Kaimu Postamasta Mkuu, Macrice Mbodo: Lazima matokeo yaonekane kwa kila anayetumikia shirika hili

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Bw. Macrice Daniel Mbodo amewataka wajumbe wa Baraza la Majadiliano wa Shirika hilo nchini kuchukua kila fursa inayoonekana inaleta tija kwa Shirika kwa lengo la kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora na zinazoendana na mahitaji yao kulingana na mabadiliko ya Teknolojia

“Kila kiongozi aone umuhimu wa kuchukua kila fursa kama inavyotakiwa na kuwajibika kwa nafasi yake ili kuleta tija kwa Shirika na Taifa”. Alisema Mbodo

Aliyasema haya tarehe 13 Januari, 2022 wakati alipokuwa akifungua rasmi Mkutano wa Baraza la Majadiliano unaofanyika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) kampasi ya Bagamoyo huku ukihudhuriwa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na wawakilishi wa Menejimenti ya Shirika la Posta nchini

Aidha, Bw. Mbodo ametumia nafasi hiyo kuwafamisha wajumbe wa Baraza hilo kuwa Serikali Kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ikishirikiana na Wizara inayosimamia Sekta ya Posta; Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini imepokea mapendekezo ya mabadiliko ya muundo wa utendaji wa Shirika yenye lengo la kuboresha utendaji kazi wa Shirika la Posta Tanzania.

Ameendelea kueleza kuwa, muundo uliopo sasa umebana upatikanaji wa baadhi ya fusra kwa kuwa Idara na Kurugenzi zimewekewa majukumu mengi yanayosababisha kupunguza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi. Hivyo maboresho ya muundo huo yatamuwezesha kila mwananchi kunufaika na huduma zinazotolewa na Shirika hili nchini

“Muundo huu unaopendekezwa una maboresho machache ambayo yamefanywa ili kugawanya majukumu yatakayotuwezesha kuziona na kuzipata kwa urahisi fursa zilizopo sokoni kwani tukiendelea kuubana hatuwezi kuzipata fursa hizo”. Alisema Mbodo

Sambamba na hilo, Bw. Mbodo amewataka wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha wanaleta matokeo chanya yenye lengo la kukuza mapato ya Shirika kwa kuwajibika katika nafasi zao na kufanya kazi kwa weledi na kwa ufanisi.

“Ni lazima matokeo yaonekane kwa kila aliyepewa nafasi ya kutumika katika Shirika hili ahakikishe analeta matokeo”. Alisema Mbodo

Naye Mwenyekiti wa Baraza hilo Bwana Omari M. Dibibi amempongeza Kaimu Postamasta Mkuu kwa utendaji wake na amemshukuru kwa kukubali kufungua mkutano na kumuahidi kuendesha mkutano huo kwa weledi ili kuleta matokea chanya kwa Shirika kama ilivyokusudiwa.

Kwa upande wa Msemaji Mkuu wa Wafanyakazi Junus Ndaro alipongeza juhudi zilizofanyika na mikakati mizuri inayoonekana ya kuboresha utendaji wa Shirika ikiwa ni sehemu ya kuliboresha Shirika la Posta nchini kwa maslahi mapana ya taifa letu.
 
Back
Top Bottom