Kama hatutaki tena EPA tuache ibaki hazina

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,978
3,888
Gazeti la Raia mwema la tarehe 16-22,2016 ukurasa wa12 lilikuwa na makala yenye kichwa cha thread hii. Mwandishi wa makala ile alijaribu kutaka kutuaminisha kuwa agizo la Rais Magufuli la kuamuru BOT kuwa msimamizi wa kulipa madeni ya nchi haukuwa sahihi eti tu kwasasbabu wataalam wakifaransa walishauri kuwa BOT isifanye kazi hiyo na ibakie na core functions zake kama ilivyoainishwa kwenye sheria iliyounda chombo hicho!! Tukumbuke kwamba BOT ndio banker of last resort wa serikali ; makusanyo yake yote yanakwenda kuhifadhiwa hapo na pia deni laTaifa ni lazima lisimamiwe na wao kwani malipo yote ni lazima yatokane la makusanyo yanayohifadhiwa na BOT. Itakuwa rahisi sana kama chombo kinachohifadhi mapato ndicho hicho kitakachokuwa kinajua kiasi gani kilipwe kwa wale wanaotudai. Wizi uliotokea pale BOT sio kwasababu ulipaji wa madeni haukuwa core function ya benki kuu bali ulikuwa ni wizi uliopangwa na wahusika wakuu wa utawala wa nchi na ndio maana hata wale washiriki wakuu wa EPA mpaka leo kesi zao zimezikwa na wala hazijasikilizwa!! Wizi ni wizi tu hata pale hazina iwapo watawala watabaliki wizi ufanyike utafanyika!! Hivyo kurudisha ulipaji wa madeni ya nje BOT ni sahii for ease of administration.

Katika makala hiyo hiyo mwandishi anajaribu kumtetea gavana wa BOT kuwa ni mtu mahili na kuwa huyo Ndullu ndiye aliyekuwa architect wa HIPC; ule mpango wa kusamehe madeni wa world bank wa kusamehe nchi masikini. Sijui taarifa hizi potofu huyu bwana alizipata wapi kwani ukweli ni kwamba HIPC ilikuwa ni initiative ya world bank na Ndullu wakati huo alikuwa anafanya kazi kule kama desk officer na hivyo si sahihi kuwa eye ndiye aliyebuni mpango ule!!

Huyu Ezekiel Kamwaga amejitahidi sana kumpamba huyu gavana wa BOT na hata kumuhusisha na kuukwamua uchumi wa Tanzania kwenye miaka ya 1980s eti alishirikiana na Samuel Wangwe kuunda mpango ulioukwamua uchumu wa nchi!! Ukweli ni kwamba hiyo miaka ya 1980s anayoizungumzia mwndishi world bank walikuja na mipango yao ya kiuchumi [ strucural adjustment programs] ambayo walikuwa wameitayarisha wao huko washington na kuileta hapa nchini itekelezwe kama conditionalities za kupewa mikopo. Sasa hawa wachumui wetu kama kawaida yao walikuwa wanatumiwa tu kwa kupewa vijisenti vya kufanya utafiti kidogo kujustify mipango ile ya world bank!! If anything hawa ndio waliodumaza uchumi wetu kwa kukubali kutumiwa kufaya tafiti uchwara zilizopelekea kuonesha kuwa strucural adjustment programs zilikuwa zinatufaa ; ukweli ni kwamba mipango ile ndio ilituharibia uchumi wetu na haikuwahi kuafanikiwa kokote duniani kama world bank wenyewe walivyokuja kukili baadae!!

Mwandishi wa hii makala kama kweli alikuwa na nia ya kumtetea Ndullu kwa Rais Magufuli juu ya utendaji wake angetueleza pia role ya huyu gavana na jinsi alivyoishauri serikali kuhusiana na sakata ya bond ya mabiilion ya shillingi iliyoihusisha benki ya stambic. Kama gavana alitakiwa atoe ushauri wa kitaalam kuhusu mkopo huo ili kulinda maslahi ya nchi ; je uhusika wake ulikuwaje? Kumbuka pesa cash kutoka Stambic bank kwa mamilioni ya $$$ yasingeweza kutolewa bila BOT kufahamu!!
Taarifa za kiuchumi zinaonesha kuwa kwa nchi kuchukua mkopo ule ,itakula hasara kubwa sana na gavana huyu akiwa hapo halo!!
 
Back
Top Bottom