Kama anakufanyia haya…! Dada unaachwa!

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,859
2,000
Mabadiliko katika mapenzi ni kitu cha kawaida sana, wakati mwingine mtu anahitaji muda wa peke yake, muda wa kutafakari mambo. Lakini kuna mambo mengine yakitokea unapaswa kuamka na kujua kua kuna kitu.

Mara nyingi wanawake ni vipofu katika mabadiliko, wanaachwa na kuonyeshwa dalili zote za kuachwa lakini bado wanang’angania hawaoni, zifuatazo ni dalili kumi kuwa mwanaume wako hakutaki tena kashakuchoka na anakaribia kukuacha.

(1) Anawasiliana, anatamani na kuongea kimahaba na wanawake wengine mbele yako.
Wala hajali upo, hajali kuwa anakuumiza, hajali kama unahisia, atawasilina na wanawake wengine, ataongea nao na kuongea maneno ya kukuumiza huku akikudharau mbele yao. Dada Unaachwa!

(2) Hakuchukulii siriasi tena;
Yaani unaweza kuongea kitu wala hajali, mnaahadi hatokei na wala haombi msamaha, kuna kitu cha muhimu kinachokuhusu wewe wala hajali na haumizi kichwa, ukiongea hakuchukulii siriasi atakebehi na kukashifu kila unachoongea. Dada Unaachwa!

(3) Hakupigii tena simu wala kujibu meseji zako;
Zamani ukibeep tu anapiga, lakini sasa wala hata hajali na ukipiga atakuambia nitakucheki ila ndiyo nitolee. Meseji ndiyo hajibu, yuko online au kwenye group, anacomment post ila wewe wala nikama vile haupo. Dada Unaachwa!

(4) Hakuonyeshi Tena Mahaba;
Mambo ya kushikana mikono kama zamani hakuna, hataki hata kuongozana na wewe na wala kukushika sehemu lizokua anakushika awali, anakukwepa kwepa na mbele ya marafiki anajifanya kama vile si mtu wake. Kama alikua anafanya hayo mambo awali na sasa hafanyi… Dada unaachwa!

(5) Hataki tena kufanya mapenzi na wewe;
Yaani imekua kama adhabu, mnaonana lakini wala hakutaki tena. Zamani alikua akikuona tu mziki wake unchanganyikiwa ila sasa ni kama unalazimisha. Hata kama ukiomba mechi ukifika hakuna rommnce wala kushikana kama analima vile kanyaga twende anakucha anaendelea na mambo yake. Dada Unaachwa!

(6) Anakuambia nataka kuwa peke yake “More Space”

Kuna mambo anafikiria msionana. Mkipanga anakuambia atakutafuta na wiki inaisha hakutafuti. Dada kama una mwezi hujaonana na mpenzi wako mko sehemu moja anakupiga chenga wewe ndiyo ushaachwa. Mwanaume anamkwepa mwanamke akiwa na mwingine anampa huduma zote na si vinginevyo hivyo kama anataka space Dada Unaachwa!

(7) Hataki kuongelea tena mambo ya mapenzi;
Zamani mlikua mkikaa kidogo anazungumzia maisha, watoto, sijui mapenzi yenu, mahusiano yenu na mahaba. Ila sasa wala hataki, ukiongelea hayo mambo anabadilisha mada, kukasirika na hata kuongea. Dada unaachwa!

(8) Hakusifii tena;

Kuna wale wanaume ambao hata hawana hayo mambo, ila kama alikua anajua umevaa nguo mpya, umesuka ana kusifia umefanya kitu kizuri anakusifia ila sasa hata ukipendeza vipi hasifii ni kama vile hata hakuoni na hata ukimuambia wala hajali anajifanya yuko bize na mambo yake. Dada Unaachwa!

(9) Hakuheshimu tena;
Zamani alikua akikuheshimu wewe kama mwanamke, anaheshimu kazi yako na ndugu zako, lakini sasa wala hajali, anakudharau anaweza kukudhalilisha mbele za watu na asijali, akakuona unadhalilika na wala hajali na kila wakati ni kutafuta neno hata moja la kukuudhi. Dada Unaachwa!

(10) Ameacha kuongelea mambo ya ndoa:

Ndiyo kuna ambao wala hawakua wakizungumzia hayo awali achana na hao. Ila kuna yule ambaye kila siku alikua ni namna akikuoa, namna sijui mkifanya hivi, mipango yake yote ilikua inakuhusiha na wewe.

Ila sasa daa hazungumzii tena mambo ya ndoa, yaani ukigusa hayo anakasirika na hata kukutukana. Au utasikia anasema mimi suala la ndoa sasa hivi bado, nataka nijinge kwanza, siwezi kuoa mpaka lini, sijui nataka mwanamke wa namna flani wakati upo na vitu kama hivyo. Dada ukiona hivyo jua Unaachwa.

Nimalizie kwa kusema kuwa hizi ni dalili tu kuwa huyu mtu kakuchoka na anataka kukuacha au kichwani kwake ashakuacha na ana mtu mwingine. Sasa kama anakufanyia yote haya wewe ushaachwa kabisa na ni wakati wakuwaza maisha mapya.

Lakini si wakati wa kukata tamaa, ni wakati wa kuanza kujipenda na kujifanyia mambo yote ambayo unaona yatakupafuraha. Kuacha kujipendekeza na kumsujudia na kuanza kujipenda wewe kwa kujifanyia mambo yanayokupa furaha.


C, E &P
Source: Ukurasa wa facebook wa Idd Makengo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom