Kama ingelitokea msanii Mkristu akashutia video yake Msikitini

Kama ingelitokea msanii Mkristu akashutia video yake Msikitini

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,360
Reaction score
11,588
Kutokana na kejeli za Diamond Platinumz juu ya kanisa Katoliki, imeonekana wazi kuwa kitendo alichokifanya sio cha haki wala heshima!

Hata isitoshe kauli yake kwenye post ya Zuchu aliyoandika kuwa hii nchi ina wenyewe mara acha tuendelee kuwawakilishia taifa lao inaonesha wazi mmomonyoko mzima wa maadili!

Unahisi tungelikuwa tunaongelea habari gani kwa sasa kama angelitokea msanii Mkristu akashuti video ya wimbo wake akiwa Msikitini?

Na je, viongozi wa Msikiti husika wangekubaliana na jambo kama hili lifanyike?
 
Kutokana na kejeli za diamond platinumz juu ya kanisa katoriki, imeonekana wazi kuwa kitendo alichokifanya sio cha haki wala heshima!

Hata isitoshe kauli yake kwenye post ya Zuchu aliyoandika kuwa hii nchi ina wenyewe mara acha tuendelee kuwawakilishia taifa lao inaonesha wazi mmomonyoko mzima wa maadili!

Unahisi tungelikuwa tunaongelea habari gani kwa sasa kama angelitokea msanii mkristu akashuti video ya wimbo wake akiwa msikitini?

Na je, viongozi wa msikiti husika wangekubaliana na jambo kama hili lifanyike?
Makanisa yenyewe yamejengwa na binadamu hao hao ambao ni walevi na wazinzi, hizi dini zina vuruga akili zenu
 
Makanisa yenyewe yamejengwa na binadamu hao hao ambao ni walevi na wazinzi, hizi dini zina vuruga akili zenu
Ndo maana sometimes naona ni bora nibaki na dini yangu mwenyewe, niamke asubuhi niseme Asante Mungu, jioni niseme Mungu Nilinde! Haya mambo ya viongozi wa kanisa kupewa pesa ili kudhihaki kanisa inachukiza sana! kama yule mwongoza kwaya alivyokuwa anapanua lile domo huku akiiangalia camera! Dah!
Diamond platinumz unakuta na yeye alikuwa ndani ya kanisa na lukamba, wanafunga camera kwenye msalaba! [emoji26]
 
Hivi mbona watz tunazidi kuwa wapumbavu kila kukicha hivi hapo Daimond ana kosa gani?

Kwani walienda wakalivamia kanisa na kuwashikia bunduki viongozi wa hilo kanisa na karekodi kwa razima?

Mpaka anakuja kufanya hicho alicho kifanya ina maana alipata baraka zote kutoka kwa viongozi wa kanisa husika na waliona hakuna tatizo yeye kufanya hivyo.
Sasa hapo Daimond ana kosa gani?
Wakulaumiwa ni wale walio waruhusu kifanya walicho kifanya.

Hizi hoja za sijui kwa nn hawajaenda msikitini ni hoja za kipumbavu kwa sababu msimamo wa viongozi wa kiislam uko wazi kabisa ya kuwa hayo mambo hayaruhusiwi ndani ya msikiti ,wakati upande wa viongozi wa pili ni rukusa na tumeshudia mara nyingi miziki na maigizo yakofanyika ndani ya makanisa tena waigizaji wakiwa wamevaa nusu uchi mbona hamkuwahi kusema huko nyuma?

Hata wanawake siku hizi wamekuwa wanaenda makanisa kwenye ibada na mavazi ya ajabu ajabu tukisema mnajitetea eti mungu ahaangilii mavazi bali ana angalia matendo.
 
Bora darasa la 7 kuliko kiongozi wa dini, maana darasa la 7 yupo huru, ila kiongozi wa dini kafungwa na mafundisho yake tuuu
Hapo Ni Kama yalivyo MAGAZIJUTO mixer mgagani lazima kila siku alikua anawapa kesi iko inashinda Vita kwa watu watatu fogo hata Kama hawapapendi Ndio Matatizo ya itatakiwa wabaki huko huko island.
 
Haitatokea Kwa sababu Waislamu wanaisimamia Dini yao.
Isitoshe misikiti inamilikiwa na Waumini Wote, hivyo hata uwe kiongozi Wa msikiti mfano Imamu, huna mamlaka ya kuamua hivyo.

Kwa wakristo Makanisa yanayomilikiwa na Waumini Wote ni ya Romani Katoriki, KKKT na Wasabato lakini sina uhakika na viongozi wa kanisa katika kuamua.

Ukija kwa haya makanisa ya Pende Coast yaani walokole, makanisa ni mali ya mchungaji, Mchungaji ndiye huamia kila kitu, si lazima kuwashilikisha Waumini.
Hivyo mchungaji mwenye njaa yake, ni rahisi kuchukua pesa na kuruhusu Diamond kurekodi ndani ya kanisa.
 
Kutokana na kejeli za diamond platinumz juu ya kanisa katoriki, imeonekana wazi kuwa kitendo alichokifanya sio cha haki wala heshima!

Hata isitoshe kauli yake kwenye post ya Zuchu aliyoandika kuwa hii nchi ina wenyewe mara acha tuendelee kuwawakilishia taifa lao inaonesha wazi mmomonyoko mzima wa maadili!

Unahisi tungelikuwa tunaongelea habari gani kwa sasa kama angelitokea msanii mkristu akashuti video ya wimbo wake akiwa msikitini?

Na je, viongozi wa msikiti husika wangekubaliana na jambo kama hili lifanyike?
Labda alitumwa
 
Shida sisi tuna mihemko kwenye dini.

Kanisa/msikiti kuna uongozi wake, DOMO platnumz hakuvamia tu, ila ni kwa ruhusa ya jengo husika, viongozi waliona ni sahihi kwa mujibu wa mafundisho yao wakamruhusu.
Hata msikitini wanaweza ruhusu ama kukata kwa jinsi watakavyoona wao inafaa.

Kwani ile ZOBA ya ndizi[emoji529]zorro ishafungiwa? kuna maudhui wapo kanisani.
 
Back
Top Bottom