Kama Dunia inazunguka jua kwa Spidi kubwa kwanini vyombo vilivyo nje ya dunia haviachwi?



Katika hali kama hiyo anatokea mtu anadai kuwa hakuna Mungu!!??.

Niingie kwenye mada, ni kwamba huna haja ya kuhoji juu ya hizo satellites (artificial), wewe kwanza fikiria juu ya mwezi ambao ni natursl satellite ya dunia, kitu ambacho mwezi unavyo behave kwa dunia ndivyo hivyohivyo artificial satellites zinavyo behave, kimsingi binadamu tumeiga sayansi ya Mungu kuhusu dunia na mwezi.

Kinachofanya mwezi siku zote uwe kando ya dunia licha ya dunia kukimbia katika kasi kubwa kiasi hicho kuzunguka jua ndiyo nguvu hiyohiyo inayozishikilia artificial satellites katika orbit zake nayo ni nguvu ya uvutano katika ya dunia na hizo satellites na ndiyo sababu hizo satellites na mwezi siku zote nazo huizunguka dunia ili kufanya nguvu ya uvutano iwiane na nguvu ya centrifugal.

Kwanini haziachani ni kwamba satellites zote zimo kwenye closed system moja na dunia. Mfano wake ni kama mtu uwemo ndani ya gari inayokwenda speed kubwa na wewe unakuwa katika kipindi hicho ni sehemu ya hilo gari na kama hakuna mtikisiko na hauta angalia nje basi huwezi kutambua kabisa kwamba gari hiyo inakimbia kwa speed kubwa kiasi hicho, na hii ndiyo hali tuliyonayo sisi tuliokuwa juu ya uso wa dunia kamwe hatuwezi kutambua/ kuhisi kwamba dunia inasafiri kwa (circular speed) kubwa kiasi hicho kwa sababu tumo ndani ya closed system na sisi tumekuwa kama ni srhemu ya dunia.
 
Kwa elimu ya kawaida ya Fzikia ambayo hata hivyo sikuendelea nayo naweza nikachangia hivi, kwanza vyombo hivi huwa vinarushwa kwa speed kubwa ili viweze kutoka kwenye uso wa dunia na vikifika kule juu vinaachiwa na kuanza kuizungua dunia kama ufanyavyo mwezi ila inategemea wanachunguza nini.

Kama kinachochunguzwa kipo sehemu flani labda bahari ya pacific wanarusha hicho chombo usawa huo na kukipa speed sawa na ya dunia inapojizunguusha kwenye mhimili wake hivyo vinakuwa vinakwenda sambamba eneo moja kama vile magari mawili yatembee barabarani kwa speed moja alafu yapo sambamba (wenyewe wanaita parking orbit)

Wanasayansi wanachoangalia ni speed ya dunia kujizunguusha kwenye mhimili wake ambayo inatupa usiku na mchana na si speed ya dunia kulizunguuka jua hivyo kwa kuwa vile vyombo vipo kwenye anga la juu la dunia vyenyewe vinafanya kazi ya kuizunguuka dunia kama unavyofanya mwezi na dunia wakati inalizunguka jua inakwenda navyo kwa pamoja kama vile unavyojitwisha mzigo huku umebeba vitu vingine mabegani unatembea

Nimejibu kisekondarisekondari yaani zamani sana miaka ya 90 na kitu hivi kabla ya google (wataalamu watakuja kuweka record sawa)
 
Umejibu vema sana
 
Umejibu vema sana


Matokea ya kani ya uvutano na kani centrifugal ni sufuri, yaani the resultant force between gravitational force and the centrifugal force equals zero.and that is why the equilibrium is achieved.

Lakini sio kwamba kani ya uvutano ni sufuri.
 
Satellite nazo zinazunguka kufuata mzungo na kasi ya mzunguko wa dunia.

Sio kwamba zinakuwa zimetulia.

Ni kama wewe upo ubavuni mwa gari unakimbia speed sawa na gari huku unawasiliana na mtu alie kwenye gari, gari ikikata kona na wewe unakata huko huko mradi ubaki usawa wa dirisha lile la gari unaloongea na mtu.
 
Je na vyenyewe huwa vinakimbia sawa sawa na dunia au vipo at stationary position sababu ya zero gravity?.
Kama vitu stationery sasa kwanin haviachwi nyuma?
 
Umefafanua vizuri mkuu maana mie nilijitutumua kwa kukumbuka Physics ya A level kitambo sana (nimezunguuka lakini wewe umenyoosha maelezo)
 
Waliiona wapi ikiwa inazunguka?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
SAMAHANI mkuu, ivi hakuna MTU anaeishi pembezoni kabisa mwa Dunia , ili awe anachugulia pembeniii au haina madirisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…