Kama hajapevuka tegemea mahusiano machungu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,407
19,074
1598117373018.png


Habarini washkaji zangu, leo nimeona tuwekane sawa kwa ambao bado hawahapebuka kiakili kwenye ku handle mahusiano na wake zao

Sizungumzii kupevuka kimwii kama kuwa fiti kiafya, kutokuwa na ugonjwa, kuwa mrefu, n.k

Mwanaume yapasa awe kapevuka kiakili lasivyo basi binyi ataonekana wa muhimu tu kunako sita kwa sita.

Nashangaaga ugomvi umetokea mwanaume analeta za kindava eti anaenda kuweka status picha za mchepuko au rafiki wa mpenzi wake, kiukweli huyu yupo kundi la wa kiume sio mwanaume, kichwani dust bin

Linapotokea tatizo, mwanaume inabidi uwe ngangari kudhihiisha kweli hicho kichwa cha juu kimebarikiwa, sio kukimbia, kukwepa au kutokomea kusikojulikana pale tatizo linapotokea linapohitaji kutatuliwa, hiki ni kigezo tosha kwamba mwanaume huyu huenda kapevuka tu kichwa cha chini lakini ni mtupu kabisa kwenye kichwa kikuu.

inabidi uwe mwanaume mbele ya mpenzi wako, usije kumfanya mwenzio kuanza kusikiliza nyimbo za kina tony braxton "he wasnt a man enough for me"

Usiwe mtu wa kufoka au hata kutoa kipigo pale mwanamke wako anapokuibgiza ukweli mchungu masikioni, kwa staili hii ya kale hamtakuja kutatua kitu chochote zaidi ya kuzidi kushuka, mfano kuacha ulevi, kuacha kuendekeza marafiki, kuondoka bila kuacha pesa, n.k huyu ni ubavu wako.

Mwanamke kakuacha una miaka 26 kwajili ya kutopevuka mmerudiana kwenye 30 bado hali ile ile, meeachana hapo 30 mmerudiana 35 bado mambo yale yale, mara ya tatu huko 40 mambo yale yale, ndivyo hali ilivyo mwanaume usipotaka kubadilika utaongezeka umri tu
 
Back
Top Bottom