Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Awali ya yote naipongeza serikali kwa kuimarisha mfumo wa malipo ya kielektroniki serikalini.
Kinachokera ni pale unapoenda afisi ya serekali na kuambiwa kalipie benki: wanakulazimisha uende benki, ujaze fomu ya makaratasi na kulipia hapo benki ili upate 'slipu' ya kurudisha afisi ya serekali, ambako utakutana na urasimu mwingine kabla ya kupewa risiti.
Zama hizi za kutumia 'App' za simu ya kiganjani, au kutumia mfumo wa USSD kukamilisha malipo, utaratibu wa kulazimisha makaratasi unaonekana ni wa kizamani mno, unaofaa kubadilishwa. Afisi za umma zingeshauriwa zifungue mifumo ya kielektroniki ambayo inaongea na mifumo mingine, hususan ule wa malipo ya serikali.
Hii itapunguza kero nyingi na kuondoa urasimu usio na tija wala ulazima.