Kama hutaki watuhumiwa watetewe, wapeleke gerezani moja kwa moja!

Kalesya

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
691
728
Watu waliotangulia na kuweka mifumo ya haki, Sheria na Utawala bora walikuwa na akili nyingi na busara kubwa sana. Na hili halikufanyika kwa siku moja bali ni mchakato(process) iliyojengwa na kutimia kwa karne nyingi sana.

Zamani ulikuwa unakuta kwenye jamii kuna Mfalme(King) ambaye anatunga Sheria(yeye ndiye Bunge) anazisimamia Sheria hizo(yeye ndiye Polisi) na anazitafsili Sheria hizo na kutoa hukumu(yeye ndiye Mahakama). YANI KILA KITU NI YEYE, UKIINGIA KWENYE ANGA ZAKE HIZO HAKUNA PA KUTOKEA.

Watu wengi walifungwa au kuhukumiwa kifo kwa chuki tu na kusingiziwa( wapinzani wengi au wote wa Mfalme walimaliziwa hapo).

Watu wenye busara wakaliona hilo, ikaanza process ambayo ilikuja kuzaa Bunge, Serikali/Utawala na Mahakama ili kuleta usawa na haki kupatikana kwa kila chombo kufanya kazi tofauti na kingine.
Maelezo ni marefu acha niyakatishe!

Mtuhumiwa hawi mkosaji mpaka idhibitike kuwa katenda kosa husika pasipo kuacha chembe ya shaka yeyote. Hata kama unadai kakutwa na ushahidi mikononi ni lazima ujiulize maswali yafuatayo:

1. Huo ushahidi umepatikana kihalali? Hajabambikiwa?
Kuwa na ushahidi ni kitu kimoja, na jinsi ushahidi huo ulivyopatikana ni kitu kingine tofauti na vyote ni muhimu Kisheria.

2. Mahakama kazi yake ni nini? Ni kupitia ushahidi huo, kuangalia uhalali wake Kisheria, ulipatikana muda gani na wapi? Ulipatikanaje na alikuwepo nani na nani wakati ukipatikana? Sheria na taratibu za kukusanya ushahidi vilifuatwa? Hakuna uongo na ubambikaji?

Baada ya kujiridhisha na yote hayo(na mengineyo ambayo sijayataja) ndipo Mahakama hutoa hukumu stahiki kama mtuhumiwa sasa ni mkosaji kamili au hapana.

Maelezo ni mengi juu ya swala hili, lakini nimalizie tu kwa kuuliza maswali:
1. KAMA HUTAKI MAHAKAMA IFANYE KAZI YAKE YA KUHAKIKI NA KUPITIA USHAHIDI, KWANINI UNAWAPELEKA WATUHUMIWA HAO MAHAKAMANI?

2. KWANINI BASI USIWAPELEKE JELA MOJA KWA MOJA TU?

3. JE UNATAKA WATU WALIOBAMBIKIWA KESI NA USHAHIDI WAFUNGWE TU BILA KUPATA HAKI YA KUTETEWA?

4. NANI ASIYEJUA KUWA KUNA POLISI NA WANASIASA NI MABINGWA WA KUBAMBIKIA WATU KESI?
 
Ngoja waje.waombaji
 
Nasubiri kama movie yenye season
Ngoja tuone maana naona
ndani ya hii nchi kuna watu matamko yao ndio sheria kabisa moja kwa moja
 
Back
Top Bottom