Kama CCM ilishamiri, kwanini watendaji wake wametoswa?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Mabibi na mabwana kwa takwimu zilizopo na yale tuliyopata kuyasikia tokea kwa watendaji wake wakuu, CCM 2015 - 2021 ndicho kipindi chama hicho kilikuwa na mafanikio makubwa zaidi katika historia yake. Ilisemekana kuwa katika kipindi hicho, chama hiki kilishamiri vilivyo.

Ya kuwa katika kipindi hicho CCM:

1. Ilipata ushindi wa kishindo (takribani wa 100%) kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.
2. Ilipata ushindi wa kishindo (takribani wa 100%) kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
3. Leo hii bunge la JMT, takribani 100% ya wabunge wote ni wa CCM.
4. Imevuna wabunge na madiwani wengi zaidi waliopita bila ya kupingwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi hii.
5. Nk, nk.

Hivi, iweje basi pamoja na mafanikio makubwa haya (kama ni kweli), watendaji wake wakuu wakiwamo mh. Dr. Bashiru Kakurwa na bwana Humphrey Polepole watoswe kwenye nafasi zao kivile?

IMG_20210501_130541_775.jpg

Ina maana CCM wameshiba sasa kushinda?

Hii shindaji ya vishindo inayoambatana na sambaratishaji ya watendaji washindaji mubashara imekaa je?

Au ni kweli kuwa kila yang'aayo siyo dhahabu?

Ninawasilisha
 
Hivi adui hasa wa chadema ni Bashiru, Polepole na Magufuli au ccm?
 
Naomba kuuliza, hivi kuna tuzo za kuanzisha uzi zinazotolewa na Uongozi wa JF?

Naomba nikujibu swali lako hili duni kabisa kama ifuatavyo:

"JF is where we dare to speak out our mind openly."

Ile kusema tu kwa uwazi yale yanayokuwa mioyoni, tunayoyaona au yanayotukera bila ya kutishwa au kuzuiwa na mtu yeyote, ni malipo makubwa mno kuliko pesa.

Uhuru wetu, haki zetu, katiba yetu, maendeleo yetu .. na zetu zingine zote uzijuazo, hazina mbadala.

Hata hivyo wewe kama una uhitaji mkubwa mno wa malipo kwa mabandiko jf, basi fanya hima, nenda kajisajili kwa Johnthebaptist mratibu wa buku 7 wa zama za pole pole, kwa sharti moja tu la kujitoa ufahamu.

Sina uhakika walakini kama katika zama hizi za awamu ya sita ajira uchwara hizi za akina "jo" kama zingalipo.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Hao hawafai kabisa na itikadi zao zenye elementi za Kayafa!! Hata huu ubunge wa special seats hawastahili kabisa!!!

Polepole, Bashiri na wenzao wa awamu ya tano wamechangia sana kuirudisha nyuma mno nchi hii.

Pongezi nyingi kwa mama Samia kwa kuliona hilo na kuhakikisha japo hawa wawili wanapumzika kunakostahili kwa kuanzia.
 
Hao hawafai kabisa na itikadi zao zenye elementi za Kayafa!! Hata huu ubunge wa special seats hawastahili kabisa!!!

We mwanamume au mwanamke. Kigezo chako cha mtu kutofaa Ni kipi. Je ni Bosi Wake wewe au. Una wivu wa kipumbavu sana. Wewe unayefaa Tuambie umelifanyia nini Taifa au hata chumba chako cha kupanga. Kwa uropokaji huu ni dalili ya mtu maisha yamempiga kwa uzembe na ujinga Wake. Grow up und Acha kujudge wanaume usiowajua.
 
Heee! Povu lote hili ni la Omo tu au na cha Arusha kimo?

Mkuu mbona hata wewe umemjaji mwenzako.

Hayo ni mawazo yake. Au wewe ndiye bashiri, pole pole au labda ni bosi wa mtoa maoni?

Kwa wizi ulioasisiwa na mabwana wawili hawa kwenye chaguzi za nchi hii, wameitia hasara nchi hii kwa kiwango kikubwa mno.

Hawa jamaa walipaswa kuwa kizimbani katika jamii zilizo staarabika.

Mkuu mbona hivyo? Watutonesha vidonda vya machungu vya wasukuma wahedi wa imani hawa!

