Kama hela zake hazionekani mwachishe hiyo kazi anaaga ana kwenda wapi umuhudumie mwenyewe

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,945
5,849
Ndugu zangu wana Jf na wasio wana Jf na wasalimu sana katika jina la Mwenyezi Mungu aliyeziumba mbingu na nchi na vyote viijazavyo dunia ikiwemo hawa watoto wazuri wa kike mauwa ya mioyo yetu.

Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu iwatetee watu wote walioachwa peke yao. Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki wapatie maskini na wahitaji haki yao

Tusipo fumbua vinywa vyetu kupinga unyonyaji uliojificha kwenye kichaka cha mahusiano na ndoa hakuna haki itapatikana, wanaume wengi ni bubu hawawezi kuyasema haya hadharani.

Waliosema hela ya mwanamke sio yako ni waongo na wapotoshaji, ukweli ni kwamba kama sio yangu basi ni yetu ni waweke wazi leo hii maana tuu mwili mmoja

Mt 19:6
Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.

Mk 10:8
na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.

Huwezi kuwa mwili mmoja na mwanamke anayefanya kazi alafu anaficha kipato chake huyo siyo mwaminifu ni msaliti , kama hataki mwachishe kazi haraka sana.

kumbukeni pia:;

alipo sema "asiyefanya kazi na asile alimaanisha kitu gani na alipo sema mwanaume akaumbiwa msaidizi wa kufanana nae alimaanisha kitu gani"

Wanawake wa kizazi hichi si wasaidizi ni wanyonya damu na malayer waliojificha kwenye kichaka cha mapenzi na ndoa tena ni wezi wa wazi wazi ijapokua hawakamatwi wanafichwa ndiyo maana taasisi ya ndoa inazidi kuhangamia na ipo siku itakuwa haipo tena hakika.

Tuna tambua siku zote mwanamke hakuumbwa kuwa mzigo kwa mwanaume wala kuwa mnyonyaji kwa mwanaume aliumbwa kuwa msaidizi na hapa ndipo tunapopata maana ya mke mwema, Mwanamke hakuumbwa kuficha kipato chake bali aliumbwa kuwa mwili mmoja na mwanaume na kutumia kipato chake kuleta chakula kutoka mbali na kuwapa watu wa nyumbani mwake chakula, hali chakula cha uvivu na moyo wa mumewe umwaminina hiyo ndiyo maana halisi ya mwanamke kuumbwa kuwa mke mwema na kuwa mwili mmoja na mwanaume ,msaidizi wa mwanaume na sii mzigo wala mnyonyaji . sasa wewe mwanamke unayefanya kazi kwanini ufiche hela zako umnyonye mwezako ili hali unasema una ndoa nae, hiyo ndoa ipo wapi kama siyo kutaka kumuua mwezako?

rejea haya maandiko:;-

Mithali 31:8-17,19,24-27
[8]Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu;
Uwatetee watu wote walioachwa peke yao;
[9]Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki;
Uwapatie maskini na wahitaji haki yao.
[10]Mke mwema, ni nani awezaye kumwona?
Maana kima chake chapita kima cha marijani.
[11]Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato.
[12]Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake.
[13]Hutafuta sufu na kitani;
Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
[14]Afanana na merikebu za biashara;
Huleta chakula chake kutoka mbali.
[15]Tena huamka, kabla haujaisha usiku;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula;
Na wajakazi wake sehemu zao.
[16]Huangalia shamba, akalinunua;
Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
[17]Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi;
Hutia mikono yake nguvu.
[19]Hutia mikono yake katika kusokota;
Na mikono yake huishika pia.
[24]Hufanya nguo za kitani na kuziuza;
Huwapa wafanya biashara mishipi
[25]Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake;
Anaucheka wakati ujao.
[26]Hufumbua kinywa chake kwa hekima,
Na sheria ya wema i katika ulimi wake
[27]Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake;
Wala hali chakula cha uvivu.

Enyi wana wa adamu ni nani alie waloga, ni nani aliye wafanya mkawa wajinga kiasi hicho. huyo mwanamke angelikua kipato chake hakionekani je, mumewe angemuamini, angelikua anaficha hela (mapato ya mikono yake )zake je, kungekua na mke hapo, jiulizeni watu wote huyu mwanamke hapo angelikua anakula chakula cha uvivu kama hao wake zenu na wachumba zenu je, kungekua na mahusiano hapo pia jiulizeni ni wapi alikua anapiga mizinga na kuomba omba hela za mwanaume.

