Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,096
- 22,826
Kumekuwa na malalamiko sana ya kimahusiano. Wenza wakilalamika kushindwa kufika katika ndoto za mahusiano bora yaani ndoa na kuanzisha familia na kudumu milele hadi uzee. Hii ni kweli inatokea sana. Sababu hutolewa nyingi sana na kila upande ukisema lake.
Leo napenda kuzungumza machache kuhusu nilichojifunza kuhusu tabia za watu ambazo hawazionyeshi ila huathiri mahusiano na kuathiri wengine.
Hivi huyu mwenzako ulienae kimahusiano ambaye umemjua akiwa na miaka 20+ umeshawahi jiuliza huyu anatoka katika background ya aina gani hadi hapo unapokutana naye?
Unajua alipitia malezi gani kipindi cha tokea utotoni mwake hadi anatimiza miaka 18?!
Nani alikuwa na bado ni mentor au idle figure wake ambaye ndie anamtumia kama mfano wa kuigwa tabia na haiba yaani ni nani kwake ni role model wa maisha yake?!
Anaishi kwa falsafa ipi ya kimahusiano?! Je anaamini katika upande wa maamuzi na fikra nje ya vitabu vya MUNGU,anaamini katika vitabu vya MUNGU ila ni mwanakondoo aliyepotea au anaamini katika vitabu vya MUNGU na anashika njia zake zote kwa nguvu zake zote bila kushikiwa akili wala kuhimizwa?!
Kama umeamua kuanzisha mahusiano serious na mtu ni vema ukajipa nafasi ya kujua huyu mtu alikuzwa na kulelewa vipi. Vijana na mabinti wengi katika jamii yetu hawajalelewa kwa upendo na kujaliwa katika makuzi yao ya utotoni hadi wanakuwa watu wazima na kuondoka nyumbani wanaondoka na spirit ile ile ya nyumbani kwao.
In short wamekuzwa katika survival mode ambayo huwataka wawe butu kihisia na kutofeel chochote sababu ya kuzoea hisia za maumivu na kuwa insensitive katika kuhisi maumivu ya wengine.
Na ndio maana siku za hivi karibuni kumekuwa na idadi kubwa ya vijana/mabinti ambao kadiri unavyomuonyesha upendo kwa kujitoa yeye anaona kama hiyo si uhalisia wa maisha ya dunia sababu yeye hakukua hivyo akijaliwa au kupendwa.
Ameshazoea kupuuzwa, kutosikilizwa, kutumiwa au kupelekeshwa, kutosifiwa bali kusimangwa au kusemwa vibaya. Mtu kama huyu akija kukutana na mtu mwenye upendo wa kweli basi kitakachotokea ni maumivu na mateso ya hisia kwa huyu ambaye anapenda kweli na kujali huyu ambaye kakuzwa bila upendo.
Utakutana na binti mrembo sana au kijana mtanashati. Kumuona tu ukaanza kuumba fikra za namna utaishi nae kwa furaha na kumpenda na kuwa muaminifu kwake tu bila kumfanyia dhuluma au baya lolote la kihisia.
Ila bila kujua kumbe huyu mtu ni damaged goods ambaye toka makuzi ya utotoni alikuzwa na hiyo dosari inayomfanya kutokuwa mtimilifu na hautalijua au kutambua hilo hadi pale utakapothubutu kutaka kupendana nae na kumuonesha upendo wako kwake.
Kama unadhania au hauamini kuwa maisha ya mtu utotoni na makuzi yake hayaathiri namna atakavyoishi katika mahusiano yake then jua unakosea sana na u are in for a big surprise.
Therapy haitibu madhara ya utotoni ila ni njia nzuri ya kumsaidia mtu ambaye ana dosari asizoziona ila anatembea nazo na kuwaathiri wale anaokutana nao kuweza kujua kuwa tabia yake inajeruhi wengine na kuendeleza chain reaction ya maumivu na kuharibu nafsi zisizo na hatia ambazo zililenga kujali na kushare upendo.
Usijinyime nafasi ya kupendwa au kupenda sababu ya kubeba msalaba wa historia mbaya ya utoto na makuzi na kuumiza wengine. Kama wewe hauna hisia jail wenye nazo kwa kuheshimu hisia zao.
Nenda katafute msaada wa kitabibu na ushauri nasaha ili uweze kuishi na jamii vema bila kuwa chanzo cha maumivu kwa wengine na kuongeza watu wenye hisia mbaya juu ya upendo na mapenzi.
Asante.