KALENDA YA KIISLAM

KALENDA YA KIISLAM

NEGLIGIBLE

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Posts
354
Reaction score
92
Waungwana hongereni kwa kuhitimisha mfungo wa Ramadhan kwa wale walio swali Idd leo,na pia nawatakia maandalizi mema kwa wale watakaosheherekea Idd kesho.Sitarajii kujadili au kuibua mjadala wa kwa nini wengine wanaswali Idd leo na wengine kesho.Kwa kupitia mijadala na machapisho mbali mbali nimegundua kuwa hata kalenda za kiislam zinapaswa kuwa tofauti tofauti kwa kila nchi kutegemea na miandamo ya mwezi na uzingatiaji wa dhehebu aidha Shia au Sunni. Logic iko simple.Sote tunajua kuwa kalenda za kawaida za kimangaribi huwa ni" pre calender" kwa maana kuwa,unaweza kujua mwaka 2020 tarehe moja mwezi wa saba itakuwa siku ya jumatatu leo.Sababu ni kuwa inajulikana idadi ya siku ambayo kila mwezi unayo.Tofauti ni mwezi wa February tu,ambao una kati ya siku 28 au 29.Kalenda za Kiislam ni tofauti,kwani zenyewe ni "post calender",kwa maana kwamba kalenda huandikwa baada ya mwezi kuonekana. Swali langu ni kuwa ,tofauti na miezi ya Ramadhan na shawal na miezi mingine kama hii ambapo miandamo ya mwezi huwa ni matukio yanayofuatiliwa na public,sijawahi kusikia kuwa kuna taasisi ambayo inafuatilia miandamo ya mwezi kwa miezi mingine kama Shaban kwa ajili ya kuweka kumbukumbu kuonyesha,say Mwezi Shaban kwa mwaka fulani ulikuwa na siku kadhaaa.Ikumbukwe kuwa taasis hii inapaswa kuwa kila nchi kutegemea na miandamo ya mwezi.Natanguliza shukrani.
 
Ngoja waje mkuu mimi nawakubali sana hao watu katika kuelimishana
 
Back
Top Bottom