Kama Dk. Edward Hoseah amefukuzwa, kwa nini Rashid Othman amebaki?

Status
Not open for further replies.

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Inafahamika mwaka 2013 Rais Kikwete alimuongezea miaka miwili zaidi ya utumishi, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS=Tanzania Intelligence and Security Service), Rashid Othman.

Matukio yaliyojitokeza baada ya Rais Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania ambapo amelazimika kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah yanaifanya pia nafasi ya Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa , Rashid Othman kuwa untenable.

Haiwezekani akasubiri mpaka muda alioongezewa umalizike wakati kuna madudu yanayohatarisha usalama wa taifa ambayo ameyaacha yakatokea na yanaendelea kutokea bila kuyadhibiti.

Ninatambua malengo makuu na madhumuni ya uwepo wa kitengo cha Usalama wa Taifa ni pamoja na:

(1) Ni kulinda maslahi ya taifa: kupambana na uhalifu mbalimbali; kulinda rasilimali zetu; kulinda na kutetea maslahi ya jamii; kukemea maovu katika jamii;

(2) Kuwatambua watu wanaoweza kuhatarisha usalama wa raia na jamii kwa ujumla kama vile majambazi; wauza na wala unga; wahaini; wabadhirifu wa mali za umma; mafisadi; watoa na wapokea rushwa; wahujumu uchumi; magaidi; na uhalifu wa kupangwa (mafia).

(3) Kuchunguza na kudadisi mafanikio ya kiuchumi na maendeleo kwa nchi za nje: kuleta habari ambazo zinaweza kuisaidia nchi yetu kupata manufaa ya kiuchumi, kisayansi, kiteknolojia na kimaendeleo kwa ujumla;

(4) Kuweza kuwachagua watu wanaoweza kuwa viongozi katika jamii: kuijulisha Serikali kuhusu mtu anayeonekana anaweza kutoa mchango mkubwa kwa jamii – kimawazo, kielimu, kimaarifa na hata kiuongozi.

Usalama wa Taifa kwa kupitia kodi za Watanzania imewaangusha sana Watanzania kwa kushindwa kusimamia Malengo na Madhumuni ya uwepo wake katika taifa letu.

Kama Dk. Edward Hoseah amekinywa kikombe cha uchafu wa bandari na rushwa nchini, kwa nini Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Rashid Othman asikinywe pia kikombe cha udhaifu wa Idara muhimu anayoisimamia?

Kama Rais Magufuli alichukua hatua ya kutengua uteuzi wa Dk. Edward Hoseah baada ya kujiridhisha kuwa utendaji kazi wa Takukuru chini ya Dk. Edward Hoseah hauwezi kuendana na kasi anayoitaka, kitu gani kinamfanya adhani utendaji wa Rashid Othman unaweza kwenda na kasi anayoitaka.

Wakati Rashid Othman akiwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa tumeshuhudia Utoroshwaji wanyama hai kwenda Qatar, Meli za nje ya nchi kuingia bila ruhusa ndani ya mipaka ya nchi na kuanza kuvua samaki na wanyama wa majini, Ndege kutoka nchi za nje kutua katika sehemu ya machimbo ya malighafi na kuondoka bila kuchunguzwa, Ufisadi, wimbi la mauaji ya Albino, kisiasa na kidini, etc.

Kwa jinsi mfumo wetu ulivyo, Kama TISS ni legelege hata TAKUKURU itakuwa legelege. Haiwezekani TISS ikawa imara halafu TAKUKURU ikawa legelege. Haiwezekani pia TAKUKURU ikawa imara wakati TISS ni legelege. Hizi taasisi zinategemeana katika utendaji.

Kwa nini fimbo iliyotumika kumchapia Dk. Edward Hoseah isitumike pia kwa Rashid Othman?
 
Last edited by a moderator:
Kwa mawazo yangu wakuu ni kwamba huenda TISS imefanya kazi zake vile inavyotakiwa na kazi za hizi organisation mbili ni concealed sana na kama zinategemeana kiutendaji basi itakuwa zote zimechunguzwa kiuhalali ndo maamuzi yakafanywa
 
nani alikuwa nani na ameshiriki vp kulirudisha nyuma taifa letu ktk kila nyanja za maendeleo nchini, Rais wetu anajua labda kuliko mtu yeyote ss hiv kilichofanyika kabla yake na hata ss,so tumpe muda!Hawezi kukurupuka akafanya kila kitu ndani ya siku moja,wiki moja au mwezi mmoja!
 
Mleta mada unatakiwa ufahamu majukumu ya PCCB na TISS,kazi ya TISS ni kukusanya taarifa kuzifikisha kwa wahusika.Tatizo la utawala uliopita wahusika wengi (decision makers) walikuwa hawachukui hatua yeyote wanapoletewa taarifa sababu kubwa ni wengi walikuwa wanahusika kwenye huo uovu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom