KAMA ACACIA NI KAMPUNI HEWA , JE MAJADILIANO NI YA NINI ??

Hashim bin Faustin

Senior Member
Jan 30, 2017
177
250
Kwanza napenda kumpongeza Mh. Rais wetu kwa kuthubutu kulianzisha Dude hili la madini kwani tumeibiwa sana tena sana.
Lakini naomba kujibiwa maswali haya ili niweze kuamini na kumuamini Rais katika hili sakata kwa ujumla wake.

(1) kwa mujibu ya ripoti iliyo wasilishwa kampuni ya Acacia haijasajiliwa hapa Nchini hivyo inafanya biashara bila kuwa na vibali halali ! ! Kama kweli JE Rais wetu anataka mazungumzo ya nini na wezi hawa wahujumu uchumi ??? Kwa nini asitaifishe Mali zote za Acacia na kuwafukuza hawa wezi.

(2) JE Rais wetu anaposema BOT haina kumbukumbu za usafirishaji wa madini JE hili linawezekana vipi ?? Au kuna jambo anataka kulielezea kuhusu BOT na biashara ya madini mimi sija muelewa ?

(3) JE nani wa kulaumiwa katika sakata hili zima ?? CCM na Serikali yake kwa kuruhusu wizi huu kwa zaidi ya miaka 20 au Wapinzani ambao wamekuwa wakipiga kelele kulaani mikataba hii mibovu lakini timu nzima ya CCM iliwakebehi na kuwadharau. JE Leo hii CCM watajikosha vipi katika hili !?

Tunahitaji kuwa Wazalendo na kuungana pamoja katika vita hii lakini lazima ukweli usemwe ili kujenga msingi mpya na imara wa Taifa letu.

Mwisho KATIBA MPYA NI LAZIMA tuungane pamoja kudai KATIBA MPYA !!
 

comred

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
1,875
2,000
Pale speech yake 75% ilikua nikumwinda yule jamaa aliekua anawapa namna yakudeal na hawa wapigaji..
Vitisho na kebehii dhidi yake..Wale wanaoitwa majizi tutakutananao mezanii..
 

ZEE LA HEKIMA

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
1,298
2,000
Mhe Rais amefanya mambo makubwa sana, tena sana. Akienda pupa na kuanza kuwaadhibu, hawatalipa hayo matrilioni waliyotuibia. Kwa hivyo, kama umemsikia vizuri, amesema ACACIA watulipe kwanza (na ni hela ndefu-matrilioni). Tena alisema mikataba YOTE ifumuliwe iandikwe upya. Kumbukeni waliokuwa wanafanya ufisadi huu wa kutisha ni watu wa chama chake. Hapa alipo ameshasema WOTE waliohusika washughulikiwe bila kujali ni nani au nani. Nampa tano ( mara tano)
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,208
2,000
Ina maana B.O.T hawana kumbukumbu za Usafirishaji wa Madini??????


Kwanini hakuwatumbua?
Kwa mujibu wa ripoti ya leo ni kwamba HAWANA wala hawajawahi kufikiria kuwa nayo..wako busy na pamba na korosho tu.
 

Pierreeppah

JF-Expert Member
Feb 2, 2014
1,547
2,000
Jk na Ben waliitafuna hii nchi afu wakaiuza wakapiga dolari zao kibindoni, afu leo wanajifanya ni wakulima kumbe geresha tu. Jk akiwa rais aliwahi ulizwa na mwandishi moja kuwa kwann tz ni masikini? Akajibu hajui ni kwanini... Nadhani leo amepata hilo jibu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom