Kailima Ramadhan: Uchaguzi 2015 ulikuwa huru na wa haki, CHADEMA imeshindwa kihalali! Hakuna upendeleo kwa CCM, NEC ni Tume huru

Kailima Ramadhan: Uchaguzi 2015 ulikuwa huru na wa haki, CHADEMA imeshindwa kihalali! Hakuna upendeleo kwa CCM, NEC ni Tume huru

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
57,101
Reaction score
128,716
Wanabodi,

Baada ya figisu figusu za uchaguzi wa marudio wa madiwani, nimebahatika ya kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima, yaliyofanyika ofisini kwake jioni hii, kuhusu uchaguzi huo, katika kipindi cha Habari Zaidi ya Habari na PPR, ambacho kinarushwa kupitia Vituo 5 vya TV, TBC, ITV, STAR TV, Channel Ten, Azam TV, Clouds TV na kwenye Youtube.

Hizi ni Baadhi ya Dondoo za Mahojiano Hayo.
  • Zoezi la Uchaguzi limekwenda vizuri kwa asilimia 95%, hakukuwa na kasoro yoyote kubwa kuathiri uchaguzi huo, hivyo uchaguzi umekamilika na taarifa rasmi, itatolewa punde itakapokamilika.
  • Uchaguzi huo ulikuwa ni uchaguzi huru na wa haki, licha ya kutokea mapungufu na dosari ndogo ndogo ambazo haziathiri matokeo, hivyo matokeo ni matokeo halali, aliyeshinda ameshinda kihalali kwa haki, aliyeshindwa, pia ameshindwa kihalali kwa haki.
  • Hakuna hata chama kimoja, kilicholalamikia jambo lolote kuhusu uchaguzi huo, mpaka sasa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, haijapokea malalamiko yoyote, kutoka chama chochote, au mgombea yoyote kwa mujibu wa utaratibu wa kujaza fomu za malalamiko.
  • Hakuna chama kilichojitoa rasmi, ila kama ilivyo kushiriki uchaguzi ni hiyari, vivyo hivyo vyama viko huru kujitoa wakati wowote, lakini mpaka zoezi la uchaguzi linamalizika, hakuna chama kilichojitoa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kujitoa.
  • Mawakala wa vyama, wanapatikana kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni, mtu ambaye hajakidhi taratibu za uchaguzi, hawezi kuruhusiwa.
  • Ameelezea kuwa Tume yake ni Tume huru, inayoendesha chaguzi kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, hakuna chama chochote, kimewahi kulalamikia kipengele chochote cha uchaguzi kinachonyima haki, kitakachoifanya tume isiwe huru.
  • Amesisitiza Tume yake haijawahi kuingiliwa na chombo chochote, wala kupokea maagizo au maelekezo kutoka kwa yeyote.
  • Tume yake haijawahi kufanya upendeleo wowote kwa chama chochote, hata CCM nayo pia inailalamikia tume yake, hata uchaguzi wa Madiwani CCM Arusha wamelalamika.
  • Pia nimeuliza kuhusu Mkurugenzi, Mwenyekiti wa NEC na makamishna kuteuliwa na rais ambaye ni mwenyekiti wa chama kimoja, wataweza kutenda haki?, na kuuliza kwanini tume ya uchaguzi sio Shirikishi?, pia amelijibu.
My Take.
Its high time vyama tuanze kutake responsibilities kwa matokeo ya utendaji wa vyama vyetu kwenye chaguzi, kwa pale ambapo uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, tukubali kushindwa kihalali, asiyekubali kushindwa sio mshindani, badala ya kutafuta visingizio.

Kama hali ya uwezo wa ushindani kwa vyama vyetu vya upinzani nchini Tanzania, jee hali itakuwaje uchaguzi wa 2020?. Kama wapinzani hawatabadili strategies, za namna ya kushindana na CCM kwenye sanduku la kura, kuna hatari ya CCM, kuyarejesha majimbo yote ya upinzani mwaka 2020, hivyo Tanzania kuanza safari ya kuelekea kuwa ni nchi ya vyama vingi jina tuu, lakini ukweli tunaelekea kuwa nchi ya chama kimoja.

NB. Kipindi kikiwa tayari, nitakipandisha humu umsikilize mwenyewe.

Wasalaam.

Paskali
Update 1.
Pascal Mayalla,

..dont be cheap.

..interview yako ilihitaji kuwa na camera mbili.

..jingine ni kwamba hukuwa ukiuliza maswali ya ziada au follow up questions.

..haya ni makosa yanayofanywa na waandishi wengi wa habari hapa nchini. They never ask follow up questions.

..Je, kabla ya haya mahojiano ulijisomea kidogo kuhusu sheria za uchaguzi, mamlaka na majukumu ya tume ya uchaguzi?

..Zaidi ulipata wasaa wa kufanya utafiti kuhusu Mh.Kailima, utendaji wake, pamoja na maamuzi aliyopata kuyafanya ktk nafasi yake?

..MWISHO, uliharibu pale camera ilipoelekezwa kwako. Ulianza kuwananga CDM kuwa they are sore loosers. Halafu on the background Mh.Kailima alikuwa akitoa sauti ya kukubaliana na mtizamo wako kuhusu CDM.

..Athari za maoni yako zinaweza kukufanya uonekane wewe na Mh.Kailima lengo lenu lilikuwa ni ku-discredit madai ya CDM kwamba tume ya uchaguzi haitendi haki.
Mkuu Joka Kuu, kwanza asante sana, kwa sababu tangu bandiko hili limepanda hadi kufikia michango 537, mchango wako ndio the most deep, the most objective, the most professional and the best analysis of the contents, kwa sababu it is the content that matters, japo the clip ni just 10 min clip, ni watu wachache sana wameiangalia na kumsikiliza, but wewe you did. Thanks for this.

On Professionalism
Uko very right one one interviews program zinahitaji 3 cameras, ya interviewer, ya interviewee na ya wide ili kuyaonyesha maswali, majibu na setting.

Hata kama zimekosekana kamera 3, then kupitia camera moja ilibidi kuyauliza maswali on camera, na kuisert majibu, na kupiga cutaways. Hivyo ni kweli kabisa the interview was unprofessional. Nakubali makosa.

On Preparation na Research.
Kabla ya kufanya any good interview, inakubidi ufanye a little research and gether all the facts, ufanye a background check on your subject who is Kailima, elimu yake, ametokea wapi hadi kuibukia NEC, uwezo wake na utendaji wake, Jee ana uwezo, ana deliver etc. Hili halikufanyika, huu pia ni udhaifu on my part.

Interview Questions.
Ilibidi nitayarishe maswali ya msingi yanayoitwa leading questions at least matano kuhusu uchaguzi huo yakifuatiwa na follow-up questions.
Kila mwandishi analo eneo la strength na weaknesses zake, hivyo kiukweli kwa upande wangu, my strength ni kwenye interviewing haswa kwenye ku shoot maswali ya kushtukiza, lakini kwenye interview hii, hili pia halikufanyika, ni kama nimempa Kailima mteremko he just flow, hili ni kosa on my part ila ni kwa sababu, for a reason!.

The Reality And The Truth Kuhusu Hii Interview.
Kwanza naomba kukiri wazi hii interview, was impromptu, haikupangwa. Nimekutana na Kailima kwenye ngazi akielekea ofisini kwakwe, nikamuomba news interview ya just 5 minutes kuhusu uchaguzi wa marudio wa madiwani, akakubali. Hivyo there was no time for preparations, kutayarisha camera mbili, wala hakukuwa na maswali yoyote yaliyotayarishwa, maswali yote yalitoka kichwani, na majibu yote ya Kailima yalitoka kichwani.

