "Doctorate" yake katika mabano, maana ameshindwa kabisa kuutetea usomi.
Using facts and figures ameshindwa ku extrapolate resultant social sentiments ambazo ndio zimemuondoa kazini.

Hili ni onyo kwa technocrats serikalini.
Tell it as it is, full stop.
"Dr" Irene akasema mara ooh, wafanyakazi mmekatwa na kuchangia 20%, sisi tunawapatia 25% ikiwa ziada ya 5%!
Stupid crap!

Hata basis ya percentages hajui, na usomi wake ukapeperuka.

Watu kama kina Dr Mpango siku hizi wamestuka, wanaeleza issues kama zilivyo, na effects zake kwa jamii.
Wamebaki wasomi fake kama "Dr" Irene, hata kudadavua issues hawawezi, achilia mbali ku forecast resultant effects.

She had to go.

Wahariri mafisadi wamlilia Dk Irene Isaka

Waandishi wa habari waandamizi wanaojiita wahariri wamepewa sana ma T shirts ya SSRA na huyu Irene Isaka.

Amekuwa pia akiwapa mishiko ya hela ( sio hongo... eee!) kila mara ili sijui kuwaziba midomo.
Ifanyike audit ya kufa tembo pale SSRA huenda kuna zaidi ya kuwadharau na kuwadhulumu wafanyazi.
Official yeyote fisadifisadi huwakumbatia sana wahariri. Ana mengi ya ku hide huyu. Hata Sara Kibonde analijua hili kwani yeye ndio hugawa hizo fulana, pesa na kalenda to the idiotic and hypocritical editors.

Bye bye Irene. Kusoma sio kila kitu.
 
Back
Top Bottom