Kama asingelikuwepo mtu huyu...!

Kama asingelikuwepo mtu huyu...!

Mi nawashauri wasijaribu kabisa. Maana wasomi wasio na ajira ni wengi kuliko watumishi walioajiriwa. Shauri zao..
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka 3 hakuna ongezek la mshahara na maslahi yenu yanazidi kukandamizwa.
 
kama asingekuwa mtu huyu vikao vya kifisadi vingekuwa vinafanyika hadi ikulu

kama asingekuwa mtu huyu , watanzania wangekuwa kama ukoo wa kambale kila mtu ana sharubu, hakuna baba wala nani

kama asingekuwa mtu huyu , maneneo kama unajua mimi nani, yangekuwa mengi sana mtaani.

kama asingekuwa mtu huyu, SGR isingejengwa, shirika la ndege lisingefufuliwa, mikataba ya madini isingerekebishwa, wakulima wangeendelea kunyanyasika, dili zingekuwa zinapigwa hadi na ikulu kabisa, watoto wa kitanzania wasingepata elimu bure

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
kama asingekuwa huyu , tanzania ingeendelea kuwa shamba la Bibi
Bora hata yangekuepo haya ila Mimi nikafanikiwa kumalzia nyumba yangu nikaacha kuishi nyumba za kupanga
 
Hapana. Anaesemwa hapa ni MTU HUYU!

MTU HUYU NI NANI?
Hapa ndipo penye kufikirisha!Lazima huyu mtu ajulikane maana ni Tatizo sugu ndani ya JF na Watz kwa ujumla wao! Ni vizuri MTU huyu ajulikane ili Watz wapenda HAKI,MAENDELEO,UCHUMI na ELIMU wakaungana kwa umoja wao ili KUMFYEKELEA MBALI....!!!Yumkini MTU huyu si katika wale WASIOJULIKANA!Naamini kwa wote walioathirika na na MTU huyu wanamjua kwa uzuri!Kifuatacho ni KUFYEKELEA MBALI MTU HUYU!
 
Sasa hivi si shamba la bibi tena,ni shamba la nyanya.
kama asingekuwa mtu huyu vikao vya kifisadi vingekuwa vinafanyika hadi ikulu

kama asingekuwa mtu huyu , watanzania wangekuwa kama ukoo wa kambale kila mtu ana sharubu, hakuna baba wala nani

kama asingekuwa mtu huyu , maneneo kama unajua mimi nani, yangekuwa mengi sana mtaani.

kama asingekuwa mtu huyu, SGR isingejengwa, shirika la ndege lisingefufuliwa, mikataba ya madini isingerekebishwa, wakulima wangeendelea kunyanyasika, dili zingekuwa zinapigwa hadi na ikulu kabisa, watoto wa kitanzania wasingepata elimu bure

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
kama asingekuwa huyu , tanzania ingeendelea kuwa shamba la Bibi
 
Tatizo lenu wabongo hamueleweki nini mnachotaka....wakati wa mzee wa kutabasamu (baba riz1)mlisema hafai.... ni bora tupate dikteta ainyooshe nchi ....sasa sala zenu zimesikika mmepewa dikteta mnahara hara hovyo ..mnataka kurudi kwenye kucheka cheka tena...
 
Tatizo lenu wabongo hamueleweki nini mnachotaka....wakati wa mzee wa kutabasamu (baba riz1)mlisema hafai.... ni bora tupate dikteta ainyooshe nchi ....sasa sala zenu zimesikika mmepewa dikteta mnahara hara hovyo ..mnataka kurudi kwenye kucheka cheka tena...


Kuinyoosha nchi sio kunyima watoto wa masikini ajira, sio kuacha kupandishia wafanyakazi mishahara. Zinduka huko ulipo wewe mtu
 
Habari wakuu.

Kwa miaka mitatu kama asingekuwa mtu huyu ungekuwa unakiwanja na ujenzi ungekuwa umeshaanza. Lakini si ajabu mpaka sasa huna hata dalili achilia mbali ndoto zako zilizokufa za kumiliki kiwanja hicho.

Kama asingekuwa mtu huyu muda huu ninapoandika ungekuwa upo ofisini unachapa kazi huenda umejiajiri au umeajiriwa. Lakini siajabu mpaka sasa huna ofisi hata ya kuuza karanga achilia mbali kuuza kashata za mia mia. Upo upo tuu na miaka inaenda na unaishi kama mgonjwa wa HIV.

Kama asingekuwa huyu mtu kwa miaka mitatu hii ungekuwa umepanda mshahara zaidi ya laki moja na nusu kulingana na ongezeko la mishahara kila mwaka. Lakini mpaka ninapozungumza muda huu ninauhakika mshahara wako umepungua zaidi ya laki moja na nusu na kama umejiajiri mapato yako kwa mwezi yamepungua kwa 20%.

Kama asingekuwa huyu mtu sasa hivi hapa ungekuwa umeoa au umeolewa lakini cha kushangaza hata yule mchumba uliyemfikiria utakuwa naye umeshaachana naye kwani maisha ni magumu. Mwanamke huenda usingezalia nyumbani kama asingekuwa mtu huyu kwani ungeshaolewa tena kwa harusi kubwa yenye zawadi kede kede. Usimchukie mchumba au mume wako aliyekuacha tatizo si yeye ni huyu mtu.

Kama asingekuwa huyu mtu ninapozungumza sasa hivi hapa usingefunga baadhi ya miradi yako kama si yote na pengine ungekuwa umeongeza miradi chungu mzima. Lakini mtu huyu ameua miradi yako alichobakiza ni roho yako tuu.

Huenda sasa hivi hapa ungekuwa umewajengea wazazi wako nyumba au kuifanyia marekebisho nyumba yao lakini sasa hivi unashindwa hata kuwatumia hata hela ya matumizi. Asingekuwepo mtu huyu ungestawi sana.

Asingekuwepo mtu huyu huenda sasa hivi watoto wako wangekuwa wanasomea shule nzuri ambazo ulipanga lakini amini usiamini kinachokufanya uwapeleke kwenye shule zile usizoridhishwa nazo ni huyu mtu. Na kama umempeleka imegeuka mzigo kwako na ada unatoa kwa kubembeleza na kutia huruma kwa waalimu wakuu.

Kama asingekuwa mtu huyu ninapozungumza hapa mafao yako ewe unayekaribia kustaafu ungekuwa unapewa kama yalivyo lakini picha limegeuka unapinga namna ya kuchukua haki yako.

Kama asingekuwa huyu mtu hapa, wewe usomaye Diploma ya fani fulani huenda ungekuwa unachukua shahada ya kwanza ya fani hiyo hiyo uipendayo lakini kwa vile marks zimeongezwa kimakusudi umeishia kusoma diploma. Mbaya zaidi huenda umeshindwa kusoma kabisa hata hako ka-diploma kako kisa huwezi kumudu gharama za malipo.

Kama asingekuwepo mtu huyu huenda leo hii tungekuwepo na kina Ben saanane, akina Mawazo na wengine wengi. Huenda Tundu Lisu angekuwa yupo Bungeni au jimboni akifanya yake. Huenda Akwilina angekuwa anafanya mahafali yake ya kuhitimu chuo huku ndugu zake na wapenzi wake wakifurahia. Lakini mtu huyu ndiye kasababisha mambo yote haya kutokea.

Kama asingelikuwa mtu huyu sasa hivi watu wangekuwa wanapigana vijembe majukwaani, kwenye mitandao ya kijamii bila woga wala uadui wowote na baada ya hapo hualikana wakicheka kwani lengo si uadui bali kujenga na kufanya maisha yaende. Lakini mtu huyu kafanya mambo haya kuwa ni chanzo cha matatizo ikibidi kifo.

Angalizo: mtu huyu anaweza kuwa mimi au wewe so kuwa makini kwenye Komenti.

JOKAJEUSI
Duh hapa mfalme jiwe anahusika...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom