Kama humjui, huyu ndiye Mustafa Sabodo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama humjui, huyu ndiye Mustafa Sabodo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 2, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Na Tausi Ally | Mwananchi

  WIKI iliyopita Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilitoa kibali cha ujenzi wa jumba la ghorofa 14 kwa mfanyabiashara Mustafa Jaffer Sabodo.

  Kibali hicho kilikabidhiwa kwake na Meya wa Ilala, Jerry Silaa katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  Lakini, unaweza kujiuliza, je, huyu Sabodo ni nani, ametokea wapi hadi kuweza kupata umaarufu ule alionao nao?

  Swali hilo linajibiwa naye ambaye licha ya kupooza sehemu ya mwili wake mwaka 2000, ameendelea kufanya kile anachotaka ikiwemo kusimamia miradi yake na ya jamii kuhakikisha inafanikiwa.

  Mei 14 mwaka huu, Sabodo alitimiza miaka 70, huku akiwa amekwishajitolea vitu vingi vya maendeleo kwenye jamii ya Watanzania ikiwemo kuwachimbia visima zaidi ya 280.

  Anasema katika mahojiano kwamba hali hiyo aliyokuwa nayo haimzuii kufikia malengo yake.

  Anasema yeye alizaliwa mwaka 1942 mkoani Lindi na kwamba ametoka kwenye familia yenye utajiri wa imani na fedha.

  "Mimi nimetoka kwenye familia ya Uislamu wa Kihindi wa Gujarati Khoja, nilijitahidi kupambana dhidi ya umaskini nikiwa na matarajio ya kuwa tajiri na ninamshukuru Mungu nimekuwa hapa nilipo,"anasema.

  Anafafanua kuwa licha ya kutoka kwenye familia ya utajiri baadaye alifilisika na akapambana dhidi ya kufilisika huko kwa kuweka matarajio ya kuwa tajiri kama alivyo sasa.

  Akizungumza katika hafla ya kuzaliwa kwake, Sabodo anasisitiza kuwa hali yake aliyonayo kwa hivi sasa haimzuii kufanya chochote anachohitaji katika harakati za kuikomboa jamii inayohitaji msaada wa kuwekeza kwenye maendeleo ya muda na mfupi yakiwemo ya elimu na afya.

  Kielimu, Sabodo anasema kuwa alisoma Shule ya Sekondari ya Lindi na baadaye alihitimu ngazi ya cheti kwenye Chuo cha Cambridge.

  "Wakati nasoma nilikuwa ni mmoja kati ya wanafunzi wazuri darasani katika kipindi hicho kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya wenzangu wengi,"alijinasibu.

  Akizungumza kwa tabasamu jepesi, wakati amepumzika nyumbani kwake, Upanga jijini Dar es Salaam, Sabodo ambaye jina lake lilianza kama utani kutokana na fujo zake anasema baadaye alihitimu Chuo cha Edinburg nchini Uingereza mwaka 1965 ambapo alisoma sheria ya biashara na usimamizi wa mifuko ya fedha.

  ‘Kozi hizi zilinisaidia mimi mwenyewe kujiletea mafanikio makubwa na kuwa mshauri wa kampuni, nimejikita zaidi katika masuala ya madeni ya kimataifa na uwezeshaji, "anasema.

  Anaongeza kuwa yeye ni mmoja kati ya wafanyabiashara wakubwa na biashara zake zimesambaa kwenye nchi mbalimbali zikiwemo Tanzania, India, Ufaransa, Kenya, Sudan na Zimbabwe.

  Anasisitiza kuwa kutokana na uchapakazi wake na kuamini katika ukweli amekuwa ni mtu mwenye mafanikio aliyoyatarajia kuyafikia na kwamba ameyafikia kwa kila kiwango ukitofautisha na matajiri wengine ambao utajiri wao umepatikana kwa bahati au kurithi kutoka kwa wazazi wao.

  Anasema yeye hayupo kwenye kundi hilo ambalo wengi wao huutumia utajiri huo wa familia vibaya, kwa kuwa amezaliwa kwenye familia mashuhuri na kuondoa vikwazo vyote vinavyomfanya mtoto wa familia ya kitajiri kutafuta utajiri wake yeye mwenyewe.

  Anafafanua kwamba mafanikio yake aliyapata kutokana na kujishughulisha. "Niliamua kupambana ili niwe hivi nilivyo sasa kutokana na kuvutiwa na mafanikio ya babu yangu, akiongeza kuwa alikuwa akitaka kuwa mtu tariji.

