Kama haujawahi kupitia machungu makali ya maisha usiwabeze na kuhukumu kirahisi wanaojitafuta kwa njia ambazo zinaoekana ni mythical.

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
1,609
2,755
Angalau hajakukaba kukupora au kufanya ujambazi wa unyama kupelekea mauti ya ndugu yako.

Hivi unadhani kuna mtu yuko tayari kupoteza nafasi ya kuhudimia familia bila ya kuwa omba omba na mfalme wa madeni.

Shida na tabu zinachaganya nyie sio hizo mlizonazo na unajua at some point unafuu una kuja, sio hizo, kuna zile ambazo mlango wa mbele na nyuma umefungwa sasa ni kunitegemea miujiza because everything is falling apart around you.

Yani unaamka asubuhi unajiona kama fala hivi kutojaribu chochote cha kubadirisha hali yako na ya familia yako.

Muda mwingine sio tabu za kujiletea ni basi tu majanga ya dunia. Kila kona unayopita hakuna msaada utafikiri umewekewa chapa ya kutosaidika na Mungu, mwanadamu wala shetani.

Ndio maana hamkosi kuwaona watu kwa hao wa kujiita manabii, waganga, masheikh wa visomo na wasafisha nyota.

Tusiwabeze, tuwaombee, hao ndio wateja wako wa kesho au wasaidizi wako wa kesho kama Mungu akiwafungulia.
 
Back
Top Bottom