Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 1,781
- 9,904
Kongamano la kujadili Mafanikio na Changamoto za Kidemokrasia, Utawala wa Sheria na Ushiriki wa Umma, Dar es Salaam.
GEOPHREY PINDA (NAIBU WAZIRI KATIBA NA SHERIA): Tanzania hakuna Sheria mbovu, bali tuna Sheria zilizopitwa na wakati, zinazohitaji kufanyiwa marekebisho ili kuendana na wakati tuliopo
KAIZA BUBERWA: Miaka ya zamani Vyama vya siasa vilipoteza dira baada ya kuweka nguvu nyingi kwenye kutaka kuiondoa CCM madarakani. Wakati huo huo wanufaika wa CCM wakizuia kwa nguvu kutoondolewa Madarakani
JENERALI ULIMWENGU: Miaka mitano ya Magufuli ilijaa ukandamizaji uliopitiliza. Tulishuhudia utawala wa mtu mmoja ukibadili sheria na katiba. Hakujali Katiba ilisema nini. Uzuri alikua mkweli, alisema waziwazi hataki vyama vingi
Magufuli aliamua Wabunge watakao ingia Bungeni yeye mwenyewe, Takwimu zilikuwa ni haramu kama hazikutolewa na Serikali, Azaki zilishindwa kufanya kazi, katika awamu yake wajinga waliibuka kwa wingi na kujiona bora
Lazima tukubali kuwa bado tupo pabaya na tunahitaji kujitafakari tumefikaje hapa, tuangalie kama kuna mtu tuliyemuumiza katika kupotea kwetu. Tujue namna gani ya kuponya mioyo iliyoumia la si hivyo maridhiano hayatakuwa na tija
Rais Samia ameonyesha nia ya kuleta maridhiano. Nasi tuunge Mkono juhudi hizo lakini tunapaswa kufanya hivyo kwa umakinifu ili tusirudi tulipotoka
HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Wanasiasa wa Upinzani kukosa ushirikiano wenyewe kwa wenyewe ni chanzo kikuu cha kukosekana kwa Upinzani imara nchini
Udhaifu wetu mkubwa ni kukosa umoja
JOHN MNYIKA (CHADEMA): Kuingia kwenye mfumo wa Vyama vingi kulipaswa kutanguliwa na mfumo unaoruhusu uwepo wa vyama vingi.
Sasa ni miaka 30 ya Vyama vingi lakini bado hakuna katiba inayoruhusu mfumo wa vyama vingi nchini
Ukosefu wa Katiba Mpya ni Mzizi wa Matatizo. Vyama vya Siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya Hadhara pamoja na kuwa na Sheria zinaruhusu hili. Pamoja na mabadiliko ya kiutawala bado katazo hili linaendelea
HAMAD RASHID MOHAMED (ADC): Katiba sio mwarobaini bali utashi ndio unatakiwa, nilimwambia Mnyika 'hamuwezi kuandamana kama tulivyokuwa tunafanya sisi'
Nilikuwa tayari kukaa ndani kutetea wenzangu, lakini wao wakisikia kuna kukamatwa watakimbia watajificha uvunguni
FATMA KARUME: Uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa hovyo kuliko chaguzi zote zilizopita. Hakujawahi kutokea chaguzi yoyote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe kusiwe na kesi Mahakamani isipokua wa 2020, na hii ni kwa sababu watu hawana imani na Mahakama
Tumetengeneza Mhimili wa Mahakama usioweza kufanya kazi yake, Rais kuwa na Uwezo wa Kumteua na Kumuondoa Jaji Mkuu kunaondoa Uhuru wa Mahakama
Pia Mahakama kutegemea bajeti ya Serikali kufanya shughuli zake hudunisha uhuru wa Mahakama
JAJI MSTAAFU ROBERT MAKARAMBA: Wale ambao hawapaswi kutunga Sheria ndio wanatunga Sheria, ambao hawapaswi kutafsiri ndio wanatafsiri Sheria
Ndio maana mnasikia mtu anasema ‘Nitakuweka ndani’, yaani anakuwa Sheria, Mahakama na Polisi kitu ambacho tulipiga marufuku
Lazima kuwe na usawa, mfano neno gender lilikuwemo kwenye Katiba yetu likaondoshwa, Wanasiasa wanashindwa kutofautisha kati ya sex na gender
Sex ni biological, gender ni social concern, sasa hivi limebaki neno sex peke yake
Kudhibiti matumizi mabaya ya madaraka, hii inaanzia ngazi ya familia, kinachotoka kwenye familia ndicho kinachoakisi jamii yetu
Mfano Mkuu wa Wilaya au Mkoa anamuweka mtu ndani akiwa hajui umefanya kosa gani
Uvunjani na ukiukwaji wa Haki za Binadamu ngazi ya binafsi ndani ya jamii zetu ni mkubwa sana, hilo tuliangalie
Umoja wa Mataifa umeshaandaa Kanuni za kuongoza biashara katika kuheshimu Haki za Binadamu
ADO SHAIBU (ACT WAZALENDO): Vyama vya Siasa viwajibike kutengeneza mazingira bora ya Ushiriki wa Wanawake
Demokrasia isipoimairishwa, Siasa zikiendelea kuwa za piga ua, za baruti, za mabomu za kukimbizana itawafanya Wanawake washindwe kushiriki Kisiasa