Kama humjui, huyu ndiye Mustafa Sabodo!

Kama humjui, huyu ndiye Mustafa Sabodo!

BILIONEA SABODO AFARIKI DUNIA..

Bilionea na Mchumi maarufu nchini, Mustafa Jaffer Sabodo amefariki Dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwakwe, Masaki jijini Dar es Salaam.

"Mzee amefariki leo alfajiri akiwa nyumbani. Taratibu za mazishi zinaendelea na atazikwa katika makaburi yaliyoko mtaa wa Bibi Titi Mohamedi karibu na CBE," amesema Danstan.

Marehemu Sabado alizaliwa mkoani Lindi na alikuwa akifanya biashara katika nchi za Ufaransa, India, Kenya, Sudan, Nigeria, Zimbabwe na Tanzania.

Atakumbukwa kwa mchango wake ulioanzisha Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery alipotoa msaada wa Sh milioni 800. Alihusika katika utoaji wa misaada kadhaa iliyohusisha kilimo, ujenzi wa visima na kusaidia wenye uhitaji.
Sabodo atazikwa leo saa 4:30 usiku.
Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un.
“We surely belong to Allah and to Him we shall return”
"Sisi sote ni wa Mola, na kwake tutarejea".

Paskali pia anakuaga!.
RIP Jaffar Sabodo.
 P
Vp mabilionea wa sasa mbona hatuwaoni wakitoa misaada ya kimaendeleo kwa jamii
Wao kutwa kuwaita wasanii na machawa tu wanaongozana nao

Ova
 
Back
Top Bottom