KAMA Chadema inatakiwa kufa ni nini kilipelekea 20% watake vyama VINGI na 80% wakatae na kushindwa?

Kapilipoint

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
381
343
Wakati Wa kuiua Chadema ulikuwa wakati Wa kupiga KURA KUKUBALI au kukata Mfumo Wa vyama VINGI au kimoja.Kama CCM ilishindwa kipindi Kile na 20% wakashinda hebu jiulize kwanini 20% washinde? CCM haina uwezo Wa kuua upinzani .
 
Ni bahati mbaya sana watanzania wengi hawakupata nafasi ya kusoma kwa undani ripoti ya tume ya jaji Francis Nyalali. Ukweli ni kwamba wananchi wengi walitaka mfumo wa Chama kimoja uendelee lakini kwa masharti mengi ikiwa ni pamoja na CCM kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Chama, mfumo mzima wa utawala wa nchi nk. Baada ya tathmini kufanywa ikaonekana kwamba mabadiliko hayo yasingeiacha CCM salama, ndio maana maoni ya wachache yakachukuliwa ili vyama vya upinzani ndio vifanye kazi hizo kama vile kuikosoa serikali nk. Na tangia kipindi hicho Kazi kubwa ya upinzani imebaki kuwa hiyo tu, sio kushika dola hata kama umma unaridhia.
 
Hizi nadharia za kuua vyama hazina mashiko! Kila chama kina haki ya kuishi. Tuwe na lugha nzuri jamani, CCM cdm, NCCR, CUF,TLP,ACT ZOOOTE ziishi milele,zina faida yake.
 
Hakuna mwanaCCM ambae anataka upinzani ufe...sidhani hata kama upinzani ukifa "natural death" CCM itaufufua tu ili wale 20%waendelee kutumbua matunda ya uhuru.
 
Back
Top Bottom