Kalamu ya Ezekiel Kamwaga inatumika vibaya!

Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,238
324
Katika Gazeti la Raia Mwema (Dec. 12-Dec. 18 2012) kuna makala "Kwa nini Zitto anafa kuwa rais 2015" mwandishi Ezekiel Kamwaga anayetambulishwa kama msomaji wa Gazeti hilo anapambanua kuwa sifa kuu ya rais anayehitajika kuitawala Tanzania kuanzia 2015 ni yule aliye "mahiri katika uandishi wa makala na machapisho mbalimbali".

Sifa nyingine ni yule anayefahamiana na viongozi maarufu (kwa mtazamo wake). Mwandishi anapambanua na kutabanaisha kuwa huyo mtu kwa hapa TZ ni Zitto pekee. Nimeshindwa kuelewa mwandishi anatumika, au ameamua kupotosha umma kwa makusudi, au aelewi anachokiandika.

Sina hakika kama sifa ya uandishi inatosha kumfanya mtu kuwa rais popote duniani, Ezekiel amesahau kwamba hata yeye ni mwandishi, na tunao wengine wengi tu wanaoandika majarida, makala, na vitabu na kushiriki midahalo mbalimbali yahusuyo mambo ya kiuchumi , kisiasa, na kijamii: kwanini yeye asifae wakati sifa hiyo anayo? kwanini wengine kama akina Dr. Rweitama, Dr. Mkumbo, watu kama Jenerali Ulimwengu na wengine wengi wasifae?? kufahamika na kuheshimiwa na viongozi ni swala la kawaida tu wapo wafanyabihashara, mishen towns na wengine wengi ambao wanafahamika na kuheshimika- sidhani kama hizi hoja zinaweza kumfanya mtu awe rais. Pengine kwa mtazamo wa Mwandishi hili linawezekana hapa TZ tu!

kimsingi waTanzania wanahitaji Rais mwenye sifa zaidi ya hizi zinazotajwa na Mwandishi. Ni kweli tunahitaji rais mwenye kujua matatizo yetu, lakini lazima pia awe na uchungu na utashi wa kuleta mabadiliko katika maisha ya waTanzania kwa ujumla, rais anayeeshimu mamlaka aliyonayo na kuitumia vizuri, rais mwenye uwezo wa kukemea mabaya na kusimamia kauli zake, rais mwenye uchungu na rasilimali za nchi. WaTanzania hawahitaji rais mbabaishaji, rais mshikaji na wenye sifa ambazo tumezichoka!

Naheshimu mawazo ya mwandishi, lakini pia waandishi wetu wasitumie kalamu zao vibaya kwa sababu tu wanafursa ya kupata majukua ya kuandikia, na tuwaogope sana waandishi ambao ni INSTRUMENTAL, wanaoweza kuchukua baadhi ya maneno katika sentensi ya mtu na kuifanya kuwa habari!

Mungu ibariki Tanzania!
 
kaandika pumba sijapata kuona..sijui katumwa na hata kama katumwa aliyemtuma kakosea maana kajenga hoja nyepesi sana za kumpamba zitto...hafai kuwa mpiga debe,..yani jamaa mambo ya buzwagi hajayagusia kabisa
eti zitto achaguliwe sababu kwenye uzinduzi wa filamu anaonekana na wasanii,.
sababu nyingine ni tamasha la leka tutigite(sijui kama nipo sawa na hiyo lugha),the guy is so poor in analysis,no wonder simba inachemsha kwenye mashindano
 
Mi nilidhan kaandika kuhusu LIVERPOOL au SIMBA!namkubal sana kwa hilo,Kumbe kaandika kuhusu si hasa,Ngoja nkajenge nchi
 
We mtu yupo chini ya rage sasa unategemea ana akili gani ya kuongea kitu ya maana
 
Du nimecheka hasa JF kuna mambo, mawazo ya mwandishi wa Raia Mwema Ezekiel Kamwaga yamegeuzwa kuwa ya Rage, Liverpool kweli ni kioja kusema mtu Mahiri wa machapisho kama ERIC SHI....... anafaa kuwa Rais nimekoma kuheshimu mawazo ya kutumwa.
 
