Kama bado hajapimwa, kwanini asipimwe?

Kwa hiyo cha msingi ni kujua kama kweli ameumia ( imesemwa Bungeni kuwa hakuumia) na kama ametumia, ameumiaje. Suala la ulevi ni sekondari. Kama amepiga mtu au kuua mtu navyo vinaweza kuthibitishwa.

Amandla...
Ulevi unasababisha mengi.

Unaweza ukasababisha mtu kuanguka na kuumia halafu akashindwa kujua kaumiaje na kuanza kudai kapigwa ilhali hajapigwa.

Ulevi unaleta impairment. Hali inayoweza kumfanya mtu aone maruerue. Mfano, mtu aliyelewa anaweza kukikimbia kivuli chake akidhani ni mtu mwingine anayetaka kumtendea ubaya.

Kwa hiyo, suala la ulevi si la upili kama unavyodai wewe. Ni suala la msingi kabisa, hususan katika kuutafuta ukweli.
 
kwani mlevi hawezi kushambuliwa?tena mimi nadhani akiwa kalewa ndio mda muafaka wa kumfanyia umafia.So hizi hoja zenu hazina mashiko.Anaweza kuwa alilewa na akashambuliwa pia.Msitufanye hatuwezi kufikiri.Mtu adondoke kwa ulevi halafu aitangazie dunia kapigwa,ili iweje?!acheni ujinga nyie lumumba boys.
 
La msingi ni kujua kama kweli aliumia mwenyewe au aliumizwa. Ikiwa ikionekana kuwa alijiumiza ndio sababu za kwa nini alisema uongo zinatafutwa. Hapo ndipo suala la impact ya ulevi linaingia. Je alisema uongo kuficha aibu ya kuwa alikuwa amelewa au ulevi ndio ulimfanya asahau. Ikithibitishwa kuwa aliumizwa na watu wengine, suala la ulevi linakuwa halina maana.

Amandla...
 
Kulewa ni ugonjwa?[emoji1]
Sasa hadi mtu wana mtransifer to Dar bado utasema ni zuga tu? Ujue hapo hili kundi linalotaka kuaminisha watu kua hajashambuliwa ndio wahusika wenyewe hao.... Kwani angekua ameanguka kwa kulewa si angesema tu nilianguka kwenye ngazi? Shida ingekua wapi?
 

Mkuu katika nchi zilizoendelea ukigonga gari au ukisadikiwa umelewa, basi polisi kitu cha kwanza watakachofanya ni kukuliza ni kwamba ulikunywa saa ngapi na kisha kukupima kwa Breathalyser.

Kisha kama umelewa kupita kiwango yaani tuseme kuanzia 75 kwenda juu basi unafungwa pingu na wapelekwa rumande ukalale ili uwe sober.

Hivyo kulewa ni primary na kuumia ni secondary.

Au weye waonaje?

Amandla.
 
kwani mlevi hawezi kushambuliwa?tena mimi nadhani akiwa kalewa ndio mda muafaka wa kumfanyia umafia.

Anaweza kushambuliwa. Lakini pia anaweza kujiumiza mwenyewe. Zaidi, anaweza kuongea maneno ya shombo kwa mtu na akasababisha kuumizwa.

So hizi hoja zenu hazina mashiko.Anaweza kuwa alilewa na akashambuliwa pia.Msitufanye hatuwezi kufikiri.Mtu adondoke kwa ulevi halafu aitangazie dunia kapigwa,ili iweje?!acheni ujinga nyie lumumba boys.

Kwa hiyo wewe na makamanda wenzio ndo mna hoja zenye mashiko?

Sijui kwa nini mnakuwa wakali hivi mkiambiwa bwana wenu alikuwa kalewa chakari.

Kwani kuna ubaya mtu akilewa?
 
Ushawahi kulewa wewe? Ushawahi kulewa chakari wewe?
 

Hapana. Ishu ya kwanza ni kama umegonga au unaendesha kiasi cha kuhatarisha maisha ya wengine. Hiyo ndio primary cause. Ili kupata sababu ya kwa nini unafanya hivyo ndio unapimwa ulevi, hiyo ni sekondari. Ukionekana kuwa kweli umekunywa kuliko inavyotakiwa, basi unalimwa DUI. Tukitumia mfano kama huo, kama ukidondoka kwenye tracks za subway, primary concern ni kuwa ulijirusha, ulisukumizwa au umeanguka kwa bahati mbaya. Hivyo hata kama utaonekana umelewa chakari, watataka kujua kwa nini ulianguka. Wataangalia kamera na kuwauliza walioshuhudia ili wajue kwa nini ulianguka. Wakiona kuwa haukusukumizwa ndio ulevi wako unapewa umuhimu wa kuwa pengine ulijirusha au uliteleza kutokana na pombe zako. Katika suala hili, hali ya ulevi wa KUB itakuwa na umuhimu pale tu ambapo inakapo onekana kuwa amesema uongo. Ikiwa ni kweli alishambuliwa na watu wasiojulikana, hilo suala la ulevi litakuwa halina mashiko. Labda kama itakuwa aliwachokoza kutokana na kulewa kwake.

Amandla...
 
Akishapimwa blood alcohol yake itasaidia nini? Kwa nini watu waiseme waangalie CCTV cameras?
 

Kwani yule aliyekatwa vidole amesemaje?
 
Medical Ripoti ya general, physical na pengine forensic examination inayotolewa na daktari ndo hua ina. Solve cases za nashambulio na vifo

Injuries za kudondoka Kwa ulevi na zile za kupigwa zipo distinct.

Kwa tukio hili alcohol level test ina nafasi pia kwani huend akawa amechanganyiwa madawa mengine na akalewa zaidi ya pombe aliokunywa kabla ya pengine matukio mengine.

Nadhani tufikirie Kwa laini ya medical report.
 

Hapana mkuu.

Siku hizi hata ukionekana wayumbayumba kuelekea kwenye gari yako basi walokuona wanaweza kupiga simu polisi na kusimamishwa na moja kwa moja ukapimwa kiwango cha pombe.

Mpaka sasa naona ushahidi wote umekwishavurugwa na majeruhi amepelekwa DSM.

Naona kamanda Muroto anapata wakti mgumu kuandaa taarifa za uchunguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…