Kalenda ya masomo ya Shule za Awali, Msingi na Sekondari zabadilika kupisha Sensa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
WARAKA WA ELIMU NA.I WA MWAKA 2022 KALENDA YA MIHULA KWA SHULE ZA AWALI MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2022

Tafadhali rejea kichwa cha habari.
Kutokana na changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa Kalenda ya Mitaala ya Elimu kwa Shule za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari nchini mwaka 2022, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeona kuna umuhimu wa kufafanua na kutoa maelekezo shirikishi ili kuweza kwa pamoja kutatua changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa awali wa Kalenda husika

Katika muktadha huo, Kalenda iliyoanza kutumika kuanzia tarehe 17/01/2022 itatumika kama Mwongozo wa Jumla katika utekelezaji wa Mitaala ya Elimu kwa ngazi hizo za elimu nchini.

Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule ambao ndio wasimamizi wakuu wa utekelezaji wa Kalenda ya Mitaala ya Elimu katika shule mbalimbali wanatakiwa kutekeleza mitaala kwa kuzingatia hali halisi na mazingira husika katika maeneo yao ili kuongeza tija katika ufundishaji na ujifunzaji na kuleta mafanikio ya kitaaluma nchini.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Kamishna wa Elimu itaendelea kupokea maoni kutoka kwa wadau kwa nia ya kuboresha Kalenda ya utekelezaji wa Mitaala ya mwaka 2022.


Aidha, Kalenda ya Mihula ya Masomo kwa Shule za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari kwa mwaka 2022 itakuwa kama ifuatavyo:

MIHULA
KUFUNGUA MUHULA​
LIKIZO FIJPI​
KUFUNGA MUHULA​
IDADI YA
SIKIJ ZA​
MASOMO
KIJFUNGAKIJFUNGUA
Muhula I17/01/202213/04/202219/04/202228/07/2022
131​
Muhula II05/09/202230/09/20221 0/10/202208/12/2022
63​
Jumla a Siku za Masomo
194​
Tanbihi:

Siku za Masomo kwa mwaka ni 194.

Wanafunzi wote watapumzika kuanzia tarehe 29/07/2022 hadi 04/09/2022 kwa Muhula wa Kwanza ili kupisha Zoezi la Kitaifa la Sensa mwezi Agosti, 2022 na mwezi Disemba, 2022 watapumzika kwa Muhula wa Pili baada ya kufunga shule tarehe 08/12/2022.

Mashindano ya UMITASHUMTA yatafanyika tarehe 30/07/2022 hadi 08/08/2022, na UMISSETA yatafanyika tarehe 09/08/2022 hadi 19/08/2022.

Mashindano ya Michezo ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki (FEASSSA) yatafanyika tarehe 10/09/2022 hadi 24/09/2022.

Waraka huu unaanza kutumika tarehe 18 Februari, 2022.

Nawatakia utekelezaji mwema.

Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa

KAMISHNA WA ELIMU​

Nakala: Wathibiti Wakuu Ubora wa Shule Kanda na Wilaya, TANZANIA BARA.
 
Kwani lazima wawatumie walimu kama makarani! Mbona watu wapo kibao tu mtaani hizo posho zingewafaa bila kuvuruga/kupangua ratiba za shule.
 
Back
Top Bottom