Kakobe asalimu amri kwa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe asalimu amri kwa serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-bongotz, Mar 8, 2010.

 1. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Lile sakata la kupitisha umeme mbele ya kanisa la Mch. Kakobe hatimaye linaonekana limefikia tamati baada ya waumini waliokuwa wanalinda kanisa hilo usiku na mchana kwa siku zote toka sakata hili lilipoanza kutawanyika rasmi hivyo kupisha njia kwa TANESCO kuendelea na mradi wao, hiyo ndiyo taswira iliyopo kanisani hapo leo asubuhi kwani hakuna 'mlinzi' hata mmoja anayeonekana.,inasemekana hii ni kutokana na kauli ya serikali iliyotolewa na waziri husika jana.
   
 2. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #2
  Mar 8, 2010
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama madhara hakuna acha kazi ziendelee!!! Ila what I know huwezi kushindana na serikali
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 37,434
  Likes Received: 27,156
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo amewatesa waumini wake kwa miezi miwili bila sababu yoyote ya msingi.
   
 4. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #4
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,478
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Walikuwa wanakesha pale 24/7...sijui kazi walikuwa wanafanya saa ngapi?
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,927
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  walikuwa wanalishwa na bwana.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 8, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 14,433
  Likes Received: 1,130
  Trophy Points: 280
  tehe tehe tehee!
  kukesha pale sio issue, mbona huwa wanakesha humo ndani wakisali bana, au kwa vile huwa hatuwaoni.
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,233
  Likes Received: 322
  Trophy Points: 180
  People, u have to talk MATERIAL, na sio porojo!

  Ongeeni kilichotokea, na si kuripoti tu vitu pasi na kufanya rejea!

  Kwa waliokuwa makini kufuatilia hili suala, Kakobe amesimama Firm KABISA kutetea maslahi ya kanisa lake hadi dakika ya mwisho ambapo MUAFAKA umefikiwa kati yake na Waziri Ngeleja.

  Actually hii ndo SPIRIT ambyo Wabongo wote tunatakiwa kuwa nayo kila uchao.
  Kakobe ameweza kuwa na Msimamo wa juu kabisa na kuifanya serikali ifikirie mara ya pili, na hatimaye kutuma ujumbe wake ukiongozwa na waziri!...Hata hivyo, waliotazama mchakato huo siku hiyo, ni kwamba ilibidi waziri na Kakobe waingie mahali pa faragha ili kuongea kwa ukaribu kabisa, ndipo muafaka ulipatikana!

  Mikataba ya kishenzi inaingiwa na serikali, wabongo kimyaaa!
  Watu wanachukua vijisenti serikalini, wabongo kimyaa, mbaya zaidi wanawalaki watu hao wezi kama mashujaa!

  KAKOBE umeonyesha kwamba mambo haya yanawezekana, na serikali iko kwaajili ya kuwatumikia watu kwa njia ya kusikilizana nao, na si kuwaburuta!
  BIG-UP KAKOBE!
   
 8. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #8
  Mar 8, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,478
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Muafaka gani ulifikiwa wakati imethibitika Kakobe alitoa vipimo visivyo sahihi? Au alitaka kukutana tu na waziri kupiga nae stori?
   
Loading...