Kakobe: Tusichague mtu kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe: Tusichague mtu kwa rushwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kaa la Moto, Oct 19, 2010.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kakobe: Tusichague mtu kwa rushwa


  na Betty Kangonga


  [​IMG] ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zachary Kakobe, amesema vitendo vya utoaji rushwa visipodhibitiwa vinaweza kuharibu uchaguzi mkuu na kusababisha kupatikana kwa viongozi wasiofaa. Aidha, Kakobe aliwataka wananchi kutokubali kununulika kutokana na fedha kukosa thamani mbele ya utu wa mtu na kuonya kuwa zipo baadhi ya taasisi zikiwemo vyombo vya usalama, mawakala, maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamoja na wapigakura wanaweza kuingia katika mtego huo wa rushwa.
  Akizungumza katika ibada ya pili iliyofanyika jana makao makuu ya kanisa hilo Mwenge jijini Dar es Salaam, Kakobe alisema kupokea na kutoa rushwa ni dhambi hata katika maandiko matakatifu yameonya hivyo isipokemewa inaweza kuondoa baraka za Mungu ndani ya taifa.
  Kakobe ambaye alitumia saa moja kuzungumzia rushwa, alitoa mifano mbalimbali ya ubaya wa rushwa kwa kutumia kitabu kitakatifu cha Biblia.
  Kakobe alisema miaka ya nyuma kulikuwa na chama cha siasa ambacho ndani ya Katiba yake kulikuwa na ahadi za wanachama na kuwataka kukataa kupokea wala kutoa rushwa.
  Alisema kwamba ili kiongozi awe na utu ni lazima ajitenge na vitendo vya kutoa au kupokea rushwa na kuongeza kuwa kushamiri kwa rushwa kunapelekea wananchi wachache kupambwa na kutukuzwa na kundi lililopokea rushwa.
  “Rushwa hupoteza baraka si kwa Mungu hata kwa familia na kwa taifa zima, ukitengeneza makazi mazuri kwa mgongo wa rushwa dhamira yako itakusuta, ni sawa na kuweka fedha katika mfuko uliotoboka,” alisema.
  Akimtolea mfano Mwalimu Nyerere ambapo alisema alikuwa maskini jeuri ambaye alisimamia misingi ya haki na alikuwa tayari kwa lolote ambapo alikuwa radhi madini yasichimbwe yabaki ardhini kwa kuwa yasingeoza kama nyanya na kuongeza kuwa kama kuna mtu yeyote ambaye amepokea rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi anatakiwa kutubu.
   
 2. u

  urasa JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  msg sent to ccm!!
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  SAFI BABA ASKOFU
  Akimtolea mfano Mwalimu Nyerere ambapo alisema alikuwa maskini jeuri ambaye alisimamia misingi ya haki na alikuwa tayari kwa lolote ambapo alikuwa radhi madini yasichimbwe yabaki ardhini kwa kuwa yasingeoza kama nyanya na kuongeza kuwa kama kuna mtu yeyote ambaye amepokea rushwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi anatakiwa kutubu.
   
Loading...