  Baadaye niliishi nje ya Tanzania kwa kufanya kazi ya ushauri wa kimataifa na kurejea nchini mwaka 1996 na kuwekeza.

  Anasema amezunguka nchi mbalimbali za Afrika, Asia , Ulaya na Mashariki ya Kati na kwamba sasa safari zake anazielekeza nchini India kwa ajili ya kupata matibabu.

  Akizungumzia moyo wake wa kujitolea, Sabodo anasema mwaka 2003 alitoa udhamini wa uchezeshaji wa bahati nasibu ya mfuko wa Mwalimu J.K Nyerere wenye thamani ya Sh 100 milioni.

  Anabainisha kuwa wazo la kuanzishwa kwa mfuko huo wa Mwalimu Nyerere lilikuwa ni lake, pia alichangia Sh 1.3 bilioni katika kuufanikisha.

  Pia, anasema amechangia miradi mbalimbali ikiwemo kutoa kiasi cha Sh5 bilioni kwa ajili ya kuchangia chuo cha ualimu cha elimu ya juu cha Mtwara, alichangia Sh 965 milioni kwa ajili ya upanuzi wa majengo ya hospitali ya Shree Hindu Mandal, mradi wa Khoja Shia-aheri Sh 1.6 bilioni.

  Ni wapi alikojifunza moyo huo wa kujitolea, naye anajibu, "Hakuna shule inayomfundisha mtu kutoa kitu, bali ni kitu kinachotoka moyoni mwake na unapokuwa unatoa unatengeneza nafasi ya wewe kupata."

  Kuhusu mafanikio yake, Sabodo anasema anamkumbuka babu yake ambaye alihitaji kuwa mkombozi wa watoto kwa kuwajengea kituo cha Ultra-Moderm katika kiwanja kilichopo karibu na makazi yake yaliyopo Mtaa wa Magore, Upanga.

  Lakini, tumaini lake kubwa linategemea Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)ambalo limempatia mwekezaji mwingine eneo hilo.

  Je, ameshauacha mradi huo, anajibu kuwa mradi huo ni wa faida ya watoto wanaohangaika kupata maeneo ya kupumzika na burudani hapa jijini Dar es Salaam.

  "Sitaki kukata tamaa nitafuata taratibu zote kuhakikisha mradi huo unakamilika," anaeleza.

  Akizungumzia kuhusu misaada anayoitoa ikiwamo kwa vyama vya siasa kama CCM na Chadema, anasema misaada yake haina dini maalum bali inatolewa kwa ajili ya mioyo ya watu wanaohitaji na ya kibinaadamu.

  Anasema dini yake yeye ni kupenda watu hususan wale wanaohitaji msaada kwa kuwawekea uwekezaji wa muda mrefu kama shule, hospitali pamoja na miradi ambayo itawanufaisha watu sawa ukiachana na dini zao.

  Anawahamasisha watu wawe na moyo wa kujitolea kama wake, pia anasema aina yoyote ya utoaji ni muhimu kwa wanaohitaji kama vile pesa, muda, ujuzi, upeo na hata usikilizaji.

  Kwa upande wa mchango katika elimu, anasema anajihusisha katika shughuli za uchumi na maendeleo ya kijamii kwa kutoa mabilioni ya Shilingi kwa kupunguza umaskini na kukuza miradi ya kijamii na afya.

  Sabodo pia amejenga kituo cha elimu cha Sabodo Education Centre kilichopo kijiji cha Mayanda umbali wa kilometa 16 kutoka Mtwara mjini.

  Sabodo ambaye anajenga jengo la ghorofa 14 la maegesho ya magari yenye uwezo wa kuegesha magari yapatayo 300 kwa wakati mmoja litakalogharimu dola za Kimarekani 3 milioni jijini Dar es Salaam, katika harakati za kupunguza tatizo la maegesho ya magari linalolikabili jiji la Dar es Salaam na kuboresha huduma hiyo.

  Aprili 5, mwaka huu, Sabodo licha ya kuwa mwanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ametoa Sh 100 milioni kwa ajili ya kukipongeza chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),kwa ajili ya ushindi wa kiti cha ubungo alichoshinda Joshua Nasari wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.

  Pia alitoa baskeli 100 na kuahidi kuchimba visima vitano katika jimbo hilo.


  CHANZO: Kama humjui, huyu ndiye Mustafa Sabodo!
   