Kwa Nini Nilimuuliza Maswali Rahisi Rahisi Bila Follow-up Questions?.
Kusema ukweli kupata chance ya impromptu interview na Mkurugenzi wa Uchaguzi Tanzania, was like a favour to me, not a right, hivyo kiukweli Kailima ameniheshimu sana kunikubalia interview ile hivyo hata maswali yangu ilikuwa lazima ya reciprocate favours niliyoipata, kwa kuto mbo bombard na maswali magumu, ili kumjengea mazingira mazuri ya future interviews kuelekea 2020. Ukiaminiwa, Jiaminishe, niliaminiwa na Kailima, ilinibidi tuu niwe mdogo to start with lakini kuna good things kuhusu Tume ya Uchaguzi vinakuja in future. Keep waiting, keep watching.

Paskali
 
Wewe Mayalla hebu acha ujinga!!! Hukuziona picha za majeruhi walioumizwa kwenye sehemu mbali mbali nchini!? Hukusikia yaliyojiri kuhusu wasimamizi wa upinzani kukamatwa au kutolewa ndani ya vituo ili kuruhusu wizi kufanyika?

Utumie akili japo kidogo badala ya kukurupuka ili kutafuta TEUZI.

MONDAY , 27TH NOV , 2017
NA MELLANIA JULIUS
Meya wa Manispaa ya Ubungo kupitia CHADEMA Jacob Boniface ambaye jana alishikiliwa na polisi, ameweka wazi sababu ambayo jana ilimsababishia kukamatwa na jeshi la Polisi na kulala ndani, huku uchaguzi ukiendelea.

case.jpg

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Meya Jacob amesema yeye alikuwa ni msimamizi wa vituo vya kupigia kura ambayo ipo kisheria, lakini baada ya muda alishangaa kuona polisi wanakuja kumkamata kwa tuhuma ambazo hazikuwa za kwlei.

“Nilikuwa nasimamia uchaguzi kama msimamizi wa uchaguzi wa chama changu, nikiwa kituoni nashangaa kuona nakuja kukamatwa na polisi, nilipofika kule wakaniambia kuwa wamepata taarifa kwamba nimejipanga kufanya vurugu na wenzangu, kitu ambacho sio kweli”, amesema Jacob Boniface.

Meya huyo ambaye ni miongoni mwa viongozi machachari wa CHADEMA amesema mpaka sasa hajajua hatma yake kama anapelekwa mahakamani au la, kwani aliachiwa huru majira ya saa saba usiku baada ya kulipa dhamana, huku uchaguzi ukiwa umeshakwisha.
 
Tume ya Uchaguzi imesema haijapokea barua rasmi ya malalamiko kutoka chama chochote kile..

Sasa Chadema badala ya kupeleka malalamiko NEC wanampelekea Da'Mange....upuuzi mtupu.
 
Mkuu BAK, uchaguzi ni process yenye sheria, taratibu na kanuni, zikiwemo taratibu za kuripoti malalamiko yoyote, kama hayo yote yametokea na hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, hadi uchaguzi unakamilika, hakuna yoyote aliyelalamika!, na hata kule kujitoa kwa Chadema, haikujitoa bali ilisusa tuu, kama ilivyo kanuni, unakuwa mgombea kwa kujaza fomu, na kujitoa ni kwa kutoa taarifa rasmi ya maandishi, na sio kuwaambia tuu waandishi wa habari. Tangazo lile ya kujitoa, lilipaswa kufuatiwa na kujaza fomu ya malalamiko, na kutoa taarifa rasmi ya kujitoa. Kama hakuna malalamiko yoyote registered, then tume iko right, no one complained!.

Paskali
 
Una ushahidi wa kuonyesha Chadema imepeleka malalamiko kwa Mange? Usijidhalilishe kiasi hicho mbele ya kadamnasi!!!

Hata kama Chadema haijapeleka malalamiko haiondoi ukweli kwamba uchaguzi haukuwa huru na wa haki.

Na wewe kwa ujuha wako unadhani hicho kitengo cha dikteta uchwara cha wizi wa kura kitatenda haki kwa Chadema?

Kama huna la maana la kuandika kaa kimya badala ya kufanya ubaradhuli kwenye issues za maana.

