Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
ASILIMIA 70 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 20 hadi 49 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, imeelezwa.
Mwita alisema kuwa katika Wilaya ya Kahama, kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo inatisha hasa miongoni mwa vijana ambapo cha mwaka 2009, maambukizi yalikuwa asilimia 7.3, lakini sasa yamefikia asilimia 9.3 hali ambayo ni mbaya.
Kahama yaangamia kwa Ukimwi
Imeandikwa na Raymond Mihayo, Kahama; Tarehe: 22nd April 2011 @ 23:35 Imesomwa na watu: 102; Jumla ya maoni: 0
ASILIMIA 70 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 20 hadi 49 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wilayani Kahama, mkoani Shinyanga wameambukizwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, imeelezwa.
Hayo yamesemwa na Ofisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kahama, Morgan Mwita katika taarifa ya hali ya Ukimwi katika Wilaya ya Kahama mbele ya wadau wa mapambano dhidi ya ugonjwa huo wakiwemo watendaji wa kata na viongozi wa dini.
Mwita alisema kuwa katika Wilaya ya Kahama, kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo inatisha hasa miongoni mwa vijana ambapo cha mwaka 2009, maambukizi yalikuwa asilimia 7.3, lakini sasa yamefikia asilimia 9.3 hali ambayo ni mbaya.
Alisema wakati wilaya hiyo ina wakazi 815,175, wakazi 85,342 walijitokeza kupima Ukimwi hadi kufikia Desemba mwaka 2010, na 7,913 waligundulika wameambukizwa virusi vya Ukimwi.
Mwita alisema kutoka na maambukizi ya ugonjwa huo kuwa makubwa, changamoto wanayoipata wao kama Wilaya ya Kahama ni pamoja na kuendelea kuelimisha jamii kuacha kabisa unyanyapaa na ubaguzi kwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
Alisema changamoto nyingine ni pamoja na kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo hasa katika maeneo ya vijijini ambako kuna idadi kubwa ya watu ambao hawajapa elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huo hatari.
Hata hivyo ofisa huyo aliyataka mashirika mbalimbali kuongeza jitihada za kutafuta fedha za kuhudumia watoto walio katika mazingira magumu na hatarishi hasa katika upande wa lishe, elimu, ujasiriamali na afya.
Why this age group: 35-39? Pesa? Ushawishi? Ni nini hasa?
.
.
.
Prime Minister Mizengo Pinda released the results from a recent survey carried out by National Bureau of Statistics with assistance from USAID. The survey interviewed and took blood samples from more than 9,000 women aged 15-49 and close to 7,000 men aged 15-49 in all 26 regions of Tanzania. The results indicated a 4.7% HIV prevalence rate among men and a 6.8% rate among women. This is a slight improvement over the 2003-04 survey which found rates of 6.3% and 7.7% respectively.
Iringa recorded the highest rate of 14.7% (previously 13.4%) followed by Dar es Salaam at 8.9% (previously 10.9%), Mbeya at 7.9% (previously 13.5%) and Shinyanga at 7.6% (previously 6.5%). Zanzibar had the lowest prevalence rate at 0.6%. Age-wise, the highest prevalence was among the 35-39 age group (10%).
The survey also collected information on knowledge of HIV, attitudes and behavourial aspects. Over 98% of respondants had heard about HIV/AIDS. 68.6% of women and 76.3% of men knew that condoms can reduce the risk of contracting HIV, while 82% and 86.6% knew that limiting sex to one uninfected partner who has no other partners would reduce the risk. 85% and 89% where aware that abstaining from sexual intercourse is another recognized prevention method.
Source: Tanzanian Affairs » AIDS/HIV & MALARIA STATISTICS
tatizo siyo madereva tu....hakuna sehemu ambao nilisha wahi kufika ambako ngono inafanyika hovyo hovyo kama mbuguni, utakuta vitoto vya darasa la tano vina mimba hapoa kuna maderva gani...mji wa kahama ni kambi kubwa ya madereva wa magari makubwa wenye masafa marefu. Uchunguzi wangu unaonyesha mikoa ya shinyanga na tabora imeadhiriwa zaidi katika miji ya kahama na nzega. Nyumba za wageni zimejaa madereva wa magari makubwa yaendayo pande za rwanda na burundi.
Iringa nako hali kama hiyo kwani madereva baada ya kulazimisha malori kupanda mlima kitonga wanajipumzisha iringa, na wengine kabla ya kujiandaa kuteremsha mlima kitonga wanajipumzisha iringa kwanza.
waambukizaji wakubwa ni madereva na dada zetu victims wanaotafuta cho chote toka kwa madereva kujikimu kimaisha. Na hawa dada zetu wanawaume au marafiki wengine wanakopandikiza walivyovuna kwa madereva.
jamani ukimwi unakwepeka kwa wanaojiamini na kuamua kuaminiana baada ya kujihakikishia usalama wao
Kumpata dada ambaye bikra siku hizi ni chanda cha dhahabu, hali kadhalika kumpata kaka asiyekuwa na uzoefu wa mahusiano ya mapenzi ni ndogo. ...
tatizo siyo madereva tu....hakuna sehemu ambao nilisha wahi kufika ambako ngono inafanyika hovyo hovyo kama mbuguni, utakuta vitoto vya darasa la tano vina mimba hapoa kuna maderva gani...
ina maana wengi wa kina dada wanazaliwa bila hiyo na wengi wa kina kaka wanapata uzoefu kabla hawajazaliwa?
Boyfriend & Girlfriend mahusiano yanaanza kabla hawajajua ulimwengu ukoje na bado wananukia maziwa ya utotoni, je hayo yatawafikisha kunako ndoa au ni mfumo wa kuiga tamaduni nyingine ambazo wazazi wetu hawakuzoea?
Eti siku hizi lazima watu wafanye majaribio kwanza, na wakijaribiana na kuchokana nini kitaendelea? Katika kujaribiana na kuzoeana hatima yake ni kutwishana mimba baadaye kuchokana hatima yake kila mmoja na njia yake huku hakuna uhakika kama walikuwa makini kujiangalia kiafya. Na mapokea kwa waafrika wengi msichana kisha zaa soko la kuolewa huwa adimu kidogo, bora ajenge njia ya kujitegemea mwenyewe.
Ukimwi unakwepeka kwa wanaojiamini na kuamua kuaminiana baada ya kujihakikishia usalama wao