Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Kwanza kakobe mwaka 2000 aliahidi kuaacha kuhubiri ikiwa mrema atashindwa Urais,huyu ni hero wa nani?
Kwanza kakobe mwaka 2000 aliahidi kuaacha kuhubiri ikiwa mrema atashindwa Urais,huyu ni hero wa nani?
Tukilinganisha kukubalika kwa viongozi wa dini na siasa tunakosea maana naamini dini mtu akiwa serious inzidi kwenye siasa, viongozi wa dini wanaweza wambia watu wao wajiue na wakajiua lakini kwenye siasa watauliza tunajiua kwanini. Mimi simwamini kakobe hata kidogo lakini namheshimu sana kwani ameshiria maisha ya waumini zaidi ya 300 ambao akiamua kuwateketeza anaweza bila kizuizi, then huyu huwezi mlinganisha na Mbowe ambaye hata akimwambia Zito wajiue kupinga tume ya uchaguzi Zito hawezi fanya.
Swala la dini halina elimu nenda kwa mwingira uone jinsi ambavyo watu wenye elimu zao wanavyopagaishwa na dini.
Inabidi msema kweli atuandikie viongozi wa upinzani ambao nia yake ni kuwinda ruzuku. teh teh teh
Natania, mkuu lakini implication ya kuwa na vyeti feki ni kama kuwa na upinzani feki.
Japo sikubaliana na msimamo wa kakobe kuhusu kupita umeme au kutopita katika eneo la kanisa lake lakini amenifurahisha kwamba anaweza kuwaongoza waumini wake wakaungana kudai wanachodai na wengi kama sio wote wako naye daima..wanamuamini na wanamfuata...
Ukilinganisha na vyama vyetu vya Upinzani (CUF, CHADEMA etc) wameshindwa kwa miaka mingi kuwaunganisha watanzania kudai vitu vya msingi kama katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, kushughulikia mafisadi etc..
My conclusion: Wapinzani hakuna leaders ambao wanaweza kupata watu mia tatu wanaowaamini kama kakobena waumini wake wakadai bila uwoga madai ya msingi????
- With all due respect mkuu wangu T, Kakobe ana-represent ishus ambazo at its core ni spiritual, as opposed na Upinzani ambao wana-represent ishus za politics ambazo basically ni ishus zinazohitaji physical demonstrations, sasa no matter how you try to reconcile hizi ishus mbili huwezi pata balanced au similar results. Kwa sababu ni ishus mbili tofauti, kumbuka Upinzani wa Tanzania ni mchanga sana kuulinganisha na imani za kidini ambazo zimekuwepo years and years sasa kina Kakobe wanaziendeleza tu,
- Sometimes we underestimates sana Wapinzani bila kujali kwamba wametufanyia taifa mengi sana mazuri, lakini tatizo ni sisi wananchi ambao we are at point of no return, yaani masikio ya kufa ambayo hayawezi kusikia dawa! hawa kina Chenge na the likes hawapelekwi bungeni na wapinzani!
- Huu ni wakati wa sisi wananchi kujiangalia na kutafakari kama kweli we deserve Upinzani! Maana the experience inaonyesha we deserve kina Chenges! Ni sisi wananchi ndio hasa part of the problem, labda siku moja tutaamka na kuwa part of the solution!
Respect.
FMEs!
wapinzani,? ninaowaaminia tu ni cuf-zanzibar, wapinzani bara hamna kitu, kujipa matumaini yasiyokuwepo, we angalia tu, Mbowe, Slaa ...... taja
Hakuna namna ambayo mtu mwenye akili timamu akasema kuna upinzani bara!
wanajitetea kwenye kivuli eti watu hawana elimu!, Tumaini, wakati Mkwawa anawapiga wajerumani alikuwa amesoma shule gani? wafuasi wake walikuwa wanasoma JF?
Simply I hate them!
Kakobe anawaumini mia tatu lakini madai yake (japo mimi naamini ame-over state issue yenyewe) lakini ameweza kuonyesha kwamba number is not the issue...
Hizo streotype kwamba watu hawana elimu ina maana wao hawana elimu kabisaa...
Kama una elimu unaweza kumfundisha mtu yeyote akakuelewa na kukuamini, hawaamini kwasababu wao wenyewe hawana elimu/maarifa ya kuwaambia wananchi wanachoelewa au wanachoamini!
Najiuliza hata wafuasi mia tatu jamani then...huko upinzani bado sana...
Wapinzani (esp chadema) waliongoza wananchi wa Tarime kupinga kodi ya maendeleo miaka kibao kabla serikali haijaamua kufuatilia suala la kodi ya maendeleo.
Wewe ulikuwa wapi kujua hili? ahhh nimekumbuka ulikokuwa .......
Watu wengine bana, kama hakuna upinzani kwa nini wewe mwenye akili timamu usianzishe upinzani wa kuaminika? Kukaa tu pembeni na kutegemea wengine wakufanyie kazi.
Hivi kodi ya maendeleo imefutwa lini?
Elimu ni msingi wa maendeleo ..... nilifundishwa hili nikiwa darasa la kwanza. Jipatie elimu mkuu kwenye mambo unayojihusisha nayo mara kwa mara (mf jukwaa la siasa la JF).
Mkuu acha kushambulia personal. teh teh teh
Nafikiri watu wenye akili timamu wao hawataki upinzani, wao wanataka maendeleo na maendeleo sio upinzani na upinzani si maendeleo.teh teh
sawa nimekubali naomba unielimishe kodi ya maendeleo ilifutwa lini? nitajitahidi kutilia maanani ushauri wako.
Kitu gani nilichosema hapo ni ushambulizi personal? Mtu akishasema kuwa watu wenye akili timamu hawaoni kama kuna upinzani Tanzania anamaanisha kuwa wale wanaoona kuwa kuna upinzani Tanzania hawana akili timamu.
Mimi nafikiri kuwa watu wenye akili timamu wanaelewa kuwa watu wenye wenye akili timamu wana uwezo na kila sababu ya kuchagua kama wanataka upinzani au la.
Mambo ya wewe kusema kuwa watu wenye akili timamu hawataki upinzani (hasa ukichukulia madhira yote yaliyoletwa na chama tawala Tanzania) ni zaidi ya fikara za kawaida.
Nilichomwambia Waberoya ni kitu simple, kama anaona upinzani ni hovyo, kwa nini asianzishe upinzani wake wenye nguvu ili watu waone mfano wa upinzani bora?