Kama Hujawahi, Bado hujui

Kama Hujawahi, Bado hujui

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,080
Reaction score
79,467
KAMA HUJAWAHI, BADO HUJUI

Na, Robert Heriel

Kama hujawahi kusalitiwa bado huyajui mapenzi
Kama hujawahi kupigana bado huijui vita
Kama hujawahi kufanya dhambi kubwa bado huujui msamaha.
Kama hujawahi kupenda bado huujui wivu

Kama hujawahi kuwa masikini bado hujui kudhalilika
Kama hujawahi kudhulumiwa bado huijui haki
Kama hujawahi kufiwa na umpendaye bado hukijui kifo
Kama hujawahi pata ajali bado hujawa dereva

Kama hujawahi kufeli bado huyajui mashindano
Kama hujawahi kuchepuka bado huujui uongo
Kama hujawahi kufungwa bado huujui Uhuru
Kama hujawahi kupata shida bado huujui upweke.

Kama hujawahi kuota ukilala bado huujui Usingizi
Kama hujawahi kutoa sadaka bado hujui ibada
Kama hujawahi kutoa msaada bado huyajui mafanikio

Kama hujawahi kutunza bado hujui kupenda
Kama hujawahi kuishi na mwanamke bado huujui uanaume wako
Kama hujawahi kuishi na mwanaume bado huujui uanamke wako

Kama hujawahi kutapeliwa bado hujui uaminifu
Kama hujawahi kusoma bado hujui maarifa
Kama hujawahi kuwa uchi basi huujui uchi wenyewe
Kama hujawahi kuwa kiongozi bado huijui lawama

Kama hujawahi kufeli mtihani bado hujui kujifunza
Kama hujawahi kusafiri bado hujui kuishi, hujui maisha
Kama hujawahi kuheshimu wazazi wako bado hujui kuheshimiwa
Kama hujawahi kukopwa pesa na mtu bado hujui namna ya kumuomba Mungu

Kama hujawahi kumtii mume wako bado hujui kupendwa na mumeo
Kama hujawahi kumpenda mkeo bado hujui/hujawahi kuheshimiwa naye
Kama hujawahi kuchimba shimo bado hujui kutumbukia
Kama hujawahi kupanda juu bado hupajui chini
Na kama hujawahi kushuka chini bado hupajui juu

Kama hujawahi kulogwa bado huujui uchawi
Kama hujawahi kufanyiwa muujiza bado humjui Mungu

Ukiona mambo yako yanakuendea tuu pasipo shida yoyote
Ukiona kila mtu anakusaidia hata kama hujamuomba
Ukiona kila mtu anakupenda na kukujali
Ukiona kila mtu anakuhurumia na kubeba matatizo yako kama yake.

Ukiona mambo yote hayo jua umekufa. Hiyo ndio maana halisi ya Kifo.

Lakini ukiona unapata hekaheka, unapanda na kushuka, husaidiwi hata unapohitaji msaada, unapendwa kwa sababu, hauonewi huruma basi jua kuwa bado unaishi. Hiyo ndio maana halisi ya kuishi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
IMESHIBa hii Mkuu.
 
Back
Top Bottom