Hiiiiii bagosha!
 
We mwanamume au mwanamke. Kigezo chako cha mtu kutofaa Ni kipi. Je ni Bosi Wake wewe au. Una wivu wa kipumbavu sana. Wewe unayefaa Tuambie umelifanyia nini Taifa au hata chumba chako cha kupanga. Kwa uropokaji huu ni dalili ya mtu maisha yamempiga kwa uzembe na ujinga Wake. Grow up und Acha kujudge wanaume usiowajua.
😹😹 Mataga mtapata tabu sana awamu hii!! Inafika wakati mnafikiri kuwa mnaota ndoto ila ndio hali halisi, unafoka kutetea watu wasio na sifa poor idiot!!
 
Wengi wao bado hawajaamini kuwa awamu ya tano ndiyo imekwisha hiyo.

Imeondoka na mwendazake kwani hata kauli ya hapa kazi tu - kwishney!

Walipa buku 7 nao ndiyo hivyo tena. Mmoja baada ya mwingine, chali!

Hiiiiii bagosha!
 
Ulitaka apewe nani

"Wangepewa watu wenye kujua na kuthamimi maana na umuhimu wa haki ingependeza zaidi" - Dr. Shika.

Mola amjalie maisha marefu mama Samia ambaye hata kodi ya dhuluma tu, haitaki kwa vitendo.
 
Ulishawahi kuwa hata katibu kata? Mkuu sikudharau lakini kuongoza huwa ni issue sana.
 
Mabibi na mabwana kwa takwimu zilizopo na yale tuliyopata kuyasikia tokea kwa watendaji wake wakuu, CCM 2015 - 2021 ndicho kipindi chama hicho kilikuwa na mafanikio makubwa zaidi katika historia yake. Ilisemekana kuwa katika kipindi hicho, chama hiki kilishamiri vilivyo.

Ya kuwa katika kipindi hicho CCM:

1. Ilipata ushindi wa kishindo (takribani wa 100%) kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.
2. Ilipata ushindi wa kishindo (takribani wa 100%) kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
3. Leo hii bunge la JMT, takribani 100% ya wabunge wote ni wa CCM.
4. Imevuna wabunge na madiwani wengi zaidi waliopita bila ya kupingwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi hii.
5. Nk, nk.

Hivi, iweje basi pamoja na mafanikio makubwa haya (kama ni kweli), watendaji wake wakuu wakiwamo mh. Dr. Bashiru Kakurwa na bwana Humphrey Pole pole watoswe kwenye nafasi zao kivile?

View attachment 1769956

Ina maana CCM wameshiba sasa kushinda?

Hii shindaji ya vishindo inayoambatana na sambaratishaji ya watendaji washindaji mubashara imekaa je?

Au ni kweli kuwa kila yang'aayo siyo dhahabu?

Ninawasilisha
Tukadanganywa kuwa uchumi umepanda hadi 7-8% dah ila these stupid politicians wako na masiala
 
Majamaa yalikuwa maongo, majizi na majambazi ya kutupwa. Hayakuwa na mawazo mwendazake angeweza kuondoka bila kuaga.

Yametuharibia nchi. Si serikali za mitaa hadi bunge.

Si mbaya wakijua ipo siku watawajibika kwa matendo yao.
 
Dah wacha nigonge K-Vant Monday nawaibukia HELSB nao waache ujinga wao
 
Ulishawahi kuwa hata katibu kata? Mkuu sikudharau lakini kuongoza huwa ni issue sana.

Haiba ya mama kwamba anataka haki ina mbeba vilivyo. Kwa sasa maadui alio nao ni lile genge la wasukuma na wanachato wa imani peke yao. Kwa sasa bila ya genge hili mbona mama ana puyanga barabarani bila ulinzi?

Haiba ya haki haikutakiwa na mwendazake na genge hili la wasukuma koko wakiwamo bashiri, katelefoni, na wenzao.

Anayewajua hawa hawezi kuwa na maneno matamu sana kwao.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Tuliomba Sana na kufunga kwa Mungu awaibishe wote wale watakaovuruga uchaguzi mkuu hakika ametenda tumeuona ukuu wake.Mwanakondoo ameshinda.
Leo madalali wa kununua malaya wa siasa wamejaa fedheha
 
Back
Top Bottom