Swali hili kamuulize Rostam Aziz aka King Maker, si yeye ndiye alitajwa na Dr Slaa kwenye orodha ya mafisadi kuwa ndiye anayemiliki Kagoda? Ningeweza kukutana nae, ambacho ningekifanya kingekuwa zaidi ya kumsuta. Na sasa anataka hitman wake Noni ndio awe gavana. Nitamshangaa Kikwete kama akiendelea kujilegeza.
Anayejua jinsi ambavyo naweza kumsogelea Rostam kwa karibu awanishauri kidogo kwenye ashabdala@yahoo.com, halafu hayo mengine nitajua mwenyewe cha kufanya.
Dawa ya mafisadi ni kuwapata kwenye ule ufisadi mwingine tu.
Asha
SI KWELI MWANAKIJIJI,hatujashindwa ila sisi wananchi hatujaamua, ama hatuko tayari, au tunaogopa au hatujui la kufanya ama pa kuanzia, kumpa mtu mwingine chako akiendeshe na akakiendesha kwa uaminifu ni nadra sana kutokea. sisi watanzania tunakawaida ya kusubiri kufanyiwa mapinduzi sio kuyaanzisha wenyewe. na kikubwa nachoweza kusema ni kwamba wanaowekwa kuendesha sehemu nyeti za nchi ama kulinda mali za nchi si wanaostahili kuwapo hapo ndio maana hawa wanaharibu na wasipokaa wanaostahaili na wenye uchungu tutaendelea kulia na kusema bila effect yoyote.hata hao wazungu unaotaka waje kutushikia ama kutufanyia pia watachuma nao na mwisho tutabakizwa weupe peeeeee.Benki Kuu inahitaji ifumuliwe kabisa. Pesa tunazowalipa tuwaombe wazungu waje kutuendeshea maana tumeshindwa. Nina uhakika wazungu hawa wana uchungu na benki yetu kuliko hawa waswahili wenzetu. Hivi ni kwanini wanafikiri sisi sote ni mazezeta?
Umekumbuka nini mkuu.Hatari sana...