Tume ya Uchaguzi imesema haijapokea barua rasmi ya malalamiko rasmi kutoka chama chochote kile..

Sasa Chadema badala ya kupeleka malalamiko NEC wanampelekea Da'Mange....upuuzi mtupu.
 
Upinzani wa wakina mbowe upinzani uchwara kinachosikitisha ni vijana wetu wengine very smart wamejikuta wanashabikia kampuni ya mtu wakidhani ni chama cha siasa (asante Mungu wenye akiri wametambua mapema na kurudi ccm) kama demokrasia haipo Tanzania wao wameshidaje wakawa wabunge?
 
Pascal Mayalla ina maana vituko vyooote vile hukuviona duuuh bado tuna kazi kubwa ya kuelimisha watanzania maana ya demokrasia
Mkuu Mkwepa Kodi, kama sheria, taratibu na kanuni zinakutaka ujaze fomu ya malalamiko ili iende NEC, WEWE UNALALAMIKIA KWENYE MEDIA TUU BILA KUJAZA FOMU, nec WANAKUWA WAKO RIGHT, HAKUNA ALIYELALAMIKA.

Ila hili la umuhimu wa elimu kwa mpiga kura nimelizungumza, na mimi nitajitolea kutoa elimu hiyo bure.

Paskali
 
Pascal Mayalla ina maana vituko vyooote vile hukuviona duuuh bado tuna kazi kubwa ya kuelimisha watanzania maana ya demokrasia
Havikuathiri matokeo watu walipiga kura.wapiga kura mfano wako elfu 10 waliopiga lakini akatokea mhuni mumoja akadakwa akadundwa bara bara huyo mmoja ni asilimia ngapi ya wapiga kura?Ni tone tu kwenye bahari huwezi sema hiyo ni kasoro kubwa ni kitu kidogo mno.Aende kujiuguza na kupambana na hali yake
 
Narudia tena uchaguzi haukuwa huru na haki sehemu nyingi tu hata kama Chadema wangeamua kujitoa.

Kwenye uchaguzi haramu wa marudio Zanzibar CUF walijitoa kwenye uchaguzi ule. Hebu tuambie CUF walifaidika vipi kwa kuamua kujitoa?

Hata kama ni kutafuta TEUZI lakini si kwa kujitoa ufahamu kiasi hiki na kutetea wizi, dhuluma na udhalimu wa mchana kweupe.

Mkuu BAK, uchaguzi ni process yenye sheria, taratibu na kanuni, zikiwemo taratibu za kuripoti malalamiko yoyote, kama hayo yote yametokea na hakuna yoyote aliyelalamika rasmi, hadi uchaguzi unakamilika, hakuna yoyote aliyelalamika!, na hata kule kujitoa kwa Chadema, haikujitoa bali ilisusa tuu, kama ilivyo kanuni, unakuwa mgombea kwa kujaza fomu, na kujitoa ni kwa kutoa taarifa rasmi ya maandishi, na sio kuwaambia tuu waandishi wa habari. Tangazo lile ya kujitoa, lilipaswa kufuatiwa na kujaza fomu ya malalamiko, na kutoa taarifa rasmi ya kujitoa. Kama hakuna malalamiko yoyote registered, then tume iko right, no one complained!.

Paskali
 
Mkuu Mkwepa Kodi, kama sheria, taratibu na kanuni zinakutaka ujaze fomu ya malalamiko ili iende NEC, WEWE UNALALAMIKIA KWENYE MEDIA TUU BILA KUJAZA FOMU, nec WANAKUWA WAKO RIGHT, HAKUNA ALIYELALAMIKA.

Ila hili la umuhimu wa elimu kwa mpiga kura nimelizungumza, na mimi nitajitolea kutoa elimu hiyo bure.

Paskali
yule mkurugenzi ukimfuatilia juujuu utamuona kama hajali, ila mimi huwa namuona yuko makini sana kufuata taratibu.
Hata kama anamapungufu yake, ila ni mara chache sana utakuta analaumiwa kwa facts.
 
Back
Top Bottom