Kaimu Jaji Mkuu wa TZ, pole Prof.

Ki Mun

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2014
Posts
3,442
Reaction score
4,389
Pole sana Prof. Ibrahim Juma kwa kukubali Mahakama yako ichezewe chezewe ...hivi ukikaa na Jaji Maranga wa Kenya unajisikiaje? Hivi kweli wajisikia na wewe ni Jaji Mkuu? Pole sana kwa kukubali kuchezewa, kwa kukubali kuwa mwanasesere, kwa kukubali kuwa mshangiliaji..

Najua huwezi kutenda haki kwa kesi za Magufuli dhidi ya raia wengine wanyonge wanaoonewa na Ma-DC, ma-RC wakiongozwa na boss wao...basi ungechukua tu hata hatua ya kujiuzulu usikubali kugeuzwa mwanasesere shehe...i mean profesa!
 
Du! Siyo kosa lake ni suala la mapungufu ya jamii yetu!
Na hasa wasomi!Kumbe wazungu wangeamua kusomesha watu wengi hii nchi isingepata kabisa Uhuru!Siwaamini wasomi wa nchi hii maana wengi wao wako brain washed kabisa na elimu yao na kuwafanya wawe wapumb.avu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa baada ya kuona mmeumbuka ndani ya muda mfupi mmeanza kusifia na kupongeza Mahakimu lakini wakati Aliyefungua kesi Raila Odinga mnamruka kama kinyesi sababu tu ni swahiba wa kitambo na JPM ambaye
Hapa wa kusifiwa siyo Odinga aliyepeleka kesi mahakamani bali ni mahakama iliyotoa hukumu!! Na wala hoja si nani anaungwa mkono na nani bali Mfumo wa Kenya unaruhusu mahakama kuwa huru kwenye mambo makubwa kama haya ya kutengua matokeo ya ushindi wa Rais.
 
Tena sasa hivi wanaiponda mahakama ya tanzania wakati kamanda wao Lissu akiwa na kesi kule ikatokea anashinda basi Huipongeza mahakama wakisema inatoa haki.
 
Mbona Lissu anaposhinda kesi dhidi ya Serikali mnatoka povu na kumsifia yaani mnasahau kusifia mahakama iliyotoa hukumu?
 
Odinga alijipanga vizuri,
Kukusanya formu za matokeo na kuwa na evidence documents siyo kazi ndogo.
Watanzania tatizo siyo tume,
Wasimamizi wengi wa uchaguzi vituoni,huwa hawako serious na mambo ya msingi ya nayo weza kuthibitika.
Nafikiri tukubari kiwango chetu cha Elimu ni tatizo la msingi.

Mahakama haiwezi kukataa ushahidi ulioshiba na vielelezo........
Acheni kuwasema sana majaji wetu kwani bado hatujawajaribu na kesi zenye vielelezo......
Mbona ubunge wanatengua?
 
Prof Juma kafanya kosa gani kiuhalisia?
Tumuogope mungu
Kukubali mahakama kukaliwa na executives
Hukumu za mahakama zinakiukwa yeye yupooo....
Kama watu wandharau court order...na mahakama iko kimya itadharaulika....ana uwezo wa kuagiza wanaodharau hukumu wakamatwe...suala la aliyewatuma watajua mbele....

Yote hii amekubali kuitwa kaimu mwaka sass ...ataitoa wapi heshima.
 
Kaimu jaji mkuu wa Tanzania hajielewi na hana maana. Tofauti yake na lipumba ni vipimo vya suruali tu.
 
Kwa kafulila ilikuwaje ?!!!
 
Lissu kushinda lazima watake wasitake, kwani huwa mahakamani huezi kufungwa kama hakuna kifungu kilichokiukwa na hiyo ndo janja ya lisuh, huwa anaongea apemdavyo ila hatoki nae ya key. Tanzania inasonga vizuri kwa sasa ila Kuna mapungufu ya kuyafanyia kazi, pendeni nchi wekeni siasa pembeni, msiwe kama hamjaaenda shule. Akikosea aambiwe na akipatia apongezwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena sasa hivi wanaiponda mahakama ya tanzania wakati kamanda wao Lissu akiwa na kesi kule ikatokea anashinda basi Huipongeza mahakama wakisema inatoa haki.

Kwa taarifa yako mahakama ya Tanzania haiko huru na hilo liko wazi kabisa. Inapotokea huyo Lissu akashinda kesi ni kwa uwezo wake na watu huwa hawapongezi haki kutendeka bali huwa wanashangaa haki kutendeka. Yaani mahakama kwao inapotenda haki huwa ni kitendo cha kushangaza na wala sio kawaida. Sio mara moja au 2 mahakama za Tanzania zinakwepa wajibu wake wa kutafsiri sheria na kusema ni jambo lenye joto la kisiasa hivyo likaamuliwe bungeni. Mifano ya mahakama kuchezewa na watawala ni mingi, mfano Lema kuwekwa ndani miezi minne wakati ni kosa lenye dhamana.
 

Sina chama ila sipendi uongo ukishamiri.

Jei-piem hakumpongeza UHURU? Naye unalisemea vipi?

Wakati mwingine msinywe gongo na sambusa, havisaidii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…