Nahitaji mwanasheria wa kunisaidia kuhusu uhamisho wa mke wangu.Suala la kwanza na muhimu kufahamu ni kwamba, maamuzi yaliyofanywa si ya Kairuki binafsi, maamuzi ni ya wizara kama taasisi ya serikali Kairuki akiwa kiongozi, hivyo yatosha kusema maamuzi ni ya serikali.
Kwa mantiki hiyona kisheria, pale ambapo maamuzi ya serikali ama chombo cha uma yaliyofanywa ama yanayotaka kufanywa yamekiuka ama yatakiuka matakwa ya sheria husika basi kesi yaweza funguliwa mahakama kuu ili kuamua uhalali wa maamuzi hayo. Mtoa maombi hayo anaweza iomba mahakama kuu kutengua maamuzi kama yamefanyika, kuweka zuio kama hayajafanyika, kutoa tamko ama vyote kutegemeana na maombi yake na taratibu za kisheria.
Mbali na hayo katiba na sheria nyingine zimeweka haki mbali mbali, pale ambapo zinakiukwa basi yule muathirika wa ukiukwaji huo ama mwenye maslahi kisheria anaweza fungua kesi ni haki yake.