Kaimu Jaji Mkuu wa TZ, pole Prof.

CHADEMA ni demockrasia kwanza hayo mengine yatafuata baadae.

Ulitaka baada ya tume kutangaza matokeo ya uraisi huko Kenya CHADEMA wapinge matokeo ya nchi ambayo haiwahusu.

Ndio maana hata baada ya mahakama kutangaza kubatilisha ushindi wa Uhuru Kenyatta bado CHADEMA wanamkubali Uhuru kwa kuruhusu hayo yatokee kwa jinsi anavyoheshimu katiba na kuwajali raia wa Kenya.

Unadhani kwa nini raisi wako na mwenyekiti wa chama chako hayupo tayari kubadilisha hii katiba ya kikoloni ambayo inaipa tume ubabe ambao hata mahakama inashindwa kuiingilia utadhani na yenyewe ni muhumili unaojitegemea?

Uhuru Kenyata alikuwa na uwezo wa kuleta ubabe na kuamuru uchaguzi umeshapita na matokeo yameshatangazwa hivyo siasa mpaka 2022 lakini aliwapa kina Odinga haki yao ya kikatiba wakafungua kesi na mahakama kwa sababu zipo huru zimetoa maamuzi kulingana na katika wala si kwa amri toka juu.

Hiyo ndio sababu pekee CHADEMA wapo upande wa Uhuru na wala hawawezi kumkubali Kagame wala Museven wala Kabila wala Nkurunzinza.

Lumumba sometimes muamke vijana msiwe wachumia tumbo hata kwenye mambo yanahusu ustawi wa taifa letu.
 
Unaandika mengi sanaaaaa lakini point ni fupi na iko wazi kuwa Katiba ya Kenya inaruhusu Matokeo ya Urais kupingwa Mahakamani.
Short and clear.
 
Kakubali kufuata maagizo toka mamlaka nyingine aka mhimili na kuweka weredi kando

Sent using Jamii Forums mobile app
Vp kuhusu yule jamaa wa ule muhimili anayetokea kongwa. Huyo ndo usiseme, nadhani anayepaswa kulaumiwa ni huyo jamaa wa kongwa kwani anayo mamlaka kumpunguzia au kumwongezea na kumfunga speed governor yule Malaika asiye jaribiwa. Cha kushangaza ni cku ile ya ripoti ya makinikia alipokubali maagizo ya mkuu.
 
Tanzania maamuzi ya tume ya uchaguzi katika okeo ya Urais hayahojiwi mahakamani ndio ya mwisho. Hata wakusanye audio kama ushahidi Katiba yetu hairuhusu kamwe..kama yangekuwa yanahojiwa uchaguzi uliopita 2015 ungerudiwa maana kulikuwa na era katika takwimu. Refers final results
 
Sisi tunahitaji haki na demokrasia yakweli na si mbwembwe. Bado tunampomgeza kwa hatua alioichukua yakukubali maamuzi halali ya mahakama kwani kwa hapa kwetu Tz ingekuwa ni ndoto na hata wewe mwenyewe ni shahidi. Mahakama na Bunge letu tukufu limewekwa mfukoni na mtu mmoja na hakuna anaethubuti kwenda kinyume na mapenzi ya Bw Yule. Kama Mahakama iliweka zuio ktk bomoabomoa lkn serikali ikalipuuza na kuendelea na walichokusudia kwa raia wake wanyonge unategemea nn?
Mh Uhuru tutaendelea kumpongeza na hivi sasa yeye ndiye Baba wa Demokrasia Barani Afrika. Ila kwa ccm swala la haki, sheria na kuheshimu katiba ya nchi ni ndoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkumbushe Odinga kuwa ingekuwa ni huku kwa "frendo" wake, kwanza angekamatwa kwa kuwa na kituo cha kukusanya na kujumlisha matokeo ambayo ni kazi ya tume peke yake. Halafu asingekuwa na nafasi ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya kura za rais. Tatu wafuasi walioandamana wangepigwa na kukamatwa kwa kuharibu amani na maandamano na mikutano yake ingepigwa marufuku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena sasa hivi wanaiponda mahakama ya tanzania wakati kamanda wao Lissu akiwa na kesi kule ikatokea anashinda basi Huipongeza mahakama wakisema inatoa haki.
Mbona Mahakama yetu mnaigeuza kuwa ni sehemu ya hoja zenu kuu kisiasa? Hivi kama mfumo wakuziendesha mahakama zetu ungekuwa imara/huru ingekuwa inachezewa na wanasiasa kama inavyofanywa hivi sasa? Mahakama yetu hivi sasa hutegemea uendeshaji wake ktk kutoa maamuzi kwa maelekezo kutoka juu yaani kwa chama tawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…