ZITTO azidi kuwaka, asisitiza Kagoda mali ya CCM
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, bado anasisitiza kuwa Kampuni ya Kagoda ni mali ya chama tawala CCM.
* Adai fedha ilizochotwa EPA zilitumika uchaguzi mkuu 2005
Na Kizitto Noya
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesisitiza kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakiwezi kukataa uhusiano wake na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited iliyochota zaidi ya Sh40 bilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania.
Zitto aliyekuwa anajibu mapigo ya CCM iliyomshutumu juzi kwa kuipaka matope kwa kuihusisha na Kagoda, alisisitiza kuwa CCM haiwezi kujivua gamba la Kagoda kwa kuwa ndiyo inayomiliki kampuni hiyo, ikiwa miongoni mwa kampuni 22 zilizochota jumla ya Sh133 bilioni katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
"CCM ndiyo inayomiliki Kagoda na Kagoda ni ya CCM. Fedha za Kagoda ndizo zilizotumika kwenye kampeni za CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Huu ndio ukweli," alilisitiza Zitto.
Kwa mujibu wa Kabwe, endapo CCM inataka kutakata inatakiwa kumruhusu Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua hesabu zake za mwaka 2004/2005 na ieleze wapi ilipata fedha za uchaguzi mkuu mwaka 2005 uliomwingiza Rais Jakaya Kikwete madarakani.
....
........
Chiligati aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa chama hicho hakina uhusiano wa aina yoyote na kampuni hiyo na kwamba hata kama kuna mwanachama anayehusika, ni suala lake binafsi na sio kwa mwavuli wa chama.
Tangu kuibuliwa kwa tuhuma hizo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiihusisha CCM na Kampuni ya Kagoda inayodaiwa kuchota Sh40 bilioni kwenye akaunti hiyo na miongoni mwa watuhumiwa wa EPA waliokwishafikishwa mahakamani, yumo Mweka Hazina wa CCM Mkoa wa Kigoma, Shaaban Maranda
Juzi Chiligati ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM alitoa tamko la kukisafisha chama hicho na kashfa hiyo akisema haina uhusiano wowote na wala hawaitambui kampuni ya Kagoda.
"Vita dhidi ya ufisadi na rushwa nyingine ielekezwe kwa mtu mmoja mmoja na siyo CCM kwani haiwezekani wana-CCM wote wakaenda benki kuiba fedha hizo pamoja," alisema Chiligati na kuongeza: "kampuni ya Kagoda haina uhusiano wa aina yoyote na CCM na wala CCM hatuijui".
Alisema kwa muda mrefu viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakifanya juhudi za makusudi kutaka kuihusisha kampuni hiyo na CCM na kutoa mfano kwamba, hivi karibuni Kabwe alinukuliwa akisema kwamba kuisha kwa suala la EPA kwa kiwango kikubwa kunategemea Kagoda itakavyochukuliwa hatua za kisheria.
Alisema CCM ni chama chenye kuheshimika, makini na safi, hivyo vijana wadogo iliowalea kuanza kukipaka matope ni kutafuta laana na njama zao hazitafanikiwa.
Hesima mbele mkuu.
Naomba tupanue kidogo huu mjadala kuhuisiana na hizi fedha zinazodaiwa kupelekwa CCM kwa ajili ya kampeni.
Kwa mtazamo wangu, hata kama aliyepeleka alikuwa individual, alifanya hivyo kwa lengo la kusaidia kitu fulani-na kitu hicho (kulingana na wakati) ilikuwa ni uchaguzi. Tunajua kuwa ili mtu achaguliwe, anahitaji kuwa nomibnated na chama. nadhani hapo ndipo CCM inapounganika na fedha hizo kwa sababu zililetwa na individual kwa ajili ya mgombea/wagombea wa CCM.
Au, unataka kutueleza kuwa fedha hizo zilizoingizwa na individual zilitumika individually? yaani zilipelekwa ofisi za Mindu badala ya Lumumba?
Si kweli.
Chama kinatakiwa kimpelekee Msajiri ripoti ya akaunti zake ambazo zimeshafanyiwa ukaguzi na chama chenyewe tayari. Na hapo ndio kuna tatizo.
Mkuu sijakuelewa hata chembe.
Fedha inayoongezwa individually kusaidia chama haimo kwenye hesabu ya fedha ya chama. Je hii ina maana kwamba CCM ikiongezewa fedha individually, let say 40,000,000,000.00 kutoka kampuni ya Kakiti Agricultural Co, fedha hiyo has nothing to do with CCM??!!!??!!??
Una maana fedha zinazofanyiwa auditing ni zile zitolewazo toka serikalini tu?au namna gani!!?
If that has nothing to do with with CCM as a party, tutajua vipi chama kinapewa fedha na KGB ,Maharamia wa Somalia, au kinanunuliwa kwa bei chee na wanachama wake ambao ni wahusika wakuu wa wizi wa aina zote serikalini?
Je mtu binafsi akikipa Chama fedha, fedha hiyo haihesabiwi kama source moja ya income ya chama?
Ni katika kutaja kujua tu mkuu, maana kuuliza si ujinga ila kubwatuka ndiyo.
Kagoda ni mali ya Rostam, nafirki Zitto anachotaka ksuema ni kesi iende kwenye sheria maana itaibua mengi sana, lakini sio siri kwamba Kagoda ni ya Rostam.
Hata Zitto, anajua kuwa kuna mkataba wa Kagoda na BOT, uliosainiwa na Rostam kwa niaba ya Kagoda, na Mgonja kwa niaba ya Serikali.
Hata mimi ninayo copy!
Shindilia hapo hapo Mh. Zitto, hakina kwaachia wapumue hadi kielweke!
Yaani ni aibu gani mtu mzima eti walio iba ni wanachama wa CCM si CCM, kwani CCM ni ninini? si mkusanyiko wa wanachama hao hao ambao waliiba tena kwa manufaa ya chama hicho hicho??
Za mwizi zenu zimetimia.. Chiligati et al...kaa tayari
Kagoda ni mali ya Rostam, nafirki Zitto anachotaka ksuema ni kesi iende kwenye sheria maana itaibua mengi sana, lakini sio siri kwamba Kagoda ni ya Rostam.
Hata Zitto, anajua kuwa kuna mkataba wa Kagoda na BOT, uliosainiwa na Rostam kwa niaba ya Kagoda, na Mgonja kwa niaba ya Serikali.
Hata mimi ninayo copy!
Zito yupo sawa kabisa kagoda ni ccm na ccm ni kagoda.
Rostam ni mwizi aliyebarikiwa na CCM kufanikisha wizi wa mali ya umma. Zito anachofanya analiweka swala zima la kagoda hadharani na nia ya kagoda kuanzia CCm, Rostam, BOT na mgonja.
Mhesmiwa field usitishike na nani alisaini au jina la nani lilifika bank kumbuka CCM ni mkusanyiko wa watu na Rostam ni mmojawapo.
Sasa yule alipelekwa leo mahakamani itakuwaje ! kama alihusika huku na anasiri nyingi sidhani kama anaweza kutoswa namna hii siataibua haya.Mhhhhhhhhhhh hapa panasomeka kichina hizi safari za mahakamani ni kujitoa one for the team hakuna lolote.