Kama Hupendi Basi Ipotezee

Kama Hupendi Basi Ipotezee

Ndallo

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2010
Posts
7,621
Reaction score
4,312
Prof.jpg
Mkongwe kwenye Game, Profesa Jay leo ameandika historia nyingine tangu atangaze kuingia rasmi kwenye jukwaa la kisiasa.

Unajua kwamba jamaa alitangaza rasmi kuvaa gwanda la CHADEMA sasa leo ameendelea kuandika historia nyingine, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Profesa Jay ameweka picha nane akionyesha shughuli za ufunguzi wa tawi jipya la CHADEMA huku akihamasisha wananchi kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la makazi na kisha kupiga Kura.


Hiki ndicho alichokiandika; “..Kuhamasisha wananchi kujiandikisha na kisha kupiga KURA. …. Hamasisha na kwa watu wako ili wajitambue na kunitumia vema HAKI yao ya kuchagua viongozi wao kwa maendeleo yao!!!…”- Prof. Jay “..Ufunguzi wa matawi mapya, Ujengaji wa chama na uhamasishaji kwa wananchi kujiandikisha kwenye daftari la makazi na kisha kupiga KURA! !!..”
 
Ama kweli shuguli na shuguli ni watu na tutajitahidi kujiandikisha na kutunza shahada kavizuri kangu poa ni safi hiyo ka kijewe kazuri hapo
 
Huyo ndio mwanaharakati joseph haule
Sioni mtu wa kumzuia asiingie mjengoni 2015
 
Mimi nilishamuunga mkono huyu jamaa bado wenzangu tu. Tujitahidi kuwaunga mkono wana harakati kama hawa ili tuiue CCM mwakani na kama ikiwezakana tuwafunge maisha marais wao waliopita kasoro Mwl. Nyerere.
 
2015 hapo mjengoni -Kulia yupo Sugu - Kushoto yupo Mzee wa Mitulinga sikilizia mistari yenye vina!
 
safi sana kawaponda kwenye mashairi ya nyimbo zake hawakusikia sasa kaamua apambane nao mjengoni
 
Back
Top Bottom