Hivi kipindi kile akiwa mwanahalisi alikuwa anaandikiwa stori? Ametumia hoja dhaifu mno kumpamba Zitto!

Zitto ni kichwa lakini hawa wapambe dizaini ya nice 2 wa JF wanamdhalilisha kwa utetezi wa kipuuzi!

Huyu Kamwaga nafikiri Kubenea hakumpika vizuri maana hata Maulid Kitenge humtoa jasho kwa maswali mepesi tu!
 
Kanjanja usingi masaburi for mshiko at work. Kamwanga huenda ametumwa na Zitto kumpigia debe hasa baada ya wanasiasa kugundua kuwa pens for hire can made ends meet. Ni aibu kuwa mwandishi kutumika kama nepi wakati kuna mambo mengi muhimu yenye manufaa kwa umma kutumiwa na wasasi madaraka. Shame on you Kamwaga umemwanga mboga tutamwanga ugali. Kweli wewe ni kamwaga.
 
jamaa ndo kamaliza hapo, maana kaipamba kwa uongo wa kishabiki SSC, mpaka kasababisha mashabiki hasira zao wazimalizie kwa Kaseja, sasa ameanza kujipendekeza kwa ZZK, akijifanya anamfahamu vzr kwa kuwa alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati mojawapo ya simba iliyovunjwa na mpenda porojo mwenzie MH RAGE, komea hapohapo ZZK ni zaidi ya hizo porojo zako za kujipendekeza na usiharibu gazeti bora kwa porojo zako za kishabiki wa soka, kuwa kama kiongozi wa mpira utakuwa mwandishi bora wa siasa.
 
jamaa ndo kamaliza hapo, maana kaipamba kwa uongo wa kishabiki SSC, mpaka kasababisha mashabiki hasira zao wazimalizie kwa Kaseja, sasa ameanza kujipendekeza kwa ZZK, akijifanya anamfahamu vzr kwa kuwa alikuwa ni mmoja wa wajumbe wa kamati mojawapo ya simba iliyovunjwa na mpenda porojo mwenzie MH RAGE, komea hapohapo ZZK ni zaidi ya hizo porojo zako za kujipendekeza na usiharibu gazeti bora kwa porojo zako za kishabiki wa soka, kuwa kama kiongozi wa mpira utakuwa mwandishi bora wa siasa.
 
Ana ubongo wa samaki yule mbwana ezekiel ni kieherehere sijapata kuona,anajua kujikomba sana kwa watu wenye ela.
 
Jamani njaa zitatuua, huyu jamaa nae njaa inampeleka kubaya toka mwandishi anayeheshimika hadi KANJANJA mchumia tumbo, maana yeye mwenyewe ameanza kwa kukiri kuwa achokiandika kitamletea upinzani mkubwa, hiyo ni ushahidi tosha kuwa alijua anaandika pumba. Any way mwacheni bwana anajua ZITTO atampoza , kama kweli hakumkatia kwanza kabla hajaandika. SHAME ON YOU Kamwaga
 
Zitto anafaa kuwa rais kwa kuwa anaandika mara kwa mara kwenye magazeti na mitandao ya kijamii!.. KULAALEKi, hivi IKULU wanaenda kuandika kwenye magazeti na mitandao ya kijamii!!!.. "Zitto anafaa kuwa Rais kwakuwa anashabikia SIMBA na timu ya TAIFA!" - Kamwaga. ...Yaani Kwakuwa Rais Kikwete ni Yanga, kwa hiyo na SIMBA itoe rais?!!.. HIZI bangi zilizochanganywa na ulanzi wa Mlangali!..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom