Kaimu Viongozi wa Simba SC semeni ukweli kuhusu Niyonzima na Manula la sivyo nalipua bomu muaibike

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,848
109,552
Narudia tena kusema enyi Kaimu Viongozi wa Simba SC Salim Abdallah a.k.a try again na mwenzako ' Mtani ' wangu wa Kihaya Idi Kajuna a.k.a tajiri kijana nawapa muda wa Saa 24 au 48 tu zijazo waambieni ukweli wana Simba SC kuhusu Wachezaji Haruna Niyonzima na Aishi Manula kabla sijaja humu na taarifa ya ukweli kabisa kuhusu wao na jinsi mnavyotudanganya kila uchao.

Semeni ukweli ili muwe huru.

Nawasilisha.
 
Ukweli ni kua wanasubiri point 3 toka fifa kwanza kabla ya kufanya maamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tumechoka kufanywa Mangumbaru / Wajinga kila uchao juu ya Usajili hewa wa Niyonzima na Manula. Na hili bomu nililonalo ambalo wakifanya mzaha nitalilipua kweli waumbuke na waaibike nimelipata kutoka kwa wenzao hao hao waliopo katika Kamati za Utendaji na Usajili.

Kinachonipandisha hasira juu yao ni kwamba kwa muda wa wiki mbili kama siyo tatu nimekuwa nikiwananga / kuwatania sana wana Yanga sehemu mbalimbali kila ninapokutana nao kiasi kwamba hadi wengine wamekuwa wakiniona tu wananikimbia kwani wimbo wangu wa kuwaringishia umekuwa ni ujio wa Haruna Niyonzima na Aishi Manula sasa nawaza tu kama taarifa hii niliyoipata ni ya ukweli nitaficha wapi msura wangu huu?

Na hakuna Watu wanaojua kutania vibaya kama Wapenzi wa Yanga na kama kweli Niyonzima na Manula hawaji au hawajasajili Simba SC hakika nitawakoma!
 
Mtoa Mada unaonyesha viroba bado havijakutoka kichwani. Na nyinyi ndio mnaoharibu mpira WA Nchi hii Kwa ushabiki Wa kijinga jingaa. Kazi yenu kuzusha uongo wa kwenye kahawa kahawa tu. Suala la usajili Lina taratibu za kiutawala liwezekana viongozi watatuambia likishishindikana tutaambiwa. Na tuwe na hekima za kuelewa. Km wewe ni mkerekwetwa toa hela saidia usajili WA hao wachezaji uwatangaze mapema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumechoka kufanywa Mangumbaru / Wajinga kila uchao juu ya Usajili hewa wa Niyonzima na Manula. Na hili bomu nililonalo ambalo wakifanya mzaha nitalilipua kweli waumbuke na waaibike nimelipata kutoka kwa wenzao hao hao waliopo katika Kamati za Utendaji na Usajili.

Kinachonipandisha hasira juu yao ni kwamba kwa muda wa wiki mbili kama siyo tatu nimekuwa nikiwananga / kuwatania sana wana Yanga sehemu mbalimbali kila ninapokutana nao kiasi kwamba hadi wengine wamekuwa wakiniona tu wananikimbia kwani wimbo wangu wa kuwaringishia umekuwa ni ujio wa Haruna Niyonzima na Aishi Manula sasa nawaza tu kama taarifa hii niliyoipata ni ya ukweli nitaficha wapi msura wangu huu?

Na hakuna Watu wanaojua kutania vibaya kama Wapenzi wa Yanga na kama kweli Niyonzima na Manula hawaji au hawajasajili Simba SC hakika nitawakoma!
Tulia subiri simba day mchezo umeisha kwisha huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo simba day watacheza na timu gani? Wapo wachezaji wengi si lazima Niyo aje simba. Kama hajasaini ni heri tu maana wachezaji wa kibongo ni walewale.
 
Hata wasipokuja si bado usajili unaendelea, watasajili wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshasajili wachezaji 12 bado tu mnataka kusajili!!??.. Msimu uliopita mlisajili 13 hivi mnatatizo gani kichwani mwenu watani!!??... Misimu mitano Bila ubingwa haujiulizi tatizo nini.... Nyinyi kila msimu mnasajili timu nzima kuanzia kipa mpaka mshambuliaji.. Watakaa na kuelewana lini mpate mafanikio!!??... Agban mmefukuza katikati ya msimu mkaleta agyei.... Mna Manyika mmesajili tena makipa Watatu Mna makipa wa 5 kweli ndio uhitaji wa Simba kwa mapungufu ya msimu uliopita...!!??...
 
Back
Top Bottom