 2. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  He is my role model
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Afi sana mzee Sabodo tunajifunza mengi sana kutoka kwako....sio wale wengine wanaficha mipesa nje hadi wanakufa hawajazungusha hapa nyumbani kuleta maendeleo na ajira!!
   
 4. k

  kijiichake JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 285
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kuna jambo moja nimelipenda sana katika misemo ya sabodo nalo nitalifanyia kazi kwa nguvu zangu zote nalo ni (kutoa ndiko kupata) amini usiamini mkono gamu utaishia na ugamu wake. Unachokipanda ndicho utakacho vuna. Toa ulicho nacho, ili upewe usichonacho. Tarajia kuvuna ulichopaoda ukipanda urasimu utavuna kurasimiwa. Ukipanda uchoyo utavuna kunyimwa, ukipanda kujitolea utavuna kupewa. Sabodo ameniamsha usingizini kwa msemo huu. Asante sana sabodo
   
 5. Sunshow

  Sunshow JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 943
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mungu amzidishie miaka ya kuishi ndugu yetu Sabodo nafurahi sana kwa jinsi anavyojitolea kuisaidia jamii maskini ya kitanzania. Ikumbukwe pia kutoa ni moyo maana licha ya kuwa na pesa nyingi angeweza kujijengea mahekalu ya kuishi na kununua vitu vya kifahari.
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Hilo Jengo(Parking Lot) lipo sehemu gani?
   
 7. chelsea fc

  chelsea fc JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 835
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  pesa ipo,unatoa ukiwa nacho!
   
 8. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Jamaa ni soo, ana moyo wa ubinadamu haswa!
  Jamaa wa dini yake wangekuwa wote wana moyo kama wake, dunia ingepata amani.
   
 9. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Sabodo uko juu Mungu akubariki na kukuponya huo ugonjwa
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkubwa Sabodo!....Mwenyezi Mungu akuongezee mara dufu pale unapotoa,uzidi kuishi maisha marefu yenye afya na baraka tele.Watanzania na hasa wapenda mageuzi tunakupenda sana na bado tunaitaji mchango wako.Mungu akubariki sana
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  mhindi anapotoa hela watu wengine wanakuwa na mashaka..mimi sina mashaka sana na huyu somji
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sabodo ni mfano wa kuigwa kwa matajiri wa kibongo.
   
 13. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Sipati picha kama sabodo angekuwa ame-base kwa magamba tu na huwa anaiponda CDM na kuipaka matope na wala angekuwa hajafanya chochote kwenye CDM.....!

  Du humu ndani leo pasingekalika maana kila mtu ungesikia mwizi huyo, gamba hilo...... Gosh!

  HONGERA SABODO KWA MAANA ULINIFURAHISHA PALE AMBAPO ULIKUWA BEGA KWA BEGA KUISADIA CDM LAKIN ISINGEKUWA HIVYO NINGEKUDIS MPAKA UNGEJUTA KUZALIWA.
   
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  ila mkuu hawa wahindi na waarabu ni watu wa kuangaliwa kwa jicho la 3.. Mm huwa siwamin sana maana ninawajua fika tabia zao ila labda kwa sabodo yy yupo tofauti na wengine.
   
 15. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #15
  Jun 2, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Makanjabay wengi huwa waoga wa kuchangia vyama vya upinzani. Lakini Sabodo amekuwa mkanjabay wa namna yake!
   
 16. S

  Sir Leem JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 564
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ikiwa huwaamini sana wahindi na waarabu ni akina nani unaye waamini sana au kabila lipi unalo liamini lina utakatifu kuizidi hao?Ambalo wewe utaliamnini
   
 17. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkubwa!....tena amekuwa wa kwanza kuchangia hadhalani,kitu ambacho kimewashinda matajiri wengi
   
 18. Simbajr

  Simbajr Senior Member

  #18
  Jun 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2010
  Messages: 186
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kudos Sabodo... Mwambie na Sir Andy Chande nae ajitoe kwa wananchi

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 19. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Ki-ukweli huyu mzee kavunja miiko na tamaduni kibao za kisias na kijamii.
  He's probably done enough to earn a rightful place in the hall of fame in Tz. May he have a good finish to all he started.
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2012
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Nimempenda. Na nilichojifunza ni kujitafutia utajiri kwa nguvu zako na sio kutegemea wa kurithi. Ila kuna moja limenitatiza la kupewa kibali na meya halafu na kufanya hafla, hapo sielewi why? kuna ugumu wa kupata vibali vya ujenzi?
   
Loading...