Enyi wanadamu jiulizeni angelikuaje mwili mmoja na msaidizi wa mwanaume kama kipato chake hakionekani kina fanya nini. huyo alinunua shamba, alileta chakula kutoka mbali, aliwapa watu wa nyumbani mwake chakula , alisokota sufu alikua ni mfanya biashara na hela zake zilionekana ndiyo maana moyo wa mumewe ulimwamini..

sasa huyo wa kwako anakuaga asubuhi anaenda wapi kama mapato yake hayaonekani anakuaga anakwenda wapi kama hawezi kuleta chakula nyumbani mkala, anakuaha anakwenda wapi kama hawezi kutoa hela mkachanga na kununua shamba likawa la kwenu, huyo mkeo anakwenda wapi jiukizeni mioyoni mwenu na mjihukumu hakika wenyewe.

maana mimi na hukumu kwa haki nikisema kama hela za mwanamke wako hazionekani zinakwenda wapi na zinafanya nini mwachishe kazi umuhudumie mwenyewe ili muwe mwili mmoja nasiyo wawili tena
 
I concur,
Kama anaamka saa 11 alfajiri anashindwa hata kuandaa watoto shule, anashindwa kuwapikia mchana na kuwaogesha, chores zote za nyumbani kahamishia kwa msaidizi au wote tunafanya, basi ni LAZIMA kuwe na input kwenye anachofanya. Otherwise awake makalio home ahudumie watoto.

Lile kundi linalosema hela ya mwanamke haiulizwi nawapa pole sana.
 
I concur,
Kama anaamka saa 11 alfajiri anashindwa hata kuandaa watoto shule, anashindwa kuwapikia mchana na kuwaogesha, chores zote za nyumbani kahamishia kwa msaidizi au wote tunafanya, basi ni LAZIMA kuwe na input kwenye anachofanya. Otherwise awake makalio home ahudumie watoto.

Lile kundi linalosema hela ya mwanamke haiulizwi nawapa pole sana.
Hela ya mwanamke lazima iulizwe kwa sababu unapo muoa mwanamke chochote anachofanya ni chenu wote kwa sababu ni mwili mmoja. Tofauti na hapo akae nyumbani apike pike na kuogesha watoto
 
Kazi ya mwanamke ni kuzaa na kulea, mwanamke ni mtunza kiota/nyumba na sio mtafutaji.

mwanaume ameumbwa awe mtafutaji/mpanaji kusudi uhai upate kulishwa na kudumishwa kwa chakula, malazi na mavazi.
 
Kazi ya mwanamke ni kuzaa na kulea, mwanamke ni mtunza kiota/nyumba na sio mtafutaji.

mwanaume ameumbwa awe mtafutaji/mpanaji kusudi uhai upate kulishwa na kudumishwa kwa chakula, malazi na mavazi.
Nime ambatanisha na maandiko matakatifu nionyeshe wapi mke siyo mtafutaji , acha kuwafundisha wanawake uvivu na unyonyaji
 
  • Thanks
Reactions: apk
Soma bandiko langu lote alafu urudi hapa
Ninesoma lote mkuuu.

1. Ni unatumia maandiko vibaya
2. Mwanamke hakuumbwa kutafuta na kulisha familia, ndio msingi wa migogoro yote inaanzia huko sababu tumekiuka malengo ya uumbaji, angali hata tofauti za mwanamke na mwanaume zilivyo k8maumbile, nguvu, kujali, kutunza, malezi, misuli nk utanielewa. Wewe unajaribu kurekebisha kitu ambacho kinamakosa tayarii kwenye msingi wake (sio mshahara wa kazi ya mwanamke uletwe mezani, ni HAKUPASWA KUFANYA KAZI KABISA), Tumeruhusu waingilie majukumu yasio ya kwao totally, hivyo hakuna haja ya kuwalaumu maana level ya ubibafsi na uchoyo walionayo wanawake (hatujui kwanini Mungu aliwaweka na level hiyo ya ubibafsi na uchoyo)
 
Back
